Anigrain
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 1,680
- 4,204
"Tofautisha uwezo na mafanikio wewe hapa unaongelea mafanikio sisi tunaongelea uwezo .."Mwanzo ulisema okocha hawezi kuwa moja ya wachezaji bora Africa sawa.
Ukasema hata tuzo alizoshiriki alikosa sababu hana mafanikio wala makombe ukatolea mfano kombe lolote africa sawa.
Kama ndiyo hivyo mbona basi kina giroud hawapewi tuzo kwa medali walizobeba?
Unaweza kuchukua makombe mengi lakini unaishia benchi kwahiyo utapata medal..
Tofautisha uwezo na mafanikio wewe hapa unaongelea mafanikio sisi tunaongelea uwezo ..
Okocha alikuwa na uwezo wa kucheza soka mkubwa sana..
Sasa mkuu kutokana na hiyo statement yako juu, huoni kama unataka tu ligi isiyokuwa na kichwa wala miguu
kama ushajua mleta mada anaongelea mafanikio na akatoa na vigezo vya kupima hayo mafanikio na Okocha hana hivo vigezo sasa huku kuzozana kunatoka wapi?
Au tuweke vigezo vya mleta Uzi pembeni, Naomba unipe namba ambayo angekaa Jay Jay Okocha kwenye top 10 ya wachezaji Bora wa Africa kisha utoe na vigezo utakavyotumia kumweka katika hiyo Namba.....!