Wachezaji kumi bora wa Afrika mpaka sasa

Wachezaji kumi bora wa Afrika mpaka sasa

yaya toure na drogba wanaanzaje kukaa juu ya mane na salah? kwa misingi ipi hasa?
Umeanza kuangalia mpira lini? Toure amebeba tuzo ya mchezaji bora Africa mara nne mfululizo, inamaana alipendelewa? Drogba kabeba mara mbili na ushindi wa makombe kibao ambayo mchango wake ulikuwa direct.

vipi umwahi kuwasikia akina ahmed Hassan? Hossam Hassan? Mboma?
kanu mbele ya okocha?
Hawa wote nimewataja kwenye list ya wote waliochambuliwa, hujaisoma hapo kwenye post?

Kanu yupo juu sana kimafanikio kufananisha na Okocha. Kanu kabeba Uefa champions league, ligi kuu england, tuzo ya mchezaji bora Africa mara mbili etc wakati Okocha hana hata kimoja kati ya hivyo.
 
Kanu yupo juu sana kimafanikio kufananisha na Okocha. Kanu kabeba Uefa champions league, ligi kuu england, tuzo ya mchezaji bora Africa mara mbili etc wakati Okocha hana hata kimoja kati ya hivyo.

Okocha alikua ndie star player wa Nigeria kwa muda wote ambao Kanu alikua ni mchezaji. Hiyo champion league aliobeba AKIWA kama mchezaji wa akiba ndio kigezo cha yeye kuwa bora kuliko Okocha?
 
Umeanza kuangalia mpira lini? Toure amebeba tuzo ya mchezaji bora Africa mara nne mfululizo, inamaana alipendelewa? Drogba kabeba mara mbili na ushindi wa makombe kibao ambayo mchango wake ulikuwa direct.

Yaya toure na Drogba hakuna aliwahi kubeba taji la Africa Cup huku kwa kila mafANIKIO WALIOYAPATA ULAYA MANE Ameyapata.
hiyo tunzo sio kigezo cha wao kuwa bora, mwaga statistics zao hapa ndio tukuelewe.
 
Okocha alikua ndie star player wa Nigeria kwa muda wote ambao Kanu alikua ni mchezaji. Hiyo champion league aliobeba AKIWA kama mchezaji wa akiba ndio kigezo cha yeye kuwa bora kuliko Okocha?
Kanu kabeba tuzo ya mataifa ya Africa wakati wanacheza pamoja timu ya taifa, tena mara mbili. Kanu amefanya vizuri sana ajax, mechi 56 na magoli 25 ndipo akanunuliwa na inter milan na kabeba ucl akiwa pale ajax.
 
Ni dharau kukosekana jay jay Okocha, nadhani anadharaulika kwa vile hakubonda timu nzuri nzuri(mafanikio makubwa) ngazi ya klabu.

Okocha ambae Ronaldinho anamkubali mnoo na aliwahi kunukuliwa dinho kuwa Okocha hakupaswa kwenda Uingereza, kilichomponza ni ile hamu yake ya kucheza premier league.

Okocha ambae alitoka kwao Nigeria kwenda Ujerumani kumtembelea rafiki yake, akaenda mazoezini kupasha kisha mwalimu akaomba asajiliwe mara moja.

Okocha ambae pale Uturuki alipewa jina la Mehmet na kuzawadiwa uraia juu kwa soka safi kabisa alilolimwaga pale FENERBAHCE.

Ndio kiungo mnyumbulifu zaidi kwa Afrika hadi kufikia leo hii

Okocha ndio Zinedine Zidane wa Afrika.

Nigeria ilikuwa anaibeba mabegani mwake.

Inasemekana okocha alikua mwalimu wa gaucho. Sema tu gaucho alikua na timu nzuri lakini si chochote si lolote kwa okocha. For me, okocha ni zaidi ya gaucho.

Kati ya huu utatu
1 zinedine zizo
2 okocha
3 gaucho

Hapo nitaenda na 1 and 2.
 
Baada ya kutomuona Mbayuwayu basi uzi wako wote ni feki. Okocha ni mmoja tu duniani na mpinzani wake ni Gaucho pekee.

Acheni kupima uchezaji bora kwa kuangalia vikombe au tuzo alizopata mchezaji.

Mpira ni zaidi ya kufunga magoli.

Aliyokuwa anaweza kuyafanya Jay Jay kwenye orodha yako hapo juu hakuna anayeelekea japo robo yake.

Hivi unamjua Diego Maradona wewe? Hivi ulimuangalia Leo Messi kwa umakini?

Hivi kuna players wanaoufanya mpira uonekane rahisi kama ambavyo Maradona na Messi tuwaonavyo!! Maradona na Messi ndio wamenifanya niupende zaidi mpira. Na ita-take time kumpata mbadala wa hao mafundi.

Ingia youtube mcheki diego akisakata kabumbu
 
Inasemekana okocha alikua mwalimu wa gaucho. Sema tu gaucho alikua na timu nzuri lakini si chochote si lolote kwa okocha. For me, okocha ni zaidi ya gaucho.

Kati ya huu utatu
1 zinedine zizo
2 okocha
3 gaucho

Hapo nitaenda na 1 and 2.
Unadhani ni kwanini Okocha hakusajiliwa na timu kubwa?
 
Okocha top 3 kwa lipi hasa? Wekeni rekodi zake ili tufahamu. Ila labda anaweza kuingia kwenye 20 bora kwa kuangalia vigezo vilivyotumika.
Vigezo vyako vinaonekana sio uwezo wa mchezaji bali ni mafanikio ya mchezaji wa kiafrika aliyechezea timu kubwa za ulaya.Hao wakina mane,Essien wako kwasababu yakucheza hizo timu kubwa za ulaya ila hawana uwezo wakuwashinda hao ambao hawako kwenye list.yaan mane anamshinda Aboutrika,Okocha,diof,rigobet song,amunike ubora?.hiyo list yako ni feki kwa kiwango kikubwa.
 
Okocha top 3 kwa lipi hasa? Wekeni rekodi zake ili tufahamu. Ila labda anaweza kuingia kwenye 20 bora kwa kuangalia vigezo vilivyotumika.
Achana na mambo ya rekodi kama okocha hayupo kwenye hiyo list jua ni feki.labda kama list yako haizungumzii ubora wa mchezaji.
 
Aboutrika atamtoa nani kwenye list?
Uliwai kumuona Aboutrika akicheza?.Kama george weah,Mane,EssienDrogba wapo kwenye hiyo list wananini chakumzidi Aboutrika.labda uniambie kwasababu akucheza timu kubwa za ulaya ila sio uwezo.
 
Unadhani ni kwanini Okocha hakusajiliwa na timu kubwa?
Usajili wa mchezaji una mambo mengi.Nikama ambavyo pamoja na uwezo wa messi bado hawezi kuja kusajiliwa simba au yanga na kinyume chake.Kwa mfano rahisi Maguire wa Man United anakiwango gani chakumzidi Dickson job wa yanga?.Fred wa Man U anakiwango gani chakumzidi Chama wa simba?.Sasa chukua hiyo mifano michache alafu isambaze kwenye timu zote kubwa unazozijua uko ulaya alafu jiulize lile swali lako ukilinganisha na wachezaji wetu wa kiafrika wanaocheza afrika na viwango vyao dhidi ya hao wanaocheza timu kubwa ulaya.
 
Acheni kumfananisha gaucho na okocha. Gaucho ana world cup, ballon d'or, Uefa champions league, la liga, seria a etc.. tutajieni mafanikio ya Okocha ili alinganishwe na wengine.
Inaonekana bado hujui ubora ni nini.Kama ni vikombe na tuzo za dunia ata oliver giruu wa ufaransa anavyo uku mane au salah hawatakaa wavipate pamoja nakwamba kwenye list yako wapo.Mambo ya kupata vikombe na tuzo bado sio kigezo cha uwezo wa mchezaji.hayo yanaitwa MAFANIKIO ya mchezaji.mafanikio na uwezo ni vitu tofauti kabisa.kwasababu unaweza kua na uwezo usipate mafanikio na unaweza kua na mafanikio bila kua na uwezo.
 
Uliwai kumuona Aboutrika akicheza?.Kama george weah,Mane,EssienDrogba wapo kwenye hiyo list wananini chakumzidi Aboutrika.labda uniambie kwasababu akucheza timu kubwa za ulaya ila sio uwezo.

Aboutrika alikua na mustafa hadji walikua mashine ya kazi, sema tu kwakua ni waarabu hawazungumziwi sana huku.
 
Hivi mafanikio mnayapimaje ?
Mnalinganisha mtu na mtu au mtu kuhama hatua Moja kwenda nyingine juu ya pale alipokua mwanzo.
 
Back
Top Bottom