4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 8,406
- 9,619
Ccm na tuvikundi vyenu ,mpo na matatizo sana, mwanaccm kuikosoa au kua na msimamo tofauti haijawai kuwa na afya kwa mwanachama husika, hii tabia haijaanza leo ndani ya ccm bali tangu kipindi cha Nyerere, sema kwa sasa mmezidi,Nimeona X-Mayor wa Ubungo Bwana Jacob akiripoti kwamba OLe MUSHI anaumwa na inasadikiwa amepewa sumu. Inaelezwa kuugua kwake ni siri na yupo Sehemu ya siri; wanadai wanasiasa wenzake wamemtenga na hakuna juhudi za kumfikisha hospital.
Nitoe rai kwa wanaohusika au familia watoke adharani kusema na jamii kuondoa uzushi huu unaolenga kubomoa taswira njema ya serikali ya kuwalinda wakosoaji wake. Serikali imejipambanua wazi kwamba haitishwi na wakosoaji hivyo ni vigumu wakosoaji wakapata madhara kiafya kisa wamesema vibaya chama au serikali.
Lakini pia nitoe wito kwa wanachama wa CCM kujiamini na kutosubiri maelekezo yakumsaidia binadamu anapopatwa na matatizo. Wenzenu CHadema wamewezaje kuwa wasemaji wema kwa wana CCM wanapougua au kupata majanga? Kwanini CHadema wawe wakwanza kutoa taarifa za msaada kwa mwana CCM?
Nape alipopata msaada marafiki wote wakamkimbia wakabaki wana harakati na CHadema kumsemea, same applies to mzee Kinana na hata akina polepole. Ninyi wahanga wanufaika wa siasa mnakosaje kujifunza kwa wenzenu?
Siasa zinapofika mahali zikakunyima uhuru wa kwenda msibani ,hospital au kwa mwanadamu mwenzako anayepitia kadhia flan basi hizo fikra za siasa zimekutenga na roho wa Mungu.
Kama ni kweli Ole MUSHI unaumwa tukutakie afya njema . Usisite kujitokeza kuomba msaada maana watu wema bado wapo na wanasubiri wito wako.
Leo huwezi kutuaminisha kwamba ni vigum wanachama wenu kuweza dhuliwa na wanaccm wenzake, inawezekana sana , kati ya chama chenye mambo ya kutendeana vibaya wanachama kwa wanachama, kufitiana, kubaguana Afrika basi ccm ni no moja,
Na kwa kweli nchi hii ukitaka ishi maisha ya amani moyoni bila kujali nafasi yako katika jamii, kaa mbali na ccm ,wasikuzoee na usiwazoee, kaa bila chama au chagua majukwaa huru, kupitia vyama vingine ila sio ccm.
Wanaccm ni nyama zinazotembea ila roho ya ubinadam, hofu ya Mungu kwao ni kama ardhi na mbingu hamna kitu pale,
Alafu unamkuta kijana , au mtu na akili yake eti ukitaka kutoboa lazima uwe ccm , pumbavu, fuatilia vizuri kuanzia wafanyabiashara wakubwa, wadogo , hao wajifanyao wanachama kindakindaki nini kipo nyuma yao , kama sio kulinda madili yao kupitia mgongo wa uanachama wa ccm (wizi ,ujangili n.k)
Be strong wewe, ccm sio Mungu, baba yako au mama yako , maisha na mafanikio yako yapo mikononi mwa Mungu wala sio ccm