Wachezaji wengi Ligi Kuu hawana Adabu, wana kiburi sana!!

Wachezaji wengi Ligi Kuu hawana Adabu, wana kiburi sana!!

Kutokana na uwanda mpana wa nidhamu ndio maana nikaomba mifano walau 3 ya utovu wa nidhamu ili tujue tunaongelea katika angle ipi.
Unajua kwa uzowefu wa majadiliano ya JF hasa kwa vijana, unapoanza kutaja majina mada inahamishwa maudhui yake na kwenda kwenye ushabiki wa kitimu. Ukimtaja mchezaji wa Azam, watu wa Simba watasema mbona hujamtaja mchezaji fulani wa Yanga, na watu wa Yanga nao watataja mchezaji wa Simba.

Mnatoka kwenye kujadiliana mnaingia kwenye kubishana. Hoja hii si kwa ajili ya kubishana.
 
Sijasema kuwa utaje majina mkuu bali nimetaka scenarios ambazo zilihusisha utovu wa nidhamu. Kwa mfano unaweza ukasema kitendo cha mchezaji kumpiga mwenzake kwenye nchezo baina ya..... na.....
 
Hiyo ni mbinu inafundishwa kabisa na makocha.... Unamvuruga muamuzi huenda akabadili maamuzi lakini unampa pia golikipa muda wa kujiandaa kisaikolojia. Ulaya kama sio kumzonga muamuzi wasingekuwa wanajisumbua kwenda kwenye VAR
Uliona lini mwamuzi kaamua penalty akabidili maamuzi kwa ajiri ya kuzongwa ?
 
Kutokana na uwanda mpana wa nidhamu ndio maana nikaomba mifano walau 3 ya utovu wa nidhamu ili tujue tunaongelea katika angle ipi.
Unawezaje kutoa mifano bila ya kutaja waliotenda huo utovu wa nidhamu? Hata hivyo mimi nimeshashuhudia kwa msisitizo wachezaji wengi wakimsukuma Refarii kwa zaidi ya dakika moja ama kumzuia asiusogelee mpira ama kuupiga mpira mbali kabisa baada ya refa kupuliza filimbi kuashiria kuna kosa limefanyika.

Ukiangalia kule mpira unapochezwa kama ajira, wachezaji humzonga refa lakini siyo kama wachezaji wetu wanavyofanya.
 
Unapimaje ili kujua kuwa muamuzi kazongwa bila adabu au la?
Waamuzi wetu wanakosa sifa za kuchezesha kimataifa kwa makosa yao wenyewe wala siyo kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji. Tumeshuhudia wakifanya maamuzi ya kijinga na yasiyoeleweka hadi kuhisiwa wanapokea rushwa.
N. B. Kwa mechi za leo ninakubaliana na wewe kuwa kwa upande wa Yanga tutaona utovu wa nidhamu utakaoigharimu timu. Simba kimataifa wanajitahidi sana kuepuka makosa ya utovu wa nidhamu.
Kwa ninavyowajua wasudani leo lazima mmoja kati ya Aucho, Djuma, Job, Bangala au Morrison akaangalizie mpira dressing room.
Ona hii kenge
 
Bernard Morrison, Sospeter Bajana, Jonas Mkude, Kanoute, na wengineo wengi! Wajitathmini kwa kweli.
 
Leo wanacheza kwa adabu sana. Yale mambo yao ya mizozo na Refa hakuna. Fikria Yanga wamekataliwa magoli matatu na wako kimya. Jee ingekuwa kwenye Ligi Kuu ndiyo wamekataliwa hayo magoli...
 
Inawezekana wanaamini kuwa mpira ni kusukuma tu gozi uwanjani ama makocha wao hawawafundishi kuwa mpira ni sayansi na ni sanaa pia. Labda pia wanadekezwa na udhaifu wa Marefa wetu katika kusimamia sheria za Mpira uwanjani. Zaidi inawezekana wanatiwa ujinga kwa utetezi wa matendo yao ya kihuni unaofanywa na mashabiki wao.

Lakini ukiangalia tabia za wachezaji wa Ligi Kuu ya Tanganyika, wawe wazawa ama wageni, nidhamu yao uwanjani iko chini ya 40% inayotakiwa kuwepo miongoni mwao.

Wameshakuwa Kaniki, hata ulifue vipi, halibadili rangi.
Naunga mkono hoja nitarudi baadaye.
 
90% ya wachezaji wamekimbia shule pia mchezo wa mpira umetokea kwenye mazingira ya kihuni huwezi kukuta uwanja ambao hakuvutwi Bangi
 
Back
Top Bottom