Hivi CHADEMA mlikuwa mnatafuta kurudisha kwa wananchi nchi yao iliyoporwa na CCM au mlikuwa mnatafuta posho na marupurupu ya ubunge? Comredi Mbowe, nimekuwa ninaamini seriousness yako katika ukombozi wa Mtanzania kuliko hicho kingine, labda kama sikuwa sahihi! Kweli katika uchaguzi ule ambao hata mtoto mdogo anajua ni uchafuzi mtakubali kula ruzuku haramu? Mlikuwa mnamaanisha au mlikuwa mnadanganya umma kuwa ninyi ni watu makini?
Wewe mwenyewe ulinyanganywa Bilicanas, ukavunjiwa Green houses zako, ukachajiwa kodi kubwa pale Protea, umehatarisha maisha yako mara nyingi, umefungwa gerezani, na hayo na mengine yakafanya watu wakuamini na kuiamini Chadema. Ulikuwa unatafuta watu wawe wabunge wa kuteuliwa? Sasa kuwepo ama kufa kwa Chadema kumefika. Chaweza kufia mikononi mwako na mtaitwa wasaliti wakubwa wa matumaini ya WaTz.
Fukuza wasaka tonge wote bila kujali ni akina nani. Hawafai kabisa kuwepo katika kikosi cha ukombozi wa nchi! Eti watapewa unaibu Waziri! Kweli? Ndicho mlichokuwa mnapigania? Kweli ndicho kilisababisha Lissu akapigwa risasi zile na bado akarudi kusimama jukwaani kuleta matumaini ya kurudisha haki, uhuru, na maendeleo? Usipochukua hatua sasa ya kuonyesha msimamo, huu ndio utakuwa mwisho wa Chadema. Na itaonekana kuwa wote mlikuwa mnacheza tu bila kumaanisha. Labda Lissu tu ndiye alikuwa anamaanisha.