Wachina wanasubiri Rais Magufuli aondoke kwenye bandari

Hakuna nchi yenye demokrasia ya kweli kweli duniani! Mpaka sasa sisi Tanzania tunazidi nchi nyingi kidemokrasia.
 
Kwakuwa eneo lililotengwa kwa mradi wa bandari ya Bagamoyo ni 'ideal' kwa bandari kubwa ya kisasa, si Jambo la busara kuacha kabisa kuijenga bandari hiyo bali ni kutafuta njia mbadala ya kuanzisha na kuuendeleza ujenzi huo!
NB: Bandari ya Dar imechoka, na msongamano wa magari jijini unapunguza 'efficiency' yake!
 
ili Bandari ijengwe lazima Naibu Rais na wajanja wachache wapewe 10% kwanza bila hilo hakuna Bandari mpaka siku wakizeeka na kufa ndipo mchakato utaendelea tena
 
Tanzania ina rasilimali nyingi ipo vizuri usifananishe Tanzania na sehemu zingine Duniani, hakuna kinachofanya Tanzania ikashindwa kulipia chochote
 
Hata hiyo SGR lilikuwa suala la muda tu,huo mkopo wao hali ingekuwa kama Kenya vile.

Wanataka waendeshe wao hadi 2027!!
 
Haina 10% so wapiga dili wameitelekeza
 
Huu ni Ujinga, hata kama China wakimiliki hiyo Bandari Tatizo liko wapi? Duniani Kote bandari nyingi tu zinamilikiwa na Private Operators, Serikali kazi yake ni kukusanya Kodi Ushuru mbalimbali

Umekurupuka kasoma sera za china za kumiliki bandari halafu uje na hoja
 


Tatizo la TZ so bandari bali ni barabara na treni. Haya ni maneno ya kulishwa
 
Hata ukiyatoa maeneo hayo kwa wafanyabiashara tambua kwamba tunahitaji bandari nyingine moja au mbili zenye viwango vya kimataifa. (Bandari ya Tanga na Mtwara)

Sijui kama umeelewa hili bandari haitakuwa ya kwetu😂😂 hiyo ndiyo point yenyewe yaani ni kama china hata blendera yao wanaweka, bei yao. Wanaosema magodauni ni ya kuuza vitu kutoka kwao. Magu kaeleza bado watu wazito kuelewa
 
Mkuu naomba kuuliza! Huo mktaba ulishasainiwa? Pili kama ulishasainiwa kwa nini usivunjwe au tuanzishe majadiliano mapya na China ili kuurekrbisha?

Tatizo la Tanzania ni kusaini mikataba ambayo haina tija mfano ni kwenye madini. Mikataba mingi ya madini ni wizi mtupu na watanzania wenzetu walisaini kwa niaba yetu na haijavunjwa licha ya mapungufu yaliyopo.
 
lakini hazimilikiwi na wachina
 
Rais ajaye ni mimi, na mimi ni kauzu zaidi ya Magu,wachina hapa wamenoa,Tanzania kwanza,mengine baadae
 

Eboo! Wanasubiri mpaka Magufuli aondoke madarakani? awali ya wote Magu yupo mpaka 2035 na mpaka hapo atapatikana Edward Moringe Sokoine II na Mwl Nyerere III(for your information Magu ni NyerereII)!!! - Shirika la Ndege (ATCL) limeshafufuliwa with 11 planes, Reli - Usafiri wa garimoshi Dsm - Arusha umefufukiwa , na mengine mengi!!
 
Endelea kuota mchana, JPM kakuambia yeye huwa haoti mchana, ni USIKU TUUUUU.Endelea kusubiri
 

Ufalme uwekwe Tanzania. Nafikiri ushabiki wenu mnajisahaulisha kwamba Watanzania ni hatari kuliko mnavyofikiri. Nyerere alishidwa hii nchi, vijiji vya ujamaa vilishidwa, kuiga China ilishindikana jiulize ni kwanini. Sababu moja ni kwamba watanzania ni mkusanyiko wa wakabila mengi sana, dini zote , mila tofauti hutaweza kuwapelekesha kama punda iko siku watagoma. Tanzania sio China wala Rwanda
 


Hakuna sababu ya msingi ya kuwa na bandari mbili Dar wakuze badari ya Tanga
 
Kuna haja gani kujenga bandari mbili katika umbali mfupi?

Akili za Chadema bwana, mtaishia hivyo hivyo

We dada una mambo? Hapa Chadema inaingiaje?? Chadema inaishi kichwani mwako bila kulipa hata kodi!

Unasahau mradi huu ni wa Kikwete?? Unasahau hata Spika aliutetea na kamati ya Bunge kufanya ziara UChina??

Chuki yako dhidi ya Chadema inakubalika lakini una wajibu wa kujitendea haki kwa kuwa mkweli kwa nafsi yako!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…