Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

Imeisha hiyo tusubiri surprise ya mkataba mwingine!
Ila hili lishapita hapa tunamsubiria mwarabu atue rasmi,
 
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa IGA ( Intergovernmental Agreement), na baada ya hapo ndipo HGA ( Host Government Agreement) zitaingiwa kati ya TPA na DPW baada ya IGA kupitishwa.

IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.

Huku mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumeisha anza kuibuka makundi sogozi yanayoleta uhayawani wa sentiments za kibaguzi, Mwarabu wa Oman anataka kumpa Bandari yetu Mwarabu wa Dubai hivyo Watanzania Wazalendo tusikubali!. Hawa ni muflis!.

Kule nyuma nilipopandisha pandisha bandiko hili Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama nilitoa angalizo hili

Angalizo hili ni muhimu sana kwenye mjadala wa leo mule Bungeni kwetu. Tunawategemea kuwasikia waheshimiwa wabunge wetu wakitanguliza mbele maslahi ya taifa letu katika kulijadili hili la DP World. Hatutarajii kabisa kutokea mbunge mmoja yoyote muflis kuipinga DP World kwa Uarabu wao, kwa hoja za kibaguzi za Mwarabu ni Mwarabu tuu, awe ni Mwarabu wa Oman, Mwarabu wa Dubai, Mwarabu wa Arabuni, Mwarabu wa Zanzibar, Mwarabu ni Mwarabu tuu ni wale wale na mambo yao ni yale yale..., watu wa type hii ni ma hayawani!, hatutegemei kabisa uhayawani huu ukaibuka kwenye mjadala huu!.

Naendelea kusisitiza, ikitokea wewe huwezi jambo fulani, lazima utasaidiwa tuu!, utake kusaidiwa, utasaidiwa, usitake kusaidiwa, utasaidiwa!, mpaka pale utakapoweza kujisaidia! Watanzania tujifunze kujikubali kuwa kuna vitu hauwezi, na tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Nawatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala na majadiliano mema kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Paskali
Paskal, kama serikali yetu imeshindwa kusimamia na kuendeleza bandari iliyopakana na Ikulu, je inaweza kusimamia uchimbaji wa Nickel kule ngara?

JPM hakuwahi kukiri kushindwa !!

Paskal Ukiona mke wako ameshindwa kukujengea nyumba ya kuishi utamwambia atafute mume mwingine Ili akujengee Wewe nyumba ya kuishi?

Nikutakie sabato njema
 
Wabunge hakuna wa kupinga hata kuleta positive challenge wanaenda kuchukua posho tu
 
Prof. Mbarawa namsikiliza ila simuelewi kabisa !
 
Hayo mambo nia aibu; hawawezi kuyaweka wazi hata siku moja maana wameshafanya ujinga
Katika hizi ngonjera na sijaskia serikali itanufaikaje kifedha. Watapata asilimia ngapi katika hio faida itokanayo na uendeshaji?
 
Wabongo wanachekesha sana
Kuna vitu vya msingi sana vinavyoathiri maisha yao moja kwa moja kama Elimu, Huduma ya Afya na Uhuru wa mahakama, ambavyo tumenyimwa waziwazi na serikali lakini wamepiga kimya na kuridhika.
Mnajibebesha kudai vitu vikubwa na kutaka kujua uendeshaji wa Bandari mara Madini,

acheni ujinga......
 
IMG-20230416-WA0018.jpg
 
Wacha tujadili mambo ya Bandari usitupotezee lengo
Naona hujapenda mama alivyoupiga mwingi. Tuendelee:

Ports and terminals are the gateways to smarter, more efficient and more secure global supply chains.

We are hard at work reimagining the future, with step-change terminal handling innovations designed to streamline our global network of ports and keep things flowing.

Smart innovations like BoxBay, our intelligent High Bay Storage (HBS) system, are disrupting business-as-usual: increasing terminal handling speed, energy efficiency and safety, while decreasing operating costs.

Looking to the future, we have invested in Virgin’s revolutionary Hyperloop technology, an advanced, on-demand, incredibly fast cargo pod system that will give cargo owners synchronised, seamless and intelligent movement of goods.

Tafsiri yake :

DP Dunia

  • Menyu
DP Dunia
Funga

Picha ya Bango

BANDARI NA VITUO​

Kufikiria upya bandari za kesho kwa wamiliki wa mizigo wa leo
Bandari na vituo ni lango la minyororo nadhifu, bora zaidi na salama zaidi ya usambazaji wa kimataifa.

Tunafanya kazi kwa bidii katika kufikiria upya siku zijazo, tukiwa na ubunifu wa ushughulikiaji wa mabadiliko ya hatua ulioundwa ili kurahisisha mtandao wetu wa kimataifa wa bandari na kudumisha mambo.

Ubunifu mahiri kama vile BoxBay, mfumo wetu mahiri wa Hifadhi ya Juu ya Ghuba (HBS), unatatiza biashara kama kawaida: kuongeza kasi ya ushughulikiaji wa wastaafu, ufanisi wa nishati na usalama, huku ukipunguza gharama za uendeshaji.

Tukiangalia siku za usoni, tumewekeza katika teknolojia ya mapinduzi ya Virgin Hyperloop, mfumo wa hali ya juu, unapohitajika, na wa haraka sana wa kubeba mizigo ambao utawapa wamiliki wa shehena upatanishi, imefumwa na usafiri wa akili wa bidhaa.
 
Kwanini Watanzania hawaliamini Bunge lao lenye wabunge waliowachagua kwa mbwembwe nyingi 2020?
2020 hakukuwa na uchaguzi. Mwendawazimu aliamua kuweka vikaragosi vya kumtengenezea utawala usio na kikomo,bahati Mungu akaingilia kati bali vimeo vyake bado vipo vinaleta usumbufu
 
Wanabodi,
Leo asubuhi hii waheshimiwa wabunge wetu, wataujadili mkataba wa IGA ( Intergovernmental Agreement), na baada ya hapo ndipo HGA ( Host Government Agreement) zitaingiwa kati ya TPA na DPW baada ya IGA kupitishwa.

IGA kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai, kuruhusu kampuni ya DP World ya Dubai, kutuboreshea Bandari zetu.

Huku mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kumeisha anza kuibuka makundi sogozi yanayoleta uhayawani wa sentiments za kibaguzi, Mwarabu wa Oman anataka kumpa Bandari yetu Mwarabu wa Dubai hivyo Watanzania Wazalendo tusikubali!. Hawa ni muflis!.

Kule nyuma nilipopandisha pandisha bandiko hili Udhalimu wa Waarabu Zanzibar na Pemba: Ndugu zetu waliteswa, hasiwa, bakwa, na kuuawa kinyama nilitoa angalizo hili

Angalizo hili ni muhimu sana kwenye mjadala wa leo mule Bungeni kwetu. Tunawategemea kuwasikia waheshimiwa wabunge wetu wakitanguliza mbele maslahi ya taifa letu katika kulijadili hili la DP World. Hatutarajii kabisa kutokea mbunge mmoja yoyote muflis kuipinga DP World kwa Uarabu wao, kwa hoja za kibaguzi za Mwarabu ni Mwarabu tuu, awe ni Mwarabu wa Oman, Mwarabu wa Dubai, Mwarabu wa Arabuni, Mwarabu wa Zanzibar, Mwarabu ni Mwarabu tuu ni wale wale na mambo yao ni yale yale..., watu wa type hii ni ma hayawani!, hatutegemei kabisa uhayawani huu ukaibuka kwenye mjadala huu!.

Naendelea kusisitiza, ikitokea wewe huwezi jambo fulani, lazima utasaidiwa tuu!, utake kusaidiwa, utasaidiwa, usitake kusaidiwa, utasaidiwa!, mpaka pale utakapoweza kujisaidia! Watanzania tujifunze kujikubali kuwa kuna vitu hauwezi, na tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Naw ftatakia waheshimiwa wabunge wetu mjadala na majadiliano mema kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Paskali
Bunge kibogoyo la majizi ya kura halina jipya. Hao watapitisha kinachotakiwa na serikali na sio kinachotakiwa na wananchi. Ifahamike hawako huko bungeni kwa kura za wananchi, bali kwa utashi wa Magufuli na serikali yake.
 
Nimemsikiliza Mbarawa hadi Sasa, ni wazi kuwa one Party is much informed than the other Party. Ni Mkataba wa kipuuzi kabisa, in short hauna manufaa yoyote zaidi ya ujanjaujanja tu. By the way, how comes utekelezaji wa mkataba uanze pasipo kuridhiwa. Professor mzima anasoma taarifa ya kipuuzi kabisa. Hauna fact zozote. Shame on him!
 
Back
Top Bottom