Wachezaji wengi Ligi Kuu hawana Adabu, wana kiburi sana!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Inawezekana wanaamini kuwa mpira ni kusukuma tu gozi uwanjani ama makocha wao hawawafundishi kuwa mpira ni sayansi na ni sanaa pia. Labda pia wanadekezwa na udhaifu wa Marefa wetu katika kusimamia sheria za Mpira uwanjani. Zaidi inawezekana wanatiwa ujinga kwa utetezi wa matendo yao ya kihuni unaofanywa na mashabiki wao.

Lakini ukiangalia tabia za wachezaji wa Ligi Kuu ya Tanganyika, wawe wazawa ama wageni, nidhamu yao uwanjani iko chini ya 40% inayotakiwa kuwepo miongoni mwao.

Wameshakuwa Kaniki, hata ulifue vipi, halibadili rangi.
 
Hua nashagaa sana unakuta refa kapuliza filimbi wanakuja wote kumzonga hasa ikitokea penalty yaani hadi aibu
Hiyo ni mbinu inafundishwa kabisa na makocha.... Unamvuruga muamuzi huenda akabadili maamuzi lakini unampa pia golikipa muda wa kujiandaa kisaikolojia. Ulaya kama sio kumzonga muamuzi wasingekuwa wanajisumbua kwenda kwenye VAR
 
Kumzonga muamuzi ni jambo moja na kumzonga muamuzi bila ya adabu ni jambo jingine kabisa. Hivi huwa hatuoni wachezaji wetu wanavyopwaya kwenye mechi za kimataifa? Nimeshuhudia magoli kadhaa mechi za kimataifa tukifungwa kwa kuwa wachezaji wetu wanashindwa kufanya utovu wa nidhamu kwenye mechi hizo.

Mechi za leo ziangalie uone jinsi uchezeshaji wa Marefa utakavyowaathiri wachezaji wetu. Labda pia ni kutokana na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani ndiyo maana marefa wetu huwa hawapati sana fursa ya kuchezesha mechi za Kimataifa hata kama wana Beji za FIFA.
 
Hapo utakuwa umeshapigwa walau mechi 4 za ligi. Utafukuzwa kabla hujaanza kuongelea huo mpira
Sidhani mkuu. Hayo maarifa yataanza kuonekana faida zake kabla hata hatujaamza kuongelea mpira.
 
Kumzonga muamuzi ni jambo moja na kumzonga muamuzi bila ya adabu ni jambo jingine kabisa. Hivi huwa hatuoni wachezaji wetu wanavyopwaya kwenye mechi za kimataifa? Nimeshuhudia magoli kadhaa mechi za kimataifa tukifungwa kwa kuwa wachezaji wetu wanashindwa kufanya utovu wa nidhamu kwenye mechi hizo.

Mechi za leo ziangalie uone jinsi uchezeshaji wa Marefa utakavyowaathiri wachezaji wetu. Labda pia ni kutokana na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani ndiyo maana marefa wetu huwa hawapati sana fursa ya kuchezesha mechi za Kimataifa hata kama wana Beji za FIFA.
Unapimaje ili kujua kuwa muamuzi kazongwa bila adabu au la?
Waamuzi wetu wanakosa sifa za kuchezesha kimataifa kwa makosa yao wenyewe wala siyo kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji. Tumeshuhudia wakifanya maamuzi ya kijinga na yasiyoeleweka hadi kuhisiwa wanapokea rushwa.
N. B. Kwa mechi za leo ninakubaliana na wewe kuwa kwa upande wa Yanga tutaona utovu wa nidhamu utakaoigharimu timu. Simba kimataifa wanajitahidi sana kuepuka makosa ya utovu wa nidhamu.
Kwa ninavyowajua wasudani leo lazima mmoja kati ya Aucho, Djuma, Job, Bangala au Morrison akaangalizie mpira dressing room.
 
Sidhani mkuu. Hayo maarifa yataanza kuonekana faida zake kabla hata hatujaamza kuongelea mpira.
Kwa sasa wadau wa mpira wako na kiu ya matokeo mazuri kuliko nidhamu ya wachezaji. Na pia sio kila tabia aggressive ni utovu wa nidhamu. Wakati mwingine unamtisha mpinzani wako ili aingiwe na hofu. Siku zote hofu hisababisha kukosa umakini hivyo kufanya makosa yenye faida kwa mpinzani.
 
Wadau tufuatilie mechi hizi tatu za kimataifa tutajua tu team ipi marefa wanawabeba watovu wa nidhamu .
 
Waamuzi wetu wanakosa sifa za kuchezesha kimataifa kwa makosa yao wenyewe wala siyo kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji.
Hayo makosa yao wenyewe ni pamoja na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani.
 
Kwa sasa wadau wa mpira wako na kiu ya matokeo mazuri kuliko nidhamu ya wachezaji. Na pia sio kila tabia aggressive ni utovu wa nidhamu. Wakati mwingine unamtisha mpinzani wako ili aingiwe na hofu. Siku zote hofu hisababisha kukosa umakini hivyo kufanya makosa yenye faida kwa mpinzani.
Nidhamu ni uwanda mpana sana na haina uhusiano wowote na kuwa au kutokuwa "aggressive". Wachezaji wetu wanatakiwa kufunzwa jinsi ya kufikiri na hili linakuja kwa kujengewa uwezo wa kiakili wa kunyambua mambo na kufanya maamuzi sahihi kwa haraka. Elimu ya darasani na hata michezo kama chess ina msaada mkubwa katika kumjenga mtu katika eneo hili.

Nitaongeza pia ufahamu wa lugha kama kiingereza. Tunawaleta makocha na wachezaji wa kigeni lakini hatujawahi kujiuliza ni kwa jinsi gani lugha ni kikwazo katika mawasiliano kati ya wachezaji wetu na wao.
 
Kutokana na uwanda mpana wa nidhamu ndio maana nikaomba mifano walau 3 ya utovu wa nidhamu ili tujue tunaongelea katika angle ipi.
 
Back
Top Bottom