Wafahamu Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania. Tunaanza na Ramadhan Omari Mapuri

Wafahamu Wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania. Tunaanza na Ramadhan Omari Mapuri

View attachment 3302178

Mzee Ramadhan Omari Mapuri amehudumu kama kiongozi Mwandamizi kwenye serikali na kwenye Chama cha Mapinduzi, Mapuri ni mwanaccm Mtiifu mwenye kadi hai ya uanachama.(Namba yake kadi tutaiweka hapa)

Huyu ni Mjumbe wa kinachoitwa Tume Huru ya Uchaguzi na ni Mzanzibar.wa Kuzaliwa.

Wasifu wake kwa ufupi huu hapa, Wasifu wake mwingine utaongezwa kwa kadri ya tutakavyopata Taarifa, hatutampunja.

View attachment 3302176

Toa maoni yako.

Muhimu: Tutaendelea kuleta Wasifu wa Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ili kila mtu awajue, hii ni kwa sababu Si kosa kisheria kuwafahamu Watumishi wa Umma, na hasa kwenye masuala ya uaminifu na uadilifu.
"TUME HURU YA UCHAFUZI"
Umetoa ushahidi wa kisayansi. Hebu endelea na hao wateule wengine. Sina shaka wote ni watu wa CCM, halafu tunaambiwa hiyo ni "Tume Huru ya Uchaguzi"!
Na kama haitosahi kwa kujiteua huko ndani ya CCM kuwa mgombea pekee, sasa tunaletewa ulaghai mwingine wa uchaguzi!
 
Wasiokubalina ni Kwa sababu wanaegemea Vyama tofauti,mpaka hapo Kuna maana gani? Ruto aliiba uchaguzi
Bora hata hao wanaokataa kukubaliana wanaonekana wa vyama vingine kwa maana tayari kuna mchanganyiko wa wajumbe toka vyama vingine.

Lakini kwa tume yetu mtu ambaye anafahamika na umma mzima ni kada wa chama na ameshawahi kuwa msemaji wa chama halafu unamuweka kama mjumbe wa tume tena inayoitwa huru huoni ni dhihaka mkuu?

Hata wapinzani wakidai mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi basi wasikilizwe wana hoja zenye mashiko kwasababu kama ni kubugi ni chama tawala ndiyo wamebugi kuweka wajumbe wa tume ambao ni makada wawe wasimamizi wa uchaguzi unaohusisha vyama vyote.
 
View attachment 3302178

Mzee Ramadhan Omari Mapuri amehudumu kama kiongozi Mwandamizi kwenye serikali na kwenye Chama cha Mapinduzi, Mapuri ni mwanaccm Mtiifu mwenye kadi hai ya uanachama.(Namba yake kadi tutaiweka hapa)

Huyu ni Mjumbe wa kinachoitwa Tume Huru ya Uchaguzi na ni Mzanzibar.wa Kuzaliwa.

Wasifu wake kwa ufupi huu hapa, Wasifu wake mwingine utaongezwa kwa kadri ya tutakavyopata Taarifa, hatutampunja.

View attachment 3302176

Toa maoni yako.

Muhimu: Tutaendelea kuleta Wasifu wa Wajumbe wote wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania ili kila mtu awajue, hii ni kwa sababu Si kosa kisheria kuwafahamu Watumishi wa Umma, na hasa kwenye masuala ya uaminifu na uadilifu.
Chadema wapo sahihi tunahitaji katiba mpya yenye tume huru ya uchaguzi
 
Haihitaji hata D moja kung'amua itakayofanya tume hii kutangaza majibu. Elimu ngumbaru inatosha kujua, hawa hawatafanya chama chao kianguke mikononi mwao. Dhana ya no reforms no election hapa ndipo inapopata mashiko
 
Polisiccm na Tumeccm wanaenda kubaka kunajis sanduku la kura haki ya kuchagua kuchaguliwa imeporwa na ccm kwa njia za kishetani
Pambaneni nao kwa matendo sio maneno. Mkiwashindwa unganeni nao.

Naichukia sana siasa
 
Hiki kinachodaiwa na CHADEMA sio takwa lao peke yao, ni takwa la kila mtanzania mwenye akili sawasawa.

Ifike wakati kila mtanzania awe na uhakika kwamba kura yake anayoenda kuipangia mstari kwenye jua kali inahesabika na inaheshimika.

Watawala na wanasiasa hawawezi hata siku moja kuwaheshimu wananchi kama wana uhakika maamuzi yao katika sanduku la kura hayana madhara katika vyeo vyao.

Nawaunga mkono CHADEMA, huwezi kuendelea kushiriki chaguzi ambazo kila baada ya uchaguzi una kazi ya kulalamika.

Ndani ya mtungi kuna nyoka, kila ukiingiza mkono nyoka anakugonga, ukiendelea kuingiza mkono wewe si utakuwa kichaa?
​
😂
 
Back
Top Bottom