Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Anataka akishahudumiwa kiroho, baada ya hapo mtumishi aende kulima sijui!???
 
Baba wa rafiki yangu alikua mzito serikalini, baada ya mzee kustaafu alianza u karibu na mchungaji. Kwakua sasa haendi kazini, basi asubuhi mchungaji anampitia wanakwenda kuona wagonjwa, kuandaa mikutano kanisani, mara anapiga simu nyumbani atakula kwa mchungaji.

Walichogundua baadae ni kuwa 10% ya pension ya dingi mchungaji aliiramba. Wakati mzee hajamalizia nyumba na ana magonjwa kibao yanahitaji pesa kutibiwa.
 
Kuna mchungaji uku anakula kondoo wake adi zile kondoo zenye couple...yaani kondoo wapo busy na malisho uku wakitafunwa.

Wachungaji 🙌
 
Hili ni agizo la Mungu toka agano la kale kwamba 10% ya makusanyo yako yote ya kazi ya mikono yako iwe kwa siku, wiki, mwezi ama mwaka ni lazima yaende kwa Mungu wako

Ilikuwa ni LAZIMA kwa wakati huo sababu Makuhani na wazee wa dini walikuwa wanajikimu kupitia fungu hili la kumi - sadaka na matoleo mengine hayo yalikwenda kwenye shughuli za kutangaza neno la Mungu

Sasa hadi leo kwa mtumishi kupewa fungu hili ni HAKI yake ila sasa linazidi na kuwa kubwa mno hadi kufikia mtumishi anaishi maisha ya juu - inafikia hatua mtumiliki hadi Private Jet - Ndege binafsi, majuumba la kifahari huko waumini wake wakitembelea ndala zilizotoboka

Ki-imani hasa ya kikristo huwezi kufanya adjustment ya hii sheria ya fungu la kumi ila ni busara tu kwa watumishi kulitumia fungu hili vizuri vinginevyo wakristo wengi wataacha kutoa - hakuna haja ya kutoa fungu la kumi afu mtumishi anamnunulia mkewe Birthday gift ya gari la dola Mil 250

Hili halikuwa lengo la Mwenyezi Mungu kutuwekea hii sheria sisi wakristo
 
Hakuna Mchungaji anayekulazimisha kutoma sadaka/zaka, kama hujisikii kutoa acha, waache wanaowiwa kuchanga wamtolee Bwana.

Na kimsingi naomba ikumbukwe kwamba maswala haya ya sadaka/zaka/dhabihu yapo Kibiblia (soma Malaki 3:8-10, Matendo ya Mitume 10:1-4, Kumb. la Torati 14:22-24). Wachungaji ni mawakala tu wa Mungu, ingawa wachungaji wengine ni matapeli kama inavyofundishwa kwenye Mathayo 24:23-25 au Luka 17:22-24.

All in all, nawasihi muweke akiba ya maneno hasa kwenye mambo haya ya kiimani ili mjiepushe na tufani inayoweza kuwakumba ninyi wenyewe au vizazi vyenu; kwasababu Mungu hadhihakiwi hata kidogo.
 
Kwa Afrika dini ni inazidi kufanya watu washindwe kutumia akili zao vizuri. Mambo kibao tu ukianza kuyaweka kwenye mizani yapo astray. Dini ni upuuzi kama maupuuzi mengi tunayoyaona mitaani.
The peace that we enjoy around the world [emoji289] is a direct result of positive religious activities. Even most of the great and accomplished scientists, educators, innovators, researchers, doctors, engineers, technology experts have had affiliations to some religious bodies.
 
Usithubutu kumtupa jongoo na mti wake, walisema wahenga. Usiache mbachao kwa msala upitao. There are many, many, many, good churches & wonderful Christians kila mahali. Find one and be part of it. Hutokaa ujute maishani mwako. Utoaji wa sadaka unapima level ya upendo wako kwa Mungu, na kukusaidia kudhibiti tamaa, uchoyo, ubinafsi na ubahili. Hata kama wahitaji wasingekuwepo, bado sadaka kutoa ni must kwa muumini. Uchoyo na ubahili wa wengi ndio huwafanya kubuni sababu lukuki za kuhalalisha wasitoe sadaka kwa Mola wao.
 
Mkuu akili za mwafrika zipo programmed na mzungu ni mpaka pale tutapoweza kuflash hili tatizo, China washang'amua hili wapo bize kutengeneza kizazi ambacho hakishabiani mawazo na Mzungu.
All humans -- Mzungu, Mwafrika, Mhindi, Mwarabu, Mwamerika etc -- their problem is essentially the same. Hakuna nafuu ya mwingine. Wewe ushakuwa brainwashed mpaka unadhani Mzungu is the best. Au kwa vile anakuletea tumisaada!???
 

..the conflicts that we face around the world is a direct result of negative religious activities. Some of the great controversies that happened back in the days are due to religions that actually don't help us. The African brains have been programmed to accept and abide to everything a white man does, says or throws into our continent.

It's time to wake up and follow our own ways of life, easterners are doing that now, so we need to do the same.
 
Sasa mzee aliona vyake ale na mchungaji, kuna tabu hapo!??? Nilidhani mchungaji alimtapeli mstaafu, hapo ingekuwa noma chacha.
 
I agree 100%
 
Perfect!!! Wakati wa matetemeko na magonjwa ndipo haohao watumishi huonekana wa maaaaanaa.
 
I pity you for trying to cluelessly change inclinations from ^Westerners^ to ^Easterners.^ Religious faith kama ingefanikiwa kuwa suspended ama obliterated ulimwenguni just for a day, believe it or not, the next morning the whole world [emoji289] would literally wake up with only soulless bodies of dead people scattered all over.
 
Kaka upo sahihi. Ila marekebisho kidogo sio Mwamposa anayeuza maji Bei kubwa n Seguye
 
wakati huo nyumba ya lawi ndio ilikuwa makufani na walfanya kazi madhabahuni watu waliambiwa watoe sadaka kuwakimu walikuwa hawana mifugo wal mashamba ili wasishawishike na kutenda dhambi wao ndio walikuwa wanapokea sadaka na kaombi na kuyaingiza mahali pnapoitwa patakatifu pa patakatifu ..story ya fungu la kumi iliazia mahali nabii sijui ni nan ajenge hekalu watu wakatangaziwa na nabii ukitoa fungu lako la kumi kwa ajili ya hekalu utazidishiwa watu wakawa wazito baadae ikawa mashindano ya kutoa wabarikiwe na walibarikiwa sana lilipo kamilika akawakataza kutoa ..hekalu limekamilika..watu akasema kuliko tukose baraka we baki nazo..kwa hio hio sheria ya kutoa ni utashi ako wala mungu hayupo na wewe hekalu lishajengwa na limekamilika hawa wanaohimiza ni wezi na hutabarikiwa wala hawana garantii ya kubarikiwa
 

Sawa mkuu, tupeleke zaka, sadaka na kila kitu madhabahuni ili tubarikiwe. Tunaanza na mwenye 100,000. Wenye jero pigeni makofi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…