Karibu sana. Nakumbuka those days 2002 nilikuwa na kademu pale CBE kakaniomba nikanunulie Motorola ilikuwa maarufu sana kwa jina la T.I.D, nikakaambia sawa. Nakuletea zawadi utakayoweza kununua T.I.D mbili, demu mawazo yake yakamruka, enzi hizo cheni za gold ndio habari ya mjini, basi akajua atapata moja.
Nikamwambia jumamosi asubuhi nakuletea zawadi nikija kunywa supu CBE Club. Ile naingia tu namuona bibie yuleeee, amewaka mwenyewe.
Basi akanipokea kwa lundo la mabusu, hata supu anainywa hainyweki. Basi nilipo maliza kula nikamwambia zawadi yako iko kwenye gari.
Tukaenda kwenye gari Toyota Hilux 12R, model 1982. Ile tumefika tu kwenye gari anaona magunia matano ya mchele, nikamwambia hii ni zawadi yako.
Msichana akaipokea kwa shingo upande sana, basi nikatafuta vijana, wakaushusha ule mchele, wakaupeleka Serengeti chumbani kwa binti.
Nikampa na mzani na mifuko, nikawa namtafutia wateja maofisini binti anafanya delivery, alitengeneza sana hela.
Mwanzoni hakuyasoma mawazo yangu