Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Lete la kiingereza lisilo na kiswahili chake ama lisilotoholeka. Goli (Goal) Golikipa (Gaolkeeper) Kona (Conner) Jezi (Jesey). Kama hayo yaliwezekana, hayo mengine inashindikana vipi?
Maneno tote ulivyoandika hapo yametoholewa.

Twende hili half space yup kiswahili chake.
Wachambuzi wanasaidia kuongeza msamiati wa kiingereza kwa jamii. Jambo ambalo shule haikumaliza kutupa msamiati kutokana na muktadha haukuwa kimichezo
 
Watu wa aina iyo wengi wao huwa hawaijui hiyo lugha ila anaipenda kwaiyo akidaka maneno fulani ya kingereza lazma ayaseme hata kama anazungumza na mama ntilie.

Ila kuna mwingine unakuta anaifahamu vizuri iyo lugha na anaipenda ila anakosa mahala pa kuizungumza au unaeza ita platform, sasa ni lazma achomekee maneno ya kingereza ili kuridhisha moyo lakini pia kuendelea kuifanyia mazoezi kwasababu siku zote lugha ya kigeni usipoizungumza kwa mda mrefu inakupotea.
 
Ukimkuta Boniface Pawasa anachambua ndiyo utafurahi....!! Na mmoja wa wasafi anasauti ya kijuaji hivi halafu mbishi sana, Ki ukweli inachefua.
 
Maneno tote ulivyoandika hapo yametoholewa.

Twende hili half space yup kiswahili chake.
Wachambuzi wanasaidia kuongeza msamiati wa kiingereza kwa jamii. Jambo ambalo shule haikumaliza kutupa msamiati kutokana na muktadha haukuwa kimichezo
Kwanza hiyo "Half space" ni nini. Jee kuna "Full space" na hiyo "full space" na "Half space" utofauti wake unaletwa na nini? Maana ili utohohe neno ni lazima liwe na sifa mbili. Sifa ya kwanza ni lazima liwe limekuja na Teknolojia au Tamaduni na maendeleo fulani,

Sasa uwanja wa mpira una sehemu zina magoli na kuna sehemu hazina magoli. Toka kwa Golikipa mmoja kwenda kwa mwingine. Kwa ivo lile eneo ambalo halina magoli, ni eneo kamili/zima, na lile lenye magoli ni eneo nusu kwa kuwa ile michoro ya pale golini, inaweka vizingiti vya matumizi kikawaida tofauti na kule kusiko na goli.

"Half space" ikiitwa eneo fupi la uwanja kuna taabu gani??
 
1)Ukitoka kwa golikipa pita katikati ya uwanja kuelekea kwa golikipa mwingine kule

2)Ukitoka kwa beki mbili nenda kwa namba saba maliza uwanja.

Half space ni katikati ya maeneo mawili niliyoeleza hapo juu. Hata ukitumia upande wa beki 3 na namba 11 pia ni half space kuna eneo ni half space.
 

Attachments

  • 16671293887984103450875970007179.jpg
    290.9 KB · Views: 4
Maelezo haya yanatofauti gani na yale ya kwangu??
 
Wewe umesoma HKL ndiyo maana unaona ni rahisi sana kupata maneno mbadala ya Kiswahili. Kama mdau alivyosema, mfumo wetu wa elimu unachangia na pia BAKITA hawana utaratibu madhubuti wa kuingiza maneno ya kiswahili kwa wakati katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande mwingine, nakubaliana na wewe kuwa inawezekana kabisa mtu kuepuka kutumia mchanganyiko wa lugha katika mazungumzo yake.

Bado nasisitiza, hatuna utaratibu bunifu wa kupenyeza maneno mapya ya kiswahili katika lugha yetu.
 
Tunache wivu jaribu na wewe kiswanglishi, ni bure tu hailipiwi, everyone has a choice, hupendi hama channel. Sio lazima katika maisha ya kawaida kulazimisha watu, Kwa hio mnataka English atumie nani? Tuache ushamba watz maisha ya uzwazwa yalishapita now tuko global. Some people, myself inclusive aren't that much good either but we get caught up sub consciously or rather involuntarily.
 
Kwa hio mnataka English atumie nani?
Inaonesha hujaielewa mada.

Kama anataka kutumia kiingereza kwenye kiswahili atumie kwa kufuata kanuni za Lugha.

Kama anataka kutumia kiingereza pekee basi akitumie kwenye Televisheni ama Redio zinazotumia Kiingereza.

Iwe kwa kiswahili ama kiingereza ni lazima kanuni za lugha zifuatwe.
 
Utasikia Mzamiru ni "Box to box midfielder". Wizi mtupu![emoji34][emoji34][emoji34][emoji21][emoji21]
 
Wakati mwingine akili yako inafanya kazi.
 
TO ME" naona mgunda anafaa, To me naona kaze abaki, to me Simba atavuka makundi,

Yaani upuuzi mtupu aisee
 
Punguza wivu wa kike kike we mleta uzi darasa la saba B
Mama yako, dada yako, mke wako ni wanawake.

Hiyo nayo ni dalili kuwa huyajui mambo mengi. Lugha ya kiingereza ni kama Kimakonde tu, unaweza usifike hata darasa la pili na ukawa unakijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…