Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

NDIYO,wameapishwa,ile exposure yao waliyokuwa nayo bunge lililopita hawatakuwa nayo tena,wakifanya umachachari tena itakuwa ni maigizo tu.Hizi siasa ni sanaa tu zilizojaa hadaa na ghiliba nyingi
 
Sasa unamtangazia nani kukujua tu hatukujui hilo tangazo lako lina impact gani kwa wananzengo na hata CHADEMA?
 
Mnyika Naye anatakiwa apate uteuzi wa mh Raisi .Lissu lazima ashike adabu
 
makamanda wanakamsemo kao kakujifariji"upinzani sio mtu bali upinzani upo kwenye mioyo ya watu"
hao watu wenyewe sasa,ndo hawa wakina,Mbowe,Mnyika,Mdee ambao wanafika Price tag kwamabaki ya chenji ya manunuzi ya mboga sokoni.
 
Kama CHADEMA ingegomea wabunge wake kuingia bungeni ingekula kwao mara 2.

Kuwapeleka bungeni akina Halima, Esther Bulaya, Pareso na Matiko kutakipasha moto kiporo cha chadema. Bunge la safari hii litakuwa live hivyo CHADEMA itaendelea kuwemo kwa masikio na macho ya watanzania. Chama kitapata ruzuku ya kuendeshea chama na wabunge 20 watapata riziki pamoja na kupata uwezo wa kukichangia chama.

Tangu chaguzi za mwaka 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 wapinzani walikuwa wakiilalamikia tume kwa kushindwa kwao lakini hatujaacha kuingia bungeni, hata 2020 wacha twende bungeni pia kwakuwa mazingira ya uchaguzi yanafanana tu nyakati zote, na wakati wote huo hatukufanya lolote tofauti ili kuoata tume huru.
 
Huyu jamaa alikuwa, hapa na rejea uteuzi wa edo 2015 alipinga ila ndio hivyo mwenye sakosi yake akameza ndoano naamini ataendelea kuwa katika misingi yake ila mazingira anayofanyia kazi kwa sasa ni magumu sana.
 
Ndugu zangu,

Nimeona nitoe ushauri tu kwa mdogo wangu John Mnyika kuwa sasa anatakiwa ang'atuke kwani BAWACHA wamemzidi nguvu.

Ni dhahiri Halima Mdee ana baraka za "mwamba" Freeman Mbowe.

Kwa ufupi tu jiweke pembeni na CHADEMA.
Naunga mkono hoja
P
 
Hivi kwa mfano chadema wasingepata mbunge hata mmoja

But Lisu angekuwa ameshinda urais je asingekwenda kuapa?
Kuna watanzania akili hawana...Lissu alishasema akishindwa kihalali atakubali au wewe kiziwi
 
Kaanza hotuba kwa kumshukuru Mwenyekiti wake Freeman Aikael Mbowe

Halima akimaliza miaka hii mitano atakuwa ndio Mbunge wa Upinzani aliekuwa Mbunge kwa miaka 20 mfululizo

Nimefarijika sana huyu Binti kurudi Bungeni

Nilitangaza humu Jukwaani kumpa kura yangu jimboni Kawe dhidi ya Josephat Gwajima wa Chama changu

Nmependa sana hotuba yake ilivyokuwa ya Kitaifa zaid
Ulitegemea mbunge wa kuteuliwa aongelee jimbo?!!!!😄
 
Naona umepata mwanya wa kuichamba Chadema Kwa hili la akina Mdee. Chuki yako haikusaidii wewe kujenga taaluma yako ya uandishi wa habari. Kama kukengeuka Chadema wanafuata nyayo zako wewe unayelamba viatu vya watawala wakuchague UDC. Nyani haoni kundule
 
Halima, Esther na wenzenu.

Kwa hakika kumekuwa na maneno mengi juu yenu tuliyoyapuuza siku zote. Ilisemekana mtatusaliti kama ilivyosemekana kwa Yuda na hapa hatimaye yametimia.

Jogoo ndiyo huyo keshawika mara tatu.

Ghafla mmesahau kuwa uchaguzi 2020 uliibiwa? Mmesahau kulikuwa na wahanga wa uonevu kwenye uchaguzi huo? Nini kimewasibu?

Habari za kuwa Esther alikuwa pandikizi tokea akiwa uvcmc hazikuwa ngeni. Kwamba wengine mlikuwa wa ile jinsia pendwa ya tatu nani hakuyasikia?

Kuwatoa segerea tulihamasishana hadi wajane wasiokuwa na kitu waliuza hadi kuku kwa ajili yenu. Mkatolewa wanawake kwanza!

Leo hii mmesahau na eti sasa mashabiki wenu waliobakia ni mi-CCM na kina jingaletu?

Malipo mliyotulipa kwa yote tuliyowafanyia siku zote tukiwaona kama wenzetu, maumivu yake yatakwisha "inshallah."

Ila japo mngetuambia, "kama Yuda nini kimewasibu kutusaliti kiasi hiki?"

Je ni kweli CDM imeridhia kinyemela, uamuzi wenu au ni njaa zenu tu ndizo zilizo wapeleka huko?

Kulikoni!
 
Naona umepata mwanya wa kuichamba Chadema Kwa hili la akina Mdee. Chuki yako haikusaidii wewe kujenga taaluma yako ya uandishi wa habari. Kama kukengeuka Chadema wanafuata nyayo zako wewe unayelamba viatu vya watawala wakuchague UDC. Nyani haoni kundule
Pascal Mayalla amepoteza objectivity sababu ya chuki. Hawezi tena kufanya uchambuzi kwa weledi bila kuegemea upande
 
Back
Top Bottom