Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Maudhui ya uzi si kutaja majina ya watu, bali matendo yao. Wewe huwa huoni wachezaji toka timu mbali mbali za Ligi Kuu wanavyobwatukiana kihuni na marefa wakati wa Mechi?Bila kuwataja majina wachezaji husika uzi wako unakuwa ni umbea tu kama umbea mwingine
Hapo utakuwa umeshapigwa walau mechi 4 za ligi. Utafukuzwa kabla hujaanza kuongelea huo mpiraTukisema wachezaji wapige vidato tunaonekana hatujui mpira. Mimi ukinipa timu nifundishe, mwezi wa kwanza wote tunaingia darasani na hatugusi wala kuongelea mpira. Tutaongea nidhamu, saikolojia, na vitu kama hivyo.
Hiyo ni mbinu inafundishwa kabisa na makocha.... Unamvuruga muamuzi huenda akabadili maamuzi lakini unampa pia golikipa muda wa kujiandaa kisaikolojia. Ulaya kama sio kumzonga muamuzi wasingekuwa wanajisumbua kwenda kwenye VARHua nashagaa sana unakuta refa kapuliza filimbi wanakuja wote kumzonga hasa ikitokea penalty yaani hadi aibu
Kumzonga muamuzi ni jambo moja na kumzonga muamuzi bila ya adabu ni jambo jingine kabisa. Hivi huwa hatuoni wachezaji wetu wanavyopwaya kwenye mechi za kimataifa? Nimeshuhudia magoli kadhaa mechi za kimataifa tukifungwa kwa kuwa wachezaji wetu wanashindwa kufanya utovu wa nidhamu kwenye mechi hizo.Hiyo ni mbinu inafundishwa kabisa na makocha.... Unamvuruga muamuzi huenda akabadili maamuzi lakini unampa pia golikipa muda wa kujiandaa kisaikolojia. Ulaya kama sio kumzonga muamuzi wasingekuwa wanajisumbua kwenda kwenye VAR
Sidhani mkuu. Hayo maarifa yataanza kuonekana faida zake kabla hata hatujaamza kuongelea mpira.Hapo utakuwa umeshapigwa walau mechi 4 za ligi. Utafukuzwa kabla hujaanza kuongelea huo mpira
Unapimaje ili kujua kuwa muamuzi kazongwa bila adabu au la?Kumzonga muamuzi ni jambo moja na kumzonga muamuzi bila ya adabu ni jambo jingine kabisa. Hivi huwa hatuoni wachezaji wetu wanavyopwaya kwenye mechi za kimataifa? Nimeshuhudia magoli kadhaa mechi za kimataifa tukifungwa kwa kuwa wachezaji wetu wanashindwa kufanya utovu wa nidhamu kwenye mechi hizo.
Mechi za leo ziangalie uone jinsi uchezeshaji wa Marefa utakavyowaathiri wachezaji wetu. Labda pia ni kutokana na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani ndiyo maana marefa wetu huwa hawapati sana fursa ya kuchezesha mechi za Kimataifa hata kama wana Beji za FIFA.
Kwa sasa wadau wa mpira wako na kiu ya matokeo mazuri kuliko nidhamu ya wachezaji. Na pia sio kila tabia aggressive ni utovu wa nidhamu. Wakati mwingine unamtisha mpinzani wako ili aingiwe na hofu. Siku zote hofu hisababisha kukosa umakini hivyo kufanya makosa yenye faida kwa mpinzani.Sidhani mkuu. Hayo maarifa yataanza kuonekana faida zake kabla hata hatujaamza kuongelea mpira.
Hayo makosa yao wenyewe ni pamoja na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani.Waamuzi wetu wanakosa sifa za kuchezesha kimataifa kwa makosa yao wenyewe wala siyo kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji.
Unaweza ukatuambia matukio walau matatu ambayo waamuzi hawakuweza kudhibiti nidhamu za wachezaji uwanjani?Hayo makosa yao wenyewe ni pamoja na kushindwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji uwanjani.
Aisee!!Unaweza ukatuambia matukio walau matatu ambayo waamuzi hawakuweza kudhibiti nidhamu za wachezaji uwanjani?
Nidhamu ni uwanda mpana sana na haina uhusiano wowote na kuwa au kutokuwa "aggressive". Wachezaji wetu wanatakiwa kufunzwa jinsi ya kufikiri na hili linakuja kwa kujengewa uwezo wa kiakili wa kunyambua mambo na kufanya maamuzi sahihi kwa haraka. Elimu ya darasani na hata michezo kama chess ina msaada mkubwa katika kumjenga mtu katika eneo hili.Kwa sasa wadau wa mpira wako na kiu ya matokeo mazuri kuliko nidhamu ya wachezaji. Na pia sio kila tabia aggressive ni utovu wa nidhamu. Wakati mwingine unamtisha mpinzani wako ili aingiwe na hofu. Siku zote hofu hisababisha kukosa umakini hivyo kufanya makosa yenye faida kwa mpinzani.
Kutokana na uwanda mpana wa nidhamu ndio maana nikaomba mifano walau 3 ya utovu wa nidhamu ili tujue tunaongelea katika angle ipi.Nidhamu ni uwanda mpana sana na haina uhusiano wowote na kuwa au kutokuwa "aggressive". Wachezaji wetu wanatakiwa kufunzwa jinsi ya kufikiri na hili linakuja kwa kujengewa uwezo wa kiakili wa kunyambua mambo na kufanya maamuzi sahihi kwa haraka. Elimu ya darasani na hata michezo kama chess ina msaada mkubwa katika kumjenga mtu katika eneo hili.
Nitaongeza pia ufahamu wa lugha kama kiingereza. Tunawaleta makocha na wachezaji wa kigeni lakini hatujawahi kujiuliza ni kwa jinsi gani lugha ni kikwazo katika mawasiliano kati ya wachezaji wetu na wao.