Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Hakuna aliye juu ya Chama!

Hii ni kauli ambayo CHADEMA imekuwa ikiitoa mara nyingi sana pindi panapotokea mtanzuko ndani ya chama unaohusisha nidhamu, taratibu na maslahi ya chama.

CHADEMA ilitoa kauli hiyo alipofukuzwa Zitto, Kitila, Mwigamba akina Silinde na hata walipohama watu wazito waliofanya kazi kubwa ya kuijenga CHADEMA enzi za uchanga wake.

Miongoni mwa vitu vilivyowavutia wananchi kuhusu CHADEMA ni uwezo wa kusimamia nidhamu za wanachama wake hata viongozi, kuibua na kukemea ufisadi kwa hoja nzito n. k

Ndugu Mbowe, majuzi uongozi wa CHADEMA ulitoa kauli kwenye press conference kuhusu kinachoitwa "uchaguzi" uliofanyika majuzi. Uongozi ulikataa katakata kutambua matokeo ya uchafuzi huo, kwa sababu kwa vigezo vyote ule siyo uchaguzi, ni uchafuzi wa kutisha, ni udhalimu usio na haya, kiufupi ni matusi ya nguoni kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!. Ni aibu!

Kwenye press hiyo, Mwenyekiti ulitamka wazi kuwa hamuutambui uchafuzi huo na Mkaenda mbele zaidi na kuonyesha baadhi ya karatasi za kura feki mlizofanikiwa kuzipata.

Sasa ndugu Mwenyekiti wananchi tunangoja Chama kichukue hatua, na hii hatua siyo ya kumuangalia nyani usoni lazima watu wawajibishwe!

Haiwezekani kuna watu wamesacrifice kwa ajili ya nchi halafu baadhi yao wananyatia kama fisi ili kudaka mfupa wa juhudi za watu waliogenuine kwa sababu ya ubinafsi uliokithiri!

Mwenyekiti Chama kichague moja, kiwe na double standard kwenye kushughulikia nidhamu za wanachama waliokiuka miongozo ya chama ili kiendelee kuheshimika na kuaminiwa na umma au kizuge, kitupige changanya la macho kwa kuendelea kuwakumbatia hawa wasaliti wakubwa wa wananchi!

Ndugu Mwenyekiti, CHADEMA itaaminika vipi kama hadharani wanatoa kauli X kumbe ikiwa sirini huenda ina misimamo Y?

Ndugu Mwenyekiti nakuomba sana, fukuza huyo Mwenyekiti wa baraza la Wanawake nchini Halima Mdee, mtu aliyepewa dhamana kubwa na wanawake lakini ameshindwa kulinda imani hii ya mamilioni ya wanawake Tanzania nzima!. Ameshindwa kuweka mbele maslahi ya vizazi na vizazi vyao kwa kukataa kutoungana na madhalimu na badala yake ameamua kuwapa legitimacy ya kisiasa kwa kuungana nao katika vikao vya dhulma dhidi ya demokrasia pana tunayoitafuta

Ndugu Mbowe, hii tuliyokuwa nayo ni turning moment kwenye historia ya chama , Mna option ya kuungwa mkono mara dufu kwa kuonyesha zero tolerance dhidi ya usaliti na kutoheshimu vikao vya chama, au muanze safari ya kuserereka kuelekea kupoteza imani kabisa kwa wananchi.

Na Magufuli anajua, njia pekee ya kuiangusha CHADEMA ni divide and rule kwamba walambishe pipi hawa kisha kaa pembeni uwasikilizie na wale waliobaki wanasemaje!

Pia Magufuli anatafuta legitimacy ndani ya nchi na nje ya nchi kwa udi na uvumba, The only way ya kujitoa kikaangoni ni kudiscredit madai yetu ya uchaguzi feki na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Na njia mojawapo ya kufanikisha hilo mosi ni kupunguza sauti za kuzidai kupitia njia hiyo ya "kurusha fupa", wale watakaokamatia fupa watang'ang'ana na fupa huku wakimuacha aende zake. Pili anawademoralize wale ambao hawatakubaliana na mambo yake kuendelea kudai uchaguzi ulikuwa feki. Tatu anatuma message kwa wahisani na wanaoinyooshea kidole Tanzania kuhusu haki za binadamu kuwa tazama, mbona kwetu mambo shwari, mnaowatetea mbona wamekubali, nyie mna tatizo gani?

Sasa ndugu Mbowe, nakuomba, kama uko real, na kama uongozi wa CHADEMA hauko nyuma ya huu ujinga, Fukuza uanachama wanawake wote hao 19 ili kutunza imani ya wananchi na wanachadema wote.

Najua, Umetoka mbali na akina Halima, mnaweza kuwa ni marafiki wakubwa, lakini maslahi mapana ya nchi na CHADEMA hayawezi kulindwa na kitendo walichokifanya.

Muweke pembeni kwa ajili ya kulinda principle na urafiki wenu uendelee nje ya shughuli za chama. Ukikosea principle this time, hiyo principle itakuja kwa namna nyingine ikuvunje!

Kama wameenda kwa baraka za uongozi wa CHADEMA tunaomba uongozi mzina na uliojihusisha na ujinga huo ujiuzulu mara moja.

Ila kama wamekiuka masharti ya vikao vya chama kwa kula njama kuhujumu maamuzi ya chama kwa ajili ya maslahi yao binafsi, basi fukuza uanachama wote hao, chama kitaendelea kusonga mbele na wao wataendelea kubaki na ubunge wao wanaoupenda sana kuliko future ya nchi, na maisha yataendelea!

Ndugu Mwenyekiti, usaliti lazima uendane na gharama kubwa, mkiuacha usaliti huu basi hiyo ni precedence itakayokuwa ikitekelezwa na wajao ambao katika juncture muhimu ya struggle za chama watanunuliwa na kufanya usaliti wao wakijua hakuna consequence yoyote ya usaliti.

Mwenyekiti, Katibu na kamati kuu ya CHADEMA, the ball is in your court, mkifunika kombe, basi mtageuka nyie wanaharamu. Washughulikieni hawa wasaliti ili chama kizidi kupata heshima na kiwe imara zaidi!
 
Naona umepata mwanya wa kuichamba Chadema Kwa hili la akina Mdee. Chuki yako haikusaidii wewe kujenga taaluma yako ya uandishi wa habari. Kama kukengeuka Chadema wanafuata nyayo zako wewe unayelamba viatu vya watawala wakuchague UDC. Nyani haoni kundule
Pascal Mayalla ni affande mwenye uzalendo kwa nchi yake!
 
Safi Wananchi hatutaki kigeugeu kama ni pesa acha CCM wawe nazo lakini mbaki na utu wenu. Chadema mko kwenye mioyo ya watu kama hao hawana nataka ya Chama. Sukuma nje kumbukeni Wana chama wako Kama milioni sita kwa mujibu wa takwimu zenu .laki mnazaidi ya mashabiki milioni ishirini .wito .Simameni Imara.wananchi tunatarajia maamuzi yenye busara kwa mstakabari wa siasa za upinzani Tanzania.
 
Safi .Wananchi hatutaki kigeugeu.kama ni pesa acha CCM wawe nazo lakini mbaki na utu wenu. Chadema mko kwenye mioyo ya watu.kama hao hawana nataka ya Chama.SuKuMa nje.kumbukeni Wana chama wako Kama milioni sita kwa mujibu wa takwimu zenu .laki mnazaidi ya mashabiki milioni ishirini .wito .Simameni Imara.wananchi tunatarajia maamuzi yenye busara kwa mstakabari wa siasa za upinzani Tanzania.

Mwalimu aliwaita wanasiasa aina ya Halima, Bulaya, Matiko na wengineo wa aina hiyo kuwa ni wanasiasa malayamalaya, wako tayari kuuza utu, dhamana na imani waliyopewa na umma kwa vijipesa!.

Watu wa aina hiyo hawastahili heshima hata kidogo!

Natambua wamewahi kuumizwa, kuwekwa jela n. k. Kumbe walikuwa wakitafuta shibe yao tu wakakutana na hiyo zahma, ila hawakuwa real hata kidogo!
 
Hakuna aliye juu ya Chama!
Hii ni kauli ambayo CHADEMA imekuwa ikiitoa mara nyingi sana pindi panapotokea mtanzuko ndani ya chama unaohusisha nidhamu, taratibu na maslahi ya chama...
Hongera sana mkuu umetoa angalizo Zuri sana. ndani ya Chama ni lazma wawepo masnitch..!! Upepo huu utapita magugu yatakaa pembeni tu.
 
Pascal Mayalla hana njaa bwashee ana kampuni yake ya matangazo.

Ni kama tu Mtei alivyo na kampuni ya Chadema na kuwaajiri ninyi!
Alikuja kulia njaa hapa mpaka akanyooka,akaenda kutubu na akasamehewa!Ule mrija wa ulaji uliokuwa umekatwa ukaunganishwa,sasa ni tumbo kwanza akili na maarifa baadaye!

Tafuta uzi uko humu JF,kimradi chake kilipigwa pini na serikali ndio akanyooka!
 
Kutoka kifungoni lazima ujisurubu na ujidhalilishe mwenyewe tena wazi wazi, huyu ndugu yangu alijua kumhoji mkuru swali aliloona litampa umaarufu kupitia tasnia alijua baada ya kutoka ukingo wa mto yordani basi atakuwa heavy journalist in industry.

Bahati mbaya kwenye madarasa ya kufundishia journalist ethics hawafundishi kila kitu bali ni kile unachokwenda kukutana nacho na kupata uwezo ufanye nini kukikabili kiuandishi.

Mbali na hilo journalist kujiona ni sehemu ya muhimili ilimpa kifua ambacho hakujua muhimili wenye nguvu unaweza kufanya lolote kuliko wewe.

👉Tumuonee huruma akumbukwe ili atulie.
 
Pascal Mayalla anatetea maslahi mapana ya Taifa. Pascal Mayalla kwake Taifa ni CCM, na CCM ndio taifa.
CHADEMA kwa jicho la Pascal Mayalla ni maadui wa taifa, wajinga, wazembe na wasiotakiwa kuwepo kwenye ramani ya nchi
Kwa jinsi mambo yalivyo ni sawa tu akifanyacho. Yanini kujikosesha ulaji kupagania lichama ambalo kumbe waliomo nao wagangaa njaa. Najiuliza wale vijana mia 200 waliokamatwa kwa kutaka kuandama wanajisikiaje sasa!

Nasemaje ukipata nafasi ya kula we kula tu, haya mambo ya kujiunga kwenye harakati bila kujua unaowaunga mkono wana lengo gani hasa utakuja kuumia sana.
 
Mwacheni mzee wangu atoe mawazo yake, halafu usisahau kwamba yeye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Alikuja kulia njaa hapa mpaka akanyooka,akaenda kutubu na akasamehewa!Ule mrija wa ulaji uliokuwa umekatwa ukaunganishwa,sasa ni tumbo kwanza akili na maarifa baadaye!
Tafuta uzi uko humu JF,kimradi chake kilipigwa pini na serikali ndio akanyooka!
Acha ajikoshe tu maana unakaza unakufa njaa ukiamini katika chama kumbe wale unaoamini na wao wana njaa kama akina Halima Mdee. Kama ukipata ulaji kula tu. Yani kama mtu kakaa bungeni miaka 10, anaona kukosa ubunge miaka 5 atakufa njaa anasaliti, kwanini wengine wakaze ambao wana mshahara hata haufiki milioni. Hapa ni mwendo wa kusifu juhudi tu
 
Mleta mada mbona unaikomalia sana Chadema kaanzishe chama chako uka implement hayo mawazo yako koko kama huridhiki

Eti last last chance kwenda huko
 
Naona umepata mwanya wa kuichamba Chadema Kwa hili la akina Mdee. Chuki yako haikusaidii wewe kujenga taaluma yako ya uandishi wa habari. Kama kukengeuka Chadema wanafuata nyayo zako wewe unayelamba viatu vya watawala wakuchague UDC. Nyani haoni kundule

Usimuonee Paschal, hamchukii mtu, anaichukiaz njaa yake!
 
Kwani Siasa ni nini?

Hili somo nadhani Serikali ilokosea Sana kuliondoa mashuleni

Na hii Ndiyo athari insyoanza kukitokeza, na ndiyo matokea ya kuuwawa Kwa watu wengi mashabiki wa siasa tofauti na wanasiasa wenyewe

Nje ya siasa mna chili, ndani ya siasa ni urafiki tupu, Chadema na CCM nje ni maadui lakini ndani Kwa ndani ni kulwa na dotto
 
Back
Top Bottom