Wafahamu Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania. Tunaanza na Ramadhan Omari Mapuri

Huwezi kujua kuwa watu wanajali matumbo Yao kuliko kuwatumikia wananchi. Kama lengo ni UCHAGUZI uwe HURU,TUME ya UCHAGUZI iwe HURU hakuna namna nyingine.
Tumeccm na Polisiccm watahesabu kura zao haramu za kishetani lakini kura za watanzania hawataziona kwani wengi hawatajitokeza kupiga kura kisha Tumeccm itangaze kinyume na chaguo lao
 
Na nyie shindeni muunde Tume yenu,hata kule Kenya Tume Ina wajumbe ambao ni Wafuasi wa Vyama.

Mwisho hata referee anaweza kuwa Yanga au Simba lakini Yuko kati kuamua dimba.
Angalau Kenya unaona kabisa kuna baadhi ya wajumbe wa tume hawakubaliani na baadhi ya maamuzi ya tume.

Sasa mkuu hebu fikiria kweli mtu kama Ramadhan Omar Mapuri ambaye ni Katibu mwenezi mstaafu na kada mtiifu wa CCM anawezaje kuwa mjumbe wa inayoitwa tume huru ya uchaguzi?

Unajua kuna vitu vingine CCM inavifanya bila hata aibu.

Bora wangeweka wajumbe ambao ni makada wa CCM ila wasiofahamika kwa umma kama kina Mapuri lakini kumuweka mtu kama Mapuri kwa mfano ni kuwakosea heshima wananchi.
 
Tumeccm na Polisiccm sasa ni janga la Taifa Nchi inaendeshwa kienyeji sana
 
Ibara 74(14) ya KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TZ inatamka
"Itakuwa ni marufuku kwa watu wanaohusika na uchaguzi kujiunga na chama chochote Cha siasa"

Watu hao kwa mujibu wa Ibara 74(15) ni
-Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi.
-Makamu mwenyekiti.
-Wajumbe wote wa tume ya uchaguzi.
-Mkurugenzi na watumishi wote wa tume ya uchaguzi
-Wasimamizi wote wa uchaguzi katika mji na wilaya zote.

Kuna uwezekano kweli akosekane mwanaccm hata mmoja katika watu wote hao walioainishwa hapo juu, wakati baadhi yao pia ni wateule wa rais!

Bado Kuna watu wanaamini uwanja ni sawa na kweli kuna "uchaguzi"!
 
Tanzania hakuna Tume ya uchaguzi, Tanzania kuna kikundi haramu Tumeccm hicho kikundi cha kishetani ndicho kinapora haki ya kuchagua na kuchaguliwa, Dawa ya kukomesha vikundi vya hovyo hovyo kama hiyo Tumeccm ni kuwafungulia kesi mahakama za kimtaifa ili ccm wazinduke waache udikiteta wao
 
Tumeccm kikundi hatarishi kwa usitawi wa Demokrasia yafaa sasa kishitakiwe kwenye mahakama za kimtaifa ili ccm wapate kujua kuwa watanzania wameamka hawataki kuburuzwa
 
Mapuri alikuwa katibu mwenezi wa CCM
G55 ni mapunguani. Ni mpango uliasisiwa na CCM kwa mgongo wa MBOWE
 
Wasiokubalina ni Kwa sababu wanaegemea Vyama tofauti,mpaka hapo Kuna maana gani? Ruto aliiba uchaguzi
 
Kihistoria ni mnyamwezi wa Tabora wazazi wake walilowea Zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…