Wachambuzi wa mpira bongo ni lazima kuongea kiingereza ugoko?

Nimeuelewa mchoro wako. Eneo nusu la uwanja (Half space) halipimwi kwa mapana bali kwa marefu. Hulitizami toka kushoto ama kulia bali toka chini kwenda juu ya mchoro wako.

Limeitwa eneo nusu la uwanja kwa kuwa kulia na kushoto mwa uwanja kuelekea kwa Golikipa wa timu nyingine hakuna ile mistari ya Golini. ndipo ama mchezaji mshabuliaji ama beki hukaa.
 
Siku hizi kuna double pivot....huwa nacheka mno nikisikia hii
Daaah mwanangu unachekaga kama mimi ninavyochekaga nikilisikiaga hili neno yaani wachambuzi uchwara bwana daaah inachekesha sasa wenyewe wakishalitamka hili ndo wanajiona boooonge la wachambuzi eti
 
Wengi wao hawana taaluma bobevu ama hawana weledi wa kutosha wa mchezo wa soka.

Wengi wao ni makasuku wazuri tu na wanatafsiri chambuzi za wataalam wanaotumia lugha za kigeni..hivyo utaona wanajua Sana kumbe ni U-lufufu mtupu..
 
Miongoni mwa sababu za code mixing ni kutafuta ufahari au ujiko kwamba na mimi nimo. Kiswahili kinajitosheleza mno,hawa wanapenda tu sifa kwa ile kuiga kutoka kwa wakoloni wetu.
 
Hiyo ni sawa na kutia vitunguu, nyanya na chumvi kwenye mboga,inaleta ladha flani hivi,cha muhimu ni kuwa tuanawaelewa...
 
Jifunzeni lugha ya kingereza sio mnaishi kwa kulalamika hata kwa Mambo Madogo
 
Kiswahili hakitoshi kuelezea mambo mengi na ujumbe uliokusudiwa ukafika bila walakini.., tujifunze kiingereza wakuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…