Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

itapendeza kama makanisa yakawa yanalipa kodi maana skuhzi zaka zinafosiwa
mfano mm nina kadi ya jengo kwenye kanisa letu na kila nikienda kanisani nachuma mchicha napeleka kama sadaka ukipigwa mnada wanaandika pale ila muinjilisti akaniita skumoja akaniambia utoaji wangu ni hafifu nkamuuliza mungunkanibariki mchicha kwahiyo nisimshukuru kwa bidhaa alio nibariki nayo akaniambia sawa mchicha mungu kakubariki nao ila unatakiwa utoe hela nyingi zaidi ya hyo ya mchicha nkamwambia nakuheshimu kwakua upo kwenye vazi la kanisa ila usije ukaniongelesha haya mambo ukiwa upo nje ya kanisa nkasepa .
hvi wanataka tutoe roho zetu ama maana wanaona tunachotoa kidogo sana wakat hawana kodi wala malipo wnaayofanya kutokana na wanachoingiza
 
Kasali mahala pengine
 
Hiki kirusi kimeingia makanisa karibu yote. Huo ndio utakuwa mwanzo wa kuanguka kwa ukristo
 
Zaidi asome neno kwa makini.... Mtafute sana Mungu ,wachungaji wamegeuza waumini ATM zao. Ukilijua neno, na ukamtafuta Mungu kwa bidii atakupa maelekezo ya sadaka zako na fedha zako kuliko kuwasikiliza Hawa watoto wa mama Hawa(Eva).
 
Sawa hata hivyo kitanzi Cha michango kimehamishiwa jumuiya ndogondogo.... La msingi ni NENO LA MUNGU na msaada wa ROHO MTAKATIFU ambae ni mshauri na mwalimu mwema atakayekufikisha kwenye KWELI.
 
Zaidi asome neno kwa makini.... Mtafute sana Mungu ,wachungaji wamegeuza waumini ATM zao. Ukilijua neno, na ukamtafuta Mungu kwa bidii atakupa maelekezo ya sadaka zako na fedha zako kuliko kuwasikiliza Hawa watoto wa mama Hawa(Eva).
Wameshatufanya chanzo cha mapato
 
A toxic person, ina maana hajali kuwa unauguliwa?

Mimi kama kuna watu hawawezi kunipata ni hao wachungaji toxic, Sadaka yangu na zaka na malimbuko najua ninapoyapeleka mwenyewe na hakika sijawahi pungukiwa.

Kuna watoto hawana chakula, hawana mavazi nichukue pesa nimpelekee mtu anayesomesha watoto wake St.constantine? Hapana sio mimi, kila mtu atumie pesa zake atakavyo.
 
Ni kwamba hawafuati mafundisho ya Muhammad kikamilifu , alikuwa huwezi muona mpaka utangulize chochote kitu
soma
Koran 58:12. Enyi mlio amini! Mnapo sema siri na Muhammad, basi tangulizeni sadaka kabla ya kusemezana kwenu.....
 
Don't bother, Soma maandiko" YESU alimwambia Yule mama msamalia,itafika wakati watu watamuabudu mungu katika ROHO na kweli" endele kwenda kanisani,na hiyo sadaka utaitoa kadri Mungu atakavyo kubariki.
 
1Wakorintho 9:13-14 "

Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu na wale waihudumio madhababu huwa na fungu lao katika madhahabu? na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwaba wale waihubiriyo injili wapate ridhiki kwa hiyo

//

Mal 3:10-12 SUV

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.

//

Mungu akubarikini nyote!
 
2Kor. 9:6-8:
6Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.
7Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu...
Brethrens, that's New Convenant; the Convenant of grace and truth whose founder is Lord Jesus Christ himself.
Wakristo tunachanganya isivyofaa Agano la Kale na hili Jipya. Tusome na kulijua vema Agano Jipya; tutampenda sana Mungu. We're no longer under The law (Torah).
 
Mchungaji wako ana njaa kinoma by the way mimi nasali tag huu ni mwaka wa 5 sitoi hicho mnachoita zaka maana haina faida na pia zaka sio sadaka ya agano jipya
 
Huo ni utumwa wa hadharani.
Nguruwe amekatazwa agano la kale lakini analiwa tu huku tukisema ni old testament commit.
Zaka iliagizwa kwenye agano la kale lakini mnalazimishwa mpaka sasa na hamshituki kuwa ni maagizo yaliyopitwa na wakati.
Wana beba yanayowapendezesha, yanayowanyima Raha wanasema Ni ya kale.

Mkuu nielekeze Ilo kanisa lilipo niwe naenda kusali daily na kubadilisha gari daily na sitoi hata shilingi moja Tena mie ndio nakuwa namueleza matatizo daily kuwa gari imezingua ball joint,Mara betri anikopeshe.
 
Nakuwa naposti daily Niko viwanja ili azidi kuumia inaonekana anaumia na watu kubadilisha usafiri huyu. Huwa napenda watu wenye karoho ka kuumia ili waumie zaidi kwa ujinga wao
 
Huku kwet katolik mpaka unaona aibu wnap tangaza kanisan una amua kutoa hakuna sms za zaka wala sadaka zaid za kuwai kwenye jumuiya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…