Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

Wadogo zangu mnapotea, bila nidhamu ya pesa utaenda kukariri plate number za wenzako

'Kaka' acheni wadogo zako wale bata hawana majukumu; wakiwa na majukumu wataanza kusave. Kwanini wajitese wakati huu ilhai bado wana nafasi ya kula bata? Bata inanoga ujanani; uzeeni unakuwa ni mtu wa kliniki ya presha, macho figo, filigisi, nk.....hutakuwa na nafasi ya kula bata.
Hahahaa

Ila walosema life starts at 40 walimaanisha mda wa kula matunda ya jasho lako ni hapo 40
 
Kiongozi pesa inatabia yake kama binadamu sasa nikuomba mungu uwe na damu ya pesa yani uendane nayo ukiona mtu anapata pesa anachezea usimlaumu uyo mtu yeye na pesa hawandani kwakua tunaitaji pesa ili kutatua changamoto za maisha ya kila siku tunazitafuta ingekuwa pesa sawa na mke amini nakwambia wengi wangeachana nayo


Swali je una damu ya pesa?

Jipime kwa kuangalia kipato chako je kinaendana na maendeleo uliyo nayo ukiona unashika pesa unashia chezeaa tambua huna damu ya pesa kwaiyo wewe chezea tu una damu ya shida ndio maana unashika pesa baada ya mda furani unakosa hata shilingi Mia ya kulinda mfuko
 
Mla Bata

Dogo anadhan tumeanza juzi kuchezea hela, mimi mwaka 2014 nilishawahi kutumia million 4 kwa starehe ya siku moja, hapo nimepanga uswahilini ndani sina kitu cha maana, uki-adjust for inflation hio ni kama 6m kwa sasa. Unaweza kusema nilinunua IST af nikaiwasha moto. Lkn toka hapo nikaapa sitokuja kuwa mpuuzi kiasi hicho

Sasa wewe endelea unadhan ni sifa kutumia pesa hivyo, utakutana na shida moja siku moja ikunyooshe na huna hata mia, akili zitarudi, lkn zitaondoka tena sababu umejiendekeza.

#WeEndeleaTu (Mwana FA)
Ukiwa mtafutaji alafu usiweke akiba hakika wewe ni bwege ..Akiba muhimu sana kwenye life mkuu .Hilo linazingatiwa kikamilifu
 
Huyo anazungumza hivyo mawili, either akikaa mwenyewe nafsi inamuuma na kujiona mjinga ama hata hiyo pesa yenyewe hajaishika na kuifanyia ujinga huo anachangamsha genge tu [emoji23][emoji23].

All in all hapangiwi mtu maisha fainali ni uzeeni.
Sijashika million ??
 
Unasema basi unywe tu bia moja ukimaliza unaskia huu wimbo

Haka ka-dame kazuri joh kako vero
Kisham-sham kinyam kitam-tam
Shuka na ngeus siezi mind ata kapedo
Dame ni kafupi kanapenda magendo
Ngoma ni kali uliza Makurutu gang gang
Imebaki shangwe, kelele na nderemo (wueh!)
Shamra-shamra kelele na nderemo (ayayaya!)
Shamra shamra kelele na nderemo (wueh!)

Nidhamu itatoka wapi😅😅😅
Niaje msupa...
Niko na talent....
Naweza fungua bra na mkono moja,wataka kuona?!
Okay,keti chini ah geuka hivi😂😂😂😂
 
Mkuu Hilo swala vijana ni gumu hasa kwa nzia miaka 16 mpaka 25 hawawezi kuwa na hio nizamu kwanza bado ujana mwingi na hio stage lazima upitie na usipoipitia utaipitia uzeeni hata Mimi nilipitia na Sasa nimekuwa na nizamu kubwa Sana ya pesa na kuna wakati nawaza hio stegi ningekuwa mbali Sana kiuchumi Kama ningekuwa na hio nizamu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Hilo swala vijana ni gumu hasa kwa nzia miaka 16 mpaka 25 hawawezi kuwa na hio nizamu kwanza bado ujana mwingi na hio stage lazima upitie na usipoipitia utaipitia uzeeni hata Mimi nilipitia na Sasa nimekuwa na nizamu kubwa Sana ya pesa na kuna wakati nawaza hio stegi ningekuwa mbali Sana kiuchumi Kama ningekuwa na hio nizamu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu ukiwaza ungekuwa mbali waza je ungekufa so shukuru Mungu kwa uzima na uhai ulionao mpaka leo
 
Ulichowaambia ni ukweli mtupu.

Nina vijana wangu nikiwaambia mimi nilikuwa naosha magari,lakini nilikuwa natunza hela kidogo kidogo kwa malengo na pombe ilikuwa mbali nami kwa kipindi hicho,labda tudemu kwa mbali kwa kipindi hicho. Nikafungua duka. Nikanunulia gari la kwanza miaka miwili baadae,hapo nina uwanja,najenga taratibuuu.

Kikubwa malengo. Hawa madogo wa siku hizi kila kitu wanaona wanachelewa. Wanafikiri zipo hela za kudondoka moja kwa moja nyingi,halafu afanye mambo yote kwa mkupuo.


Ndani ya mada,kipindi mimi nina mtaji wa milioni 40. Mjombaangu akawa anastafu anapata kiinua mgongo cha milioni 250. Nikampa plan hizo pesa afanyie nini,akaona kama nazimendea hela zake. Nikamwambia mimi sina shida hata na senti 5 yako ila nakusaidia ksbb nawajua nyie wastaafu,utarudi kunisumbua muda si mrefu.

Nikamwambia mimi nina milioni 40 tu,lakini ninazo nyingi kuliko zako milioni 250. Kwani miaka miwili mingi?. Nikawa na mtaji wa kama milioni 90+,anakuja kukumbuka yale maneno yangu na anaona aibu hata kunisalimia. Kachokaa hatari
Daaah noma hii.
 
Umenikumbusha fundi wangu mmoja alikuwa akinijengea kibanda mahali fulani, ilikuwa nikimlipa maybe 350k basi atakuja kazini tena baada ya siku tatu hadi nne hela zikimwishia.

Kuna siku nimemlipa 700k baada ya siku mbili anasema anaumwa hana hata mia ya kwenda Hospitali, kumbe jana yake alikesha Kitambaa Cheupe na wale slay queens.

Yaani totozi na gambe ndiyo moto wa kuchomea hela za wengi
Bila kusahau kamari na madawa ya kulevya.

Bora totoz kuliko vyote hapo.
 
Nidhamu ya pesa ni mtihani mzito shekh!

Imagine umehangaika zako mara umepiga “mshindo” wako alafu ukiangalia ndio weekend imeingia kila mahali ukipita unamsikia mariooo

“Shiiiiiiii badiiiii”
“nilikuwa na wanangu kina chinooo”
“niseme nsisemee, semaaaa” X 2

Ukizidi kusogea unamsikia jux nae ,
“huyuuu demu ake naniiii, anpandisha midadiii, anitafutia lawama,……….”

Ukisema uzame ndaniii tu kwisha habari yako, unakuta watoto wamepanda juu ya meza wanacheza na wamependeza balaaa!

Unaendaje kulala mkuu, au tukuulize,

we kuwezaaa???

Nyie achenii banaa starehe ni tamuuu 😂😂

Tukiamka asubuhi ndio majuto huanza.
🥴
 
Yaan ndo kinachofanya huu uzi uwe interesting sana, story zote ni mulemule, mizunguko tofauti ila conclusion ni moja.

Hivi ushawahi kumka ukaanza kujisachi kila kona angalau ufikishe 3000 ukanywe supu na jana yake umetumia kama laki?
Ahhahh,aisee kumbe hili pepo linatukuta wengi,sasaiv starehe za makundi ya chawa sitaki kabisa
 
Kaka niko pamoja na wewe...
Ukifika unasema ngoja niagize Nyagi ndogo na Vibia tuwili vya kutolea uchovu na aibu.
Mara paap wana hawa hapa sijui nini kinaendelea...
Asubuhi Lak imekata mtoto anavaa asepe...Dah.Hii miaka kushinda Stareh inahitajika Juhudi
Miaka kama mi 4 nyuma nilikuwa nafanya kampuni moja hivi siku hyo nikawaambia likizo yangu nitaondoka wakasema hakuna wa kushika nafasi yako kama uza upige kazi. Nikawaambia hakuna noma.

Siku ya siku nimeenda nikaitwa hela ya likizo imeshawekwa na marupurupu kadhaa, balance kama laki 9 hivi. Nikasema yees jioni nikawashtua wanangu wawili hapo kazin nikawaambia oya tukapunguze kidogo hizi chenchi.

Hao tukatoka na jamaa wawili hadi bar agiza msosi kwanza zikaanza chupa. Mara washkaji simu zikaanza kuwashtua madem zao naona wanakuja wawili wawili meza ikajaa na washkaji wengine wakajiunga backet ikaww haitoshi sasa ni kreti linaletwa bill kwangu, wengine saint Anna bill kwangu.

Asee kufika mida ya saa nane hivi kucheki balance nina laki 3 pekee. Na nilipanga kesho asubuhi nikanunueTv kubwa hiyo hela nikatoa yote bank.😂😂
Kesho yake nikabaki na mawazo tu.
 
Back
Top Bottom