Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Huduma hazitakiwi kufuatwa, huduma zinatakiwa zipelekwe walipo watu.

Ndio maana huwa mna chuki na wachaga wenzenu wilaya zao zote wanajitoshereza mpaka vijijini unskunywa maji ya bomba na wana umeme na lami na hawajawahi kutowa Rais Mchaga.
Mkuu Matola waambie hao wanaodhani kuwa maendeleo yao yataletwa na kugawa mikoa yao, wilaya zao, tarafa zao au kata zao, kwa maana ya kuzigawa na kuunda nyingi zaidi.
Kinachotakiwa ni kuwa pesa zitumike kupeleka maendeleo maeneo yote, huduma za miundombinu ya barabara, elimu, maji, umeme na nyingnezo.
 
Sababu zinazotumika kuanzisha mkoa wa chato ni za kihuni na ulevi wa madaraka. Sababu hizi za kihuni zimetumika pia kujenga matawi makubwa sana ya CRDB bank na TRA, kuanzisha mbuga mpya ya wanyama, na mambo mengine CHATO, eti kisa ni nyumbani kwa kiongozi mkuu. Kwanini na Lupaso usiwe mkoa, kwanini huko Rufiji kwa mzee mwingi kusiwe mkoa, kwani Msoga sio Wilaya? Kwanini hakuna mkoa wa butiama?
 
Kwa lugha nyingine wanasema kuwa Bwana Bigambo alikuwa anajaribu kumsingizia marehemu 😀
 
Si kweli, kuwa hilo ndilo litakuwa suluhisho pekee...

Kama ndivyo, wako ktk mkoa wa Geita. Kwanini mkoa wa Geita usiilee miradi hiyo kama ndiyo hoja yako?

Sikiliza bwana. Hizi ndizo athari ya maamuzi ya upendeleo maana ukipotea wewe uliyekuwa na maamuzi ya kujipendelea, watakaokuja baada watafuta ujinga huo na hivyo kuwaachia taabu na mahangaiko wanao...!

Watoto wa Magufuli, wana CHATO pambaneni na athari za maamuzi mabaya ya baba yenu. Msitafute mtu wa kuwasaidia unless mmugeukie Mungu muumba na kuomba toba kwa niaba ya baba yenu...
 
Mkoa ukigawanywa makao makuu yawe Lusahunga ili hizo huduma ziwe karibu na wananchi wote, Chato, Kakonko na Ngara. Kuweka makao makuu Chato ni kuwaonea wengine na mantiki ya kusogeza huduma kwa wananchi inakuwa haipo.
Majadiliano katika muktadha huo sio mbaya ni jambo na mjadala.
 
Dah!...kazi kweli kweli.... anyway sababu zao zina ukweli.
 
"Huyo Bigambo aliyasema hayo kama utani tu kwa Jamii ya Wahaya" alisikika akisema mlevi mmoja wa rubhisi pale Nyakanyasi.
 
Sikubaliani na hoja hii. Mgawanyo wa Mikoa haufuati kabila linaloishi eneo hilo. Kwa mantiki hiyo tungekuwa na Mkoa wa Moshi kwa ajili ya Wachagga na Mkoa wa Same kwa ajili ya Wapare.
 
4.1 (iii) hii ni point ya msingi sana. Lazima tuwe makini na Bahima empire.
 
Hawa majamaa watatu walioshindwa kutetea majimbo yao hawawezi kuwa wasemaji wa wilaya za biharamulo na ngara. Mustakabali wa biharamulo na ngara upo mikononi mwao maana wao ndo wanajua shida ya kusafiri umbali mrefu kuja Bukoba
 
Wangepinga na uchaguzi fake uliowapa ubunge.

Maadamu walimpenda Jiwe, wapende na makandokando yake yaliyotufikisha hapa leo hii.

Na hapa CCM ndio mjue madhara ya hii katiba mbovu si kwa wapinzani tu.
Yaani ma-ccm bana yanashindwa kutatua matatizo majimboni kwao yanaongelea vitu visivyo na manufaa
 
Wana kagera msikubali mnaamishwa chato, huko ni kuharibu historia ya mkoa wenu ilianza kumegwa biharamulo na sasa ngara, kisa interest za kiongozi mubinfasi.

Nawaona wahaya kwa mbuli zenu
 
Kumbe wabunge wa Bukoba, nilifikiri wabunge wa Ngara na Biharamulo maeneo yanayopendekezwa kumegwa...nyie wahaya acheni ubinafsi mnajidai leo ndio mnazithamini Ngara na Biharamulo pathetic!
Wala usiwaseme Wahaya hiyo mijamaa mitatu haiwezi kuwa wasemaji wa Wahaya, wawaache biharamulo na ngara waamue mambo yao.
Hata hivo ukiacha biharamulo na ngara bado wabunge wa Bukoba manispaa, misenyi, Karagwe na kyerwa hawamo katika upuuzi huo.
 
Labda wangekuwa wabunge wa ngara na biharamulo ila hao wengine ni porojo tu haitabadilisha kitu chochote maana hoja zao ni dhaifu
 
Mwl JK Nyerere amezikwa Butiama kwanini hawakuipandisha hadhi na kuwa mkoa?
Mkuu kuna mtu (Sukumagang) nilimuuliza ni kwanini adhimisho ni la JK Nyerere lakini mashada yaliwekwa Chato akaniambie kule ndo kuna "kaburi la taifa".

Ujue tatizo ni kuwa nchi yetu ina maskini wengi wa akili na kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…