Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Umenikumbusha fundi wangu mmoja alikuwa akinijengea kibanda mahali fulani, ilikuwa nikimlipa maybe 350k basi atakuja kazini tena baada ya siku tatu hadi nne hela zikimwishia.

Kuna siku nimemlipa 700k baada ya siku mbili anasema anaumwa hana hata mia ya kwenda Hospitali, kumbe jana yake alikesha Kitambaa Cheupe na wale slay queens.

Yaani totozi na gambe ndiyo moto wa kuchomea hela za wengi
Huwezi amini hata huyu dogo nnaemuongelea hapa ni fundi wa kitu fln hivi,
 
Nimependa haka ka mustari πŸ‘‡

"masikin ya Mungu weekend ilikua kesho yake nakuta yupo chimbo langu anakunywa hovyo na videm viwili, wanapiga piga picha tu, mimi nikapotezea sabab huwa sina mambo ya kuwapangia watu matumizi."
Hahahahaa

Dogo anaiga
 
Nidhamu ya pesa ni mtihani mzito shekh!

Imagine umehangaika zako mara umepiga β€œmshindo” wako alafu ukiangalia ndio weekend imeingia kila mahali ukipita unamsikia mariooo

β€œShiiiiiiii badiiiii”
β€œnilikuwa na wanangu kina chinooo”
β€œniseme nsisemee, semaaaa” X 2

Ukizidi kusogea unamsikia jux nae ,
β€œhuyuuu demu ake naniiii, anpandisha midadiii, anitafutia lawama,……….”

Ukisema uzame ndaniii tu kwisha habari yako, unakuta watoto wamepanda juu ya meza wanacheza na wamependeza balaaa!

Unaendaje kulala mkuu, au tukuulize,

we kuwezaaa???

Nyie achenii banaa starehe ni tamuuu πŸ˜‚πŸ˜‚

Tukiamka asubuhi ndio majuto huanza.
Yaani hapa nilipo huo wimbo wa marioo niseme nisiseme unabang..hahhahha vijana kazi mnayo
 
Maisha ni haya haya nikipata milioni Laki Tano nafanya mambo ya msingi Laki Tano totozi k vant mpepe nk
Mla Bata

Dogo anadhan tumeanza juzi kuchezea hela, mimi mwaka 2014 nilishawahi kutumia million 4 kwa starehe ya siku moja, hapo nimepanga uswahilini ndani sina kitu cha maana, uki-adjust for inflation hio ni kama 6m kwa sasa. Unaweza kusema nilinunua IST af nikaiwasha moto. Lkn toka hapo nikaapa sitokuja kuwa mpuuzi kiasi hicho

Sasa wewe endelea unadhan ni sifa kutumia pesa hivyo, utakutana na shida moja siku moja ikunyooshe na huna hata mia, akili zitarudi, lkn zitaondoka tena sababu umejiendekeza.

#WeEndeleaTu (Mwana FA)
 
Achaaa tu mkuu, kuna majuto huwa tunapitia [emoji23]
Ile asubuhi unaamka unaanza kwanza kuitafuta wallet, unapapasa suruali unaikuta iko mfuko wa nyuma.

Issue inakuja kwenye kuifungua. Aisee...unachokumbuka ni kwamba jana yake ulipita kwa wakala ukatoa laki 2, labda elfu hamsini ukamtumia mdogo wako ambaye yuko Chuo.

Swali ni je, kwenye ile laki na nusu iliyosalia, ulitumia sh ngapi na bakaa ni sh ngapi?

Ukikuta imebaki 7,500/= lazima upate wenge urudi kulala [emoji23], ukikuta imebaki walau 70,000/= lazima ujisogeze tena kwenye ki-pub cha jirani ukazimue kwa furaha [emoji23]

Maisha haya...
 
Mla Bata

Dogo anadhan tumeanza juzi kuchezea hela, mimi mwaka 2014 nilishawahi kutumia million 4 kwa starehe ya siku moja, hapo nimepanga uswahilini ndani sina kitu cha maana, uki-adjust for inflation hio ni kama 6m kwa sasa. Unaweza kusema nilinunua IST af nikaiwasha moto. Lkn toka hapo nikaapa sitokuja kuwa mpuuzi kiasi hicho

Sasa wewe endelea unadhan ni sifa kutumia pesa hivyo, utakutana na shida moja siku moja ikunyooshe na huna hata mia, akili zitarudi, lkn zitaondoka tena sababu umejiendekeza.

#WeEndeleaTu (Mwana FA)

Huyo anazungumza hivyo mawili, either akikaa mwenyewe nafsi inamuuma na kujiona mjinga ama hata hiyo pesa yenyewe hajaishika na kuifanyia ujinga huo anachangamsha genge tu πŸ˜‚πŸ˜‚.

All in all hapangiwi mtu maisha fainali ni uzeeni.
 
Back
Top Bottom