Ulichowaambia ni ukweli mtupu.
Nina vijana wangu nikiwaambia mimi nilikuwa naosha magari,lakini nilikuwa natunza hela kidogo kidogo kwa malengo na pombe ilikuwa mbali nami kwa kipindi hicho,labda tudemu kwa mbali kwa kipindi hicho. Nikafungua duka. Nikanunulia gari la kwanza miaka miwili baadae,hapo nina uwanja,najenga taratibuuu.
Kikubwa malengo. Hawa madogo wa siku hizi kila kitu wanaona wanachelewa. Wanafikiri zipo hela za kudondoka moja kwa moja nyingi,halafu afanye mambo yote kwa mkupuo.
Ndani ya mada,kipindi mimi nina mtaji wa milioni 40. Mjombaangu akawa anastafu anapata kiinua mgongo cha milioni 250. Nikampa plan hizo pesa afanyie nini,akaona kama nazimendea hela zake. Nikamwambia mimi sina shida hata na senti 5 yako ila nakusaidia ksbb nawajua nyie wastaafu,utarudi kunisumbua muda si mrefu.
Nikamwambia mimi nina milioni 40 tu,lakini ninazo nyingi kuliko zako milioni 250. Kwani miaka miwili mingi?. Nikawa na mtaji wa kama milioni 90+,anakuja kukumbuka yale maneno yangu na anaona aibu hata kunisalimia. Kachokaa hatari