Wabunge wanne - Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde na Wilfred Lwakatare wafutwa uanachama wa CHADEMA

Chadema sasa sio ile ya kusimamia maadili, sio ile ya 'opersheni sangara', 'list of shame' na makamanda wa uhanarakati. Kipindi kile watu walikipenda chama na ideology yake...
Kitendo cha CHADEMA kuhama kutoka kwenye chama cha wanaharakati kwenda chama dola sio kibaya ila inaonekana some tips are missing on the whole process.

Nilitegemea kuhamia kwenye status ya chama dola kutawafanya wawe wakomavu zaidi kisiasa ikiwemo kukubaliana na fikra tofauti juu ya maamuzi ya kamati kuu (chama).

Bado CHADEMA ina safari ndefu ya kujifunza na kukomaa zaidi kifikra na kimkakati
 
Niliandika hapa siku si nyingi, kwamba chadema itaingia kwenye wiki mbili ngumu mno. Naona yameaza kutokea. Mwenyekiti anapaswa mawazo yake yawe shirikishi, huwezi kutoa maamuzi kama vile unaowaongoza ni watoto wa nursery...
Umetumia zaidi ya dakika 10 kuandika huu uchafu uliokujaa kichwani, huu muda uliopoteza ungemsaidia dada yako kuosha vyombo hapo kwa shemeji yako angekuona wa maana sana
 
Yalikuwa ni maamuzi ya mihemko. Hakutakiwa kabisa kuwafukuza uanachama. Ingekuwa ni vema zaidi kama angeonesha ukomavu kwa kukubaliana na fikra zao tofauti
 
Umetumia zaidi ya dakika 10 kuandika huu uchafu uliokujaa kichwani, huu muda uliopoteza ungemsaidia dada yako kuosha vyombo hapo kwa shemeji yako angekuona wa maana sana
Hajaandika uchafu, what he said is exactly right, na ndio maana inaonekana dhahiri kwamba itatuchukua muda mrefu sana kukomaa kisiasa
 
NCHI IPO KWENYE HARAKATI ZA KUPAMBANA NA CORONA WAO WAPO BUSY NA KUFUTA WABUNGE UANACHANA HAWA HAWANA UCHUNGU NA HILI TAIFA TUWAPUUZE WAMETUMWA NA MABEBERU
Hivi kama walishasema wanaenda upande wa pili waachwe tuu waendelee kufanya uharibu? Hivi mke wa Chuwa akamwambia Chuwa ifikapo July 2020 sitakuwa nawewe naenda kuolewa na Massawe, unataka Chuwa aendelee tuu kuishi na huyo mke hadi July 2020 amkabidhi Massawe?
 
Mkuu . . . comment yako nimeitunza. Ile CHADEMA ya uanaharakati ilitikisa sana. CHADEMA ilikua kwenye peak yake. Zinatakiwa juhudi zaidi kurudisha muziki ule katika ulimwengu wa siasa za nchi yetu
 
Mkuu umesema kabla ya 2015 walikuwa hawana vurugu? Hvi kuna vurugu zaidi ya maandamano ya Arusha 2011, au mauaji kwenye zile chaguzi ndogo ama Kupigana bungeni zaidi ya kipindi cha before 2015?

Naomba unisaidie, vurugu gani waliofanya CHADEMA awamu hii imezidi awamu ya 4!!

I'm waiting mkuu
 
Hoja sio kudiscredit ila generalisation ndio napinga.

Yaani huwezi sema wazee wa HAI wakati kuna kata kibao.

Nachopinga ni kufungamanisha maoni ya wachache kuwa ya wilaya nzima.

Ww ni msomi hvi leo niweke watu 10 hpa waseme Kichuguu ni mwizi basi habari iandikwe WATANZANIA WASEMA KICHUGUU NI WIZI!!

Hizo ni cheap propaganda za CCM, mtu ameshinda halmashauri nzima afu unamchafua kwa kelele za kijiwe kimoja cha kahawa?
 
Sasa hawa wanafukuzwa ubunge wakati bado mwezi moja tu Bunge liishe ndo nini? Lakini wahenga walisema "Alieko juu mgonje chini"
 
Hoja sio kudiscredit ila generalisation ndio napinga.

Yaani huwezi sema wazee wa HAI wakati kuna kata kibao...
Una matataizo ya uelewa; na sababu kubwa inatokana na ama kutokujua kusoma au kusoma mambo ukiwa na mindeset fulani. Wengine tumekomalia katika kusoma substance, siyo ushabiki kama unavyokomaa hapa.

Ukirudi kwenye hiyo post niliyoweka, utashangaa kuona kuwa hakukuwa na maneno yangu yanayodai unavyosema, ila kwa sababu uliisoma ukiwa na mindset fulani ndiyo maana unapiga kelel bila ushahdi wowote.

Ingawa sikumbuki nilitumia maneno gani ila ilikuwa ni kama "nimeipata hii" ndivyo nilivyoandika; unaweza kuijadili au kutioijadili. Sikusema kuwa hao wote ndio wazee wa hai, inawezekana wanawakilisha mawazo ya majority ya minority, siyo jukumu langu; tunaweza kuijadili kuliko kuidscredit on the spot.

Kama nilivyokwambia mimi sijawahi hata kufika Hai, sikupiga wala kuedit picha hiyo.

Wewe ukiona hayo usiyokubaliana nayo tu, unapata kiwewe bila hata kujua yana maana gani. Punnguza kiwewe, jenga tabia ya kutafakari mambo kabla ya kuyajibu,
 
Niliandika hapa siku si nyingi, kwamba chadema itaingia kwenye wiki mbili ngumu mno. Naona yameaza kutokea. Mwenyekiti anapaswa mawazo yake yawe shirikishi, huwezi kutoa maamuzi kama vile unaowaongoza ni watoto wa nursery...
Kma Kutimua CHADEMA ilifanya hivyo tokea zamani, kumbuka ilitimuaga madiwani 4 kwa mpigo, ilitimua kina Shonza na wenzie, ilitimua kina Zitto na wenzie... And well Slaa naye alisusa hao wote walikuwa wazito sana kuliko hawa kina Komu by far ila bado chama hakikuyumba kwa lolote huyo zitto akaambulia 1% pekee!!

Uchaguzi ukiwa huru na haki bado hakuna replacement ya CHADEMA kwa hivi vyama vingine NCCR wala ACT havina political base huku bara.

Hta kura zikiibiwa sana CHADEMA ina hakika ya kura walau million 2 hizo tu hakuna mpinzani mwingine anaweza pata.

So CHADEMA itapata viti maalum +30 so hta wakipata majimbo 10 tu wanatosha kuunda KUB.

Ssa niambie ACT/NCCR wana base ya kupata kura hta laki 2 kweli huku bara??

Siasa ni hesabu tu sio kelele za mitandaoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…