Hakuna aliye juu ya Chama!
Hii ni kauli ambayo CHADEMA imekuwa ikiitoa mara nyingi sana pindi panapotokea mtanzuko ndani ya chama unaohusisha nidhamu, taratibu na maslahi ya chama.
CHADEMA ilitoa kauli hiyo alipofukuzwa Zitto, Kitila, Mwigamba akina Silinde na hata walipohama watu wazito waliofanya kazi kubwa ya kuijenga CHADEMA enzi za uchanga wake.
Miongoni mwa vitu vilivyowavutia wananchi kuhusu CHADEMA ni uwezo wa kusimamia nidhamu za wanachama wake hata viongozi, kuibua na kukemea ufisadi kwa hoja nzito n. k
Ndugu Mbowe, majuzi uongozi wa CHADEMA ulitoa kauli kwenye press conference kuhusu kinachoitwa "uchaguzi" uliofanyika majuzi. Uongozi ulikataa katakata kutambua matokeo ya uchafuzi huo, kwa sababu kwa vigezo vyote ule siyo uchaguzi, ni uchafuzi wa kutisha, ni udhalimu usio na haya, kiufupi ni matusi ya nguoni kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!. Ni aibu!
Kwenye press hiyo, Mwenyekiti ulitamka wazi kuwa hamuutambui uchafuzi huo na Mkaenda mbele zaidi na kuonyesha baadhi ya karatasi za kura feki mlizofanikiwa kuzipata.
Sasa ndugu Mwenyekiti wananchi tunangoja Chama kichukue hatua, na hii hatua siyo ya kumuangalia nyani usoni lazima watu wawajibishwe!
Haiwezekani kuna watu wamesacrifice kwa ajili ya nchi halafu baadhi yao wananyatia kama fisi ili kudaka mfupa wa juhudi za watu waliogenuine kwa sababu ya ubinafsi uliokithiri!
Mwenyekiti Chama kichague moja, kiwe na double standard kwenye kushughulikia nidhamu za wanachama waliokiuka miongozo ya chama ili kiendelee kuheshimika na kuaminiwa na umma au kizuge, kitupige changanya la macho kwa kuendelea kuwakumbatia hawa wasaliti wakubwa wa wananchi!
Ndugu Mwenyekiti, CHADEMA itaaminika vipi kama hadharani wanatoa kauli X kumbe ikiwa sirini huenda ina misimamo Y?
Ndugu Mwenyekiti nakuomba sana, fukuza huyo Mwenyekiti wa baraza la Wanawake nchini Halima Mdee, mtu aliyepewa dhamana kubwa na wanawake lakini ameshindwa kulinda imani hii ya mamilioni ya wanawake Tanzania nzima!. Ameshindwa kuweka mbele maslahi ya vizazi na vizazi vyao kwa kukataa kutoungana na madhalimu na badala yake ameamua kuwapa legitimacy ya kisiasa kwa kuungana nao katika vikao vya dhulma dhidi ya demokrasia pana tunayoitafuta
Ndugu Mbowe, hii tuliyokuwa nayo ni turning moment kwenye historia ya chama , Mna option ya kuungwa mkono mara dufu kwa kuonyesha zero tolerance dhidi ya usaliti na kutoheshimu vikao vya chama, au muanze safari ya kuserereka kuelekea kupoteza imani kabisa kwa wananchi.
Na Magufuli anajua, njia pekee ya kuiangusha CHADEMA ni divide and rule kwamba walambishe pipi hawa kisha kaa pembeni uwasikilizie na wale waliobaki wanasemaje!
Pia Magufuli anatafuta legitimacy ndani ya nchi na nje ya nchi kwa udi na uvumba, The only way ya kujitoa kikaangoni ni kudiscredit madai yetu ya uchaguzi feki na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Na njia mojawapo ya kufanikisha hilo mosi ni kupunguza sauti za kuzidai kupitia njia hiyo ya "kurusha fupa", wale watakaokamatia fupa watang'ang'ana na fupa huku wakimuacha aende zake. Pili anawademoralize wale ambao hawatakubaliana na mambo yake kuendelea kudai uchaguzi ulikuwa feki. Tatu anatuma message kwa wahisani na wanaoinyooshea kidole Tanzania kuhusu haki za binadamu kuwa tazama, mbona kwetu mambo shwari, mnaowatetea mbona wamekubali, nyie mna tatizo gani?
Sasa ndugu Mbowe, nakuomba, kama uko real, na kama uongozi wa CHADEMA hauko nyuma ya huu ujinga, Fukuza uanachama wanawake wote hao 19 ili kutunza imani ya wananchi na wanachadema wote.
Najua, Umetoka mbali na akina Halima, mnaweza kuwa ni marafiki wakubwa, lakini maslahi mapana ya nchi na CHADEMA hayawezi kulindwa na kitendo walichokifanya.
Muweke pembeni kwa ajili ya kulinda principle na urafiki wenu uendelee nje ya shughuli za chama. Ukikosea principle this time, hiyo principle itakuja kwa namna nyingine ikuvunje!
Kama wameenda kwa baraka za uongozi wa CHADEMA tunaomba uongozi mzina na uliojihusisha na ujinga huo ujiuzulu mara moja.
Ila kama wamekiuka masharti ya vikao vya chama kwa kula njama kuhujumu maamuzi ya chama kwa ajili ya maslahi yao binafsi, basi fukuza uanachama wote hao, chama kitaendelea kusonga mbele na wao wataendelea kubaki na ubunge wao wanaoupenda sana kuliko future ya nchi, na maisha yataendelea!