Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Benchika kocha wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anafundishi timu JS Kabylie ya Algeria amemjumuisha kikosini kiungo Sadio Kanoute ambaye Simba imeachana naye, iwe kwa kumaliza kandarasi au vip, sasa hivi Benchika amekimbilia kwa Babacar Sarr ambaye Simba imetemana naye kwa kutoridhishwa na uwezo wake.
Babacar ambaye amekuwa na majeruhi ya mara kwa mara ndani ya kikosi, mchezo ambazo uko sana katika timu yetu kwa mchezaji anakuja vizuri anacheza mechi tatu tayari amekuwa mtu wa kufunga bandeji kila siku, akicheza amecheza kipindi kimoja tu.
Nilimshuhudia Kibu Denis kwenye mchezo wa Namungo kule Ruangwa ambako nilikwenda uwanjani kuangalia Kibu alikuwa akicheza huku akiwa na bandeji mguuni, hatimaye hakumaliza mchezo wenyewe akaingia Somba Somba Onana.
Kanoute naye alikuwa majeraha kila siku.Huko nyuma akina Tadeo Lwanga nao majeraha ya kila siku yalikuwa yanamuandama, leo yuko APR anakiwasha mwanzo mwisho.
Kwanini huu mchezo wa majeraha uwe sana katika timu yetu? Hili jambo lazima liangaliwe, nani anafanya mchezo huu?
Lakini hoja yangu kubwa hawa wachezaji wanaoletwa Simba msimu uliopita lakini wametemwa na sasa wanakimbiliwa na timu kubwa hapa Afrika, nini kimewatokea pale unyamani?
Viongozi wangu wa Simba, jambo hili liangaliwe, hawa akina Funga Funga, Mavambo, Okajepha wanaweza kufanyiwa mchezo mchafu wakaishia kuwa majeruhi na viwango kuporomoka kama alivyofanyiwa Onana.
Kitengo cha uchawi Utopolo kiangaliwe vingine tutakwisha.