Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na kisa cha asiyefanya kazi na asile

Alikuja kulia njaa hapa mpaka akanyooka,akaenda kutubu na akasamehewa!Ule mrija wa ulaji uliokuwa umekatwa ukaunganishwa,sasa ni tumbo kwanza akili na maarifa baadaye!
Tafuta uzi uko humu JF,kimradi chake kilipigwa pini na serikali ndio akanyooka!
Toba ni tendo la kiungwana!
 
Ungejua, usingepoteza muda wako kuandika maelezo mareeeeeefu kwa kitu usichokijua.

Pole sana kijana.
 
Ni kauli au misimamo mingapi ilishawahi kutolewa alafu baadaye kukawa na maridhiano?? Kauli siyo misahafu au maandiko matakatifu. Muhimu kuliko zote ni UTAIFA KWANZA, nyie endeleni na majungu, fitna za kwenye mitandao lakini kuna wananchi huku vijijini wamefurahia sana kitendo cha wabunge wa viti Maalum wa chadema. That's WIN WIN situation.
 
Mleta mada mbona unaikomalia sana Chadema kaanzishe chama chako uka implement hayo mawazo yako koko kama huridhiki

Eti last last chance kwenda huko
Mbona wewe huwa unaikomalia sana chadema kwanini usidili na CCM yako
 
Safi .Wananchi hatutaki kigeugeu.kama ni pesa acha CCM wawe nazo lakini mbaki na utu wenu. Chadema mko kwenye mioyo ya watu.kama hao hawana nataka ya Chama.SuKuMa nje.kumbukeni Wana chama wako Kama milioni sita kwa mujibu wa takwimu zenu .laki mnazaidi ya mashabiki milioni ishirini .wito .Simameni Imara.wananchi tunatarajia maamuzi yenye busara kwa mstakabari wa siasa za upinzani Tanzania.
Hao malaya 20 wakisiasa wafutwe wote uanachama
 
Hakuna aliye juu ya Chama!

Hii ni kauli ambayo CHADEMA imekuwa ikiitoa mara nyingi sana pindi panapotokea mtanzuko ndani ya chama unaohusisha nidhamu, taratibu na maslahi ya chama..

Kitendo walichofanya akina Halima hakisameheki na kufukuzwa ndani ya chama ndio haki pekee tunayoisubiria na kama sio hivyo basi tugawane fito kama CUF walivyofanya Mbowe abaki na akina dada wake na Tundu Lissu aondoke na kundi lake lenye msimamo ulionyooka
 
Ni kauli au misimamo mingapi ilishawahi kutolewa alafu baadaye kukawa na maridhiano?? Kauli siyo misahafu au maandiko matakatifu. Muhimu kuliko zote ni UTAIFA KWANZA, nyie endeleni na majungu, fitna za kwenye mitandao lakini kuna wananchi huku vijijini wamefurahia sana kitendo cha wabunge wa viti Maalum wa chadema. That's WIN WIN situation.
Utaifa siyo kuiba kura za wananchi kisha mkagawana nyadhifa!. Utaifa ni kuheshimu wananchi, siyo kupozana kwa vyeo/nafasi

Kuiba uchaguzi ni kama Uhaini, na Uhaini ndiyo kosa la juu kabisa katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania!
 
Hongera sana kwa andiko zuri MKUU MISSILE of the nation.

JIWE AMETUMIA PRINCIPLE YA DEVIDE AND LURE KUIANGAMIZA CHADEMA.

# hakika hakuna umoja mbele ya njaa anapojitokeza mwenye chakula.

VIONGOZI WA JUU WA CHAMA WAMEWASALITI WANANCHI.

1.watu walichanga fedha za kuwatoa hadi Jela
2. watu wamepotezwa kwa ajili ya CHADEMA.
3. watu wamekufa kwa ajili ya CHADEMA.
4.Watu wametekwa, wamefilisiwa, wamepata ulemavu nk.

HUU NI USALITI MKUBWA SANA KWA WATANZANIA MBOWE UMETUSALITI WATANZANIA.
 
Utaifa siyo kuiba kura za wananchi kisha mkagawana nyadhifa!. Utaifa ni kuheshimu wananchi, siyo kupozana kwa vyeo/nafasi

Kuiba uchaguzi ni kama Uhaini, na Uhaini ndiyo kosa la juu kabisa katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania!
Ulimsikia huyo unayemwamini "LISU" akiwa Ubelgiji akiomba maridhiano?? Kwenye siasa hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya! Usiteseke wala kusononeka sana ukapata magonjwa ya presha bure kisa siasa! Kilichofanyika Jana kina baraka zote za uongozi wa chadema pamoja na mgombea wake Lisu, ila siyo kila kitu kinawekwa wazi. Uchaguzi umeisha, viti maalum tayari.. endelea kuchapa kazi.
 
Ulimsikia huyo unayemwamini "LISU" akiwa Ubelgiji akiomba maridhiano?? Kwenye siasa hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya! Usiteseke wala kusononeka sana ukapata magonjwa ya presha bure kisa siasa! Kilichofanyika Jana kina baraka zote za uongozi wa chadema pamoja na mgombea wake Lisu, ila siyo kila kitu kinawekwa wazi. Uchaguzi umeisha, viti maalum tayari.. endelea kuchapa kazi.
Maridhiano maana yake ni talks (mazungumzo) yanazozaa muafaka wenye manufaa kwa Taifa na wadau na society nzima, kuanzia civil organisations zao, vyaa vyama vya siasa, juuia za kidini n. k na miongoni mwa vitu vya kujadiliana katika hayo maridhiano ni kwa mfano

1. Uwepo wa tume huru ya uchaguzi
2. Katiba mpya
3. Kufungulia wafungwa wa kisiasa
4. Kuheshimu haki za vyama kufanya siasa kwa mujibu wa sheria

Haimaanishi kugawana vyeo au nyadhifa na kisha mambo yaendelee vilevile business as usual!

Muelewe Lissu, ile ni akili kubwa
 
Hakuna aliye juu ya Chama!

Hii ni kauli ambayo CHADEMA imekuwa ikiitoa mara nyingi sana pindi panapotokea mtanzuko ndani ya chama unaohusisha nidhamu, taratibu na maslahi ya chama.

CHADEMA ilitoa kauli hiyo alipofukuzwa Zitto, Kitila, Mwigamba akina Silinde na hata walipohama watu wazito waliofanya kazi kubwa ya kuijenga CHADEMA enzi za uchanga wake.

Miongoni mwa vitu vilivyowavutia wananchi kuhusu CHADEMA ni uwezo wa kusimamia nidhamu za wanachama wake hata viongozi, kuibua na kukemea ufisadi kwa hoja nzito n. k

Ndugu Mbowe, majuzi uongozi wa CHADEMA ulitoa kauli kwenye press conference kuhusu kinachoitwa "uchaguzi" uliofanyika majuzi. Uongozi ulikataa katakata kutambua matokeo ya uchafuzi huo, kwa sababu kwa vigezo vyote ule siyo uchaguzi, ni uchafuzi wa kutisha, ni udhalimu usio na haya, kiufupi ni matusi ya nguoni kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!. Ni aibu!
Kwenye press hiyo, Mwenyekiti ulitamka wazi kuwa hamuutambui uchafuzi huo na Mkaenda mbele zaidi na kuonyesha baadhi ya karatasi za kura feki mlizofanikiwa kuzipata.

Sasa ndugu Mwenyekiti wananchi tunangoja Chama kichukue hatua, na hii hatua siyo ya kumuangalia nyani usoni lazima watu wawajibishwe!

Haiwezekani kuna watu wamesacrifice kwa ajili ya nchi halafu baadhi yao wananyatia kama fisi ili kudaka mfupa wa juhudi za watu waliogenuine kwa sababu ya ubinafsi uliokithiri!
Mwenyekiti Chama kichague moja, kiwe na double standard kwenye kushughulikia nidhamu za wanachama waliokiuka miongozo ya chama ili kiendelee kuheshimika na kuaminiwa na umma au kizuge, kitupige changanya la macho kwa kuendelea kuwakumbatia hawa wasaliti wakubwa wa wananchi!

Ndugu Mwenyekiti, CHADEMA itaaminika vipi kama hadharani wanatoa kauli X kumbe ikiwa sirini huenda ina misimamo Y?

Ndugu Mwenyekiti nakuomba sana, fukuza huyo Mwenyekiti wa baraza la Wanawake nchini Halima Mdee, mtu aliyepewa dhamana kubwa na wanawake lakini ameshindwa kulinda imani hii ya mamilioni ya wanawake Tanzania nzima!. Ameshindwa kuweka mbele maslahi ya vizazi na vizazi vyao kwa kukataa kutoungana na madhalimu na badala yake ameamua kuwapa legitimacy ya kisiasa kwa kuungana nao katika vikao vya dhulma dhidi ya demokrasia pana tunayoitafuta

Ndugu Mbowe, hii tuliyokuwa nayo ni turning moment kwenye historia ya chama , Mna option ya kuungwa mkono mara dufu kwa kuonyesha zero tolerance dhidi ya usaliti na kutoheshimu vikao vya chama, au muanze safari ya kuserereka kuelekea kupoteza imani kabisa kwa wananchi.

Na Magufuli anajua, njia pekee ya kuiangusha CHADEMA ni divide and rule kwamba walambishe pipi hawa kisha kaa pembeni uwasikilizie na wale waliobaki wanasemaje!

Pia Magufuli anatafuta legitimacy ndani ya nchi na nje ya nchi kwa udi na uvumba, The only way ya kujitoa kikaangoni ni kudiscredit madai yetu ya uchaguzi feki na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Na njia mojawapo ya kufanikisha hilo mosi ni kupunguza sauti za kuzidai kupitia njia hiyo ya "kurusha fupa", wale watakaokamatia fupa watang'ang'ana na fupa huku wakimuacha aende zake. Pili anawademoralize wale ambao hawatakubaliana na mambo yake kuendelea kudai uchaguzi ulikuwa feki. Tatu anatuma message kwa wahisani na wanaoinyooshea kidole Tanzania kuhusu haki za binadamu kuwa tazama, mbona kwetu mambo shwari, mnaowatetea mbona wamekubali, nyie mna tatizo gani?

Sasa ndugu Mbowe, nakuomba, kama uko real, na kama uongozi wa CHADEMA hauko nyuma ya huu ujinga, Fukuza uanachama wanawake wote hao 19 ili kutunza imani ya wananchi na wanachadema wote.

Najua, Umetoka mbali na akina Halima, mnaweza kuwa ni marafiki wakubwa, lakini maslahi mapana ya nchi na CHADEMA hayawezi kulindwa na kitendo walichokifanya.

Muweke pembeni kwa ajili ya kulinda principle na urafiki wenu uendelee nje ya shughuli za chama. Ukikosea principle this time, hiyo principle itakuja kwa namna nyingine ikuvunje!

Kama wameenda kwa baraka za uongozi wa CHADEMA tunaomba uongozi mzina na uliojihusisha na ujinga huo ujiuzulu mara moja.

Ila kama wamekiuka masharti ya vikao vya chama kwa kula njama kuhujumu maamuzi ya chama kwa ajili ya maslahi yao binafsi, basi fukuza uanachama wote hao, chama kitaendelea kusonga mbele na wao wataendelea kubaki na ubunge wao wanaoupenda sana kuliko future ya nchi, na maisha yataendelea!
Pole ndugu yangu. Una uchungu sana. Kweli ndugu yangu lazima uumiè. Umetumia muda mwingi sana kwenye mapambano ya mitandao, oh pole bwana. Nayaona maumivu makali zaidi kwa Amsterdam na bwana yule ubavuni
 
Kama huzijui siasa za ndani ya CHADEMA unaweza kudhani kuna suala la kisiasa ambalo Halima Mdee anaweza kulifanya bila ridhaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe! Haiwezekani.

Halima Mdee ni mmoja wa watu ndani ya CHADEMA ambao ni sehemu ya Freeman Mbowe. Mwingine ni Godbless Lema na genge lake!

Kwa maana nyingine, ukimgusa kisiasa Halima Mdee unakuwa umemgusa kisiasa Mbowe! Yote anayofanya kisiasa Halima Mdee yanakuwa ni mkono wa Mbowe!

Kitu ambacho nampa hongera Mbowe ni uwezo wake wa kutumia ''wakala'' katika kutimiza malengo yake ya kisiasa. kwa wasiojua wanaweza kudhani wanapambana na ''mtu fulani'' ndani ya CHADEMA bila kujua kama wanapambana na Freeman Mbowe kwa kupitia ''wakala''.

Mbowe ndani ya madaraka anatumia nadharia inayosema, '' Always say less than necessary'' kama inavyobainishwa katika sheria ya 4 ndani ya kitabu kinachoitwa The 48 Laws of Power kilichoandikwa na Mmarekani, Robert Greene.

Kuna msema pia usemao, ''Ukiona kifaranga kipo juu ya chungu ujue chini kuna mama yake''. Hii ina maana kuwa, ukimuona Halima Mdee anatamba juu kisiasa ujue Freeman Mbowe yuko chini yake!

Ikumbukwe, Mbowe alishawahi kufanya mazungumzo ya siri ya kumleta Edward Lowassa huku kina Mdee na Lema wakijua lakini hakuwahi kumwambia Dk. Slaa mpaka mazungumzo yalipokamilika.

Hata Mashinji hakuwahi kuambiwa mapema kama nafasi yake itachukuliwa na John Mnyika lakini kina Mdee na Lema walijua mapema.

Muda ni mwalimu mzuri anayetoa mafunzo ya ukweli kwa wale wazito kujua au kung'amua ukweli wa mambo!

NB:
Kwenye sakata la kina Halima Mdee, Mbowe atasema ameamua waende bungeni kwa sababu chama hakiwezi kuwazuia wabunge wa viti maalum kwenda bungeni kwa mujibu wa katiba halafu kikaendelea kuchukua ruzuku ya serikali itokanayo na kura za wabunge ambazo zimezaa wabunge wa viti maalum!
 
Back
Top Bottom