Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 41,558
- 64,966
Pale D.I.T enzi hizo alikuwepo Prof. Kondoro na UDSM alikuwepo Prof. Luhanga.
Hawa walikuwa ni viongozi ambao walikuwa na maono na walitengeneza vichwa kweli kweli.
Tatizo ni kila mmoja anayekuja anakuja na sera na maono yake.
Prof. Mwamila alikuwa na "incubation programme" ya kuibua na kulea wagunduzi wanafunzi pale St. Joseph, Nelson Mandela na MIST, sijui zinaendeleaje maana sijaonana naye kitambo.
Kwa ujumla, duniani kote sekta ya elimu imeathiriwa na siasa; inayopelekea wajuzi kutokujikita kwenye taaluma zao na kukimbilia au kutegemea shukrani kwenye siasa. Hii pia imewaathiri ata wanafunzi, na kupelekea kukariri vitini ili afaulu, maisha mengine yaendelee.
Miaka ya nyuma tukiwa vyuoni, wengi walikuwa wakitamani kubaki vyuoni na kuwa wakufunzi, lakini kwa nyakati hizi, kila mmoja anapambana kuangalia ni wapi atapata pesa nyingi, iwe inamshushia heshima au haimshushii ili mradi tu apate pesa.