Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

1)Ukitoka kwa golikipa pita katikati ya uwanja kuelekea kwa golikipa mwingine kule

2)Ukitoka kwa beki mbili nenda kwa namba saba maliza uwanja.

Half space ni katikati ya maeneo mawili niliyoeleza hapo juu. Hata ukitumia upande wa beki 3 na namba 11 pia ni half space kuna eneo ni half space.
Nimeuelewa mchoro wako. Eneo nusu la uwanja (Half space) halipimwi kwa mapana bali kwa marefu. Hulitizami toka kushoto ama kulia bali toka chini kwenda juu ya mchoro wako.

Limeitwa eneo nusu la uwanja kwa kuwa kulia na kushoto mwa uwanja kuelekea kwa Golikipa wa timu nyingine hakuna ile mistari ya Golini. ndipo ama mchezaji mshabuliaji ama beki hukaa.
 
Siku hizi kuna double pivot....huwa nacheka mno nikisikia hii
Daaah mwanangu unachekaga kama mimi ninavyochekaga nikilisikiaga hili neno yaani wachambuzi uchwara bwana daaah inachekesha sasa wenyewe wakishalitamka hili ndo wanajiona boooonge la wachambuzi eti
 
Wengi wao hawana taaluma bobevu ama hawana weledi wa kutosha wa mchezo wa soka.

Wengi wao ni makasuku wazuri tu na wanatafsiri chambuzi za wataalam wanaotumia lugha za kigeni..hivyo utaona wanajua Sana kumbe ni U-lufufu mtupu..
 
Code mix hizo na chanzo chake kikubwa ni kuto kuwa na lugha moja ya mawasiliano na kujifunzia hasa wakati wanasoma mashuleni kwahyo inapelekea mtu kuwa affected wakati wakutumia lugha kwahyo usiwalamu bari toa lawama kweny mfumo wako wa elimu na lugha ndio kweny Tatizo
Miongoni mwa sababu za code mixing ni kutafuta ufahari au ujiko kwamba na mimi nimo. Kiswahili kinajitosheleza mno,hawa wanapenda tu sifa kwa ile kuiga kutoka kwa wakoloni wetu.
 
Huwa nakereka sana hawa jamaa wanaochambua soka la bongo wanavyopambana kufa na kupona kuongea kiingereza. Hivi hawawezi kuchambua mpira bila kuingiza hivyo viingereza vyao vya ugoko?

Badala ya kusema "Value" kwa nini wasiseme thamani?

Badala ya kusema "Flanks" kwa nini wasiseme eneo la kulia au kushoto?

Badala ya kusema "assists" kwa nini wasiseme amesaidia wengine kufunga?

Na vingereza vingine vingiiiiiiiii!!
Hiyo ni sawa na kutia vitunguu, nyanya na chumvi kwenye mboga,inaleta ladha flani hivi,cha muhimu ni kuwa tuanawaelewa...
 
Jifunzeni lugha ya kingereza sio mnaishi kwa kulalamika hata kwa Mambo Madogo
 
Kiswahili hakitoshi kuelezea mambo mengi na ujumbe uliokusudiwa ukafika bila walakini.., tujifunze kiingereza wakuu
 
Back
Top Bottom