Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Jifunzeni lugha ya kingereza sio mnaishi kwa kulalamika hata kwa Mambo Madogo
kama hatujui Kiingereza tungetoa tafsiri yake!!?

Au wewe unadhani Kiingereza ni Lugha ya mungu kwa ivo ili uijue ni lazima uwe malaika au mtakatifu??
 
Kiswahili hakitoshi kuelezea mambo mengi na ujumbe uliokusudiwa ukafika bila walakini.., tujifunze kiingereza wakuu
Siyo kweli. Ni kasumba tu kuonesha kwamba Kiingereza ndiyo utaalamu, kiingereza ni Lugha tu sawa na Kisambaa.
 
kama hatujui Kiingereza tungetoa tafsiri yake!!?

Au wewe unadhani Kiingereza ni Lugha ya mungu kwa ivo ili uijue ni lazima uwe malaika au mtakatifu??
Aaaah , Mkuu wachambuzi wetu wakiongea hivyo ndo wanajiona wameongea sahihi 😁
 
Aaaah , Mkuu wachambuzi wetu wakiongea hivyo ndo wanajiona wameongea sahihi 😁
Wawe na sababu za msingi kuchanganya Lugha. Wenzao kina Charles Hilary, Ahmed Kipozi au Sued Mwinyi walikuwa watangazaji mahiri na maarufu bila ya kuchanganya Lugha kishamba kishamba.

Mechi ya Simba na Mtibwa Sugar, watangazaji wa Azam walijitahidi sana kutangaza na kuchambua vizuri bila ya hivyo viingereza vyao vya ugoko.
 
Siyo kweli. Ni kasumba tu kuonesha kwamba Kiingereza ndiyo utaalamu, kiingereza ni Lugha tu sawa na Kisambaa.
Mkuu kiswahili hakitoshi na ni kirefu, mfano haya maneno Good,better and Best ni rahisi zaid kuyatumia kufanya ulinganifu kuliko kiswahili

Kuna mtu alikua anafanya kazi ya kutafsiri maneno ya kiingereza kwenda kiswahili na sentesi yenyewe ilikua ni hii

Use the Constant Multiplication Rule for Integrals

Unaweza kusaidia kutafsiri hio sentesi kwa kiswahili na ukaeleweka..?
 
Back
Top Bottom