DOKEZO Wafanyabiashara Kariakoo kugoma Mei 15, 2023

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tunakokwenda kubaya kodi zitakua hazilipwi tutaanza kukomoana mimi kama mfanyabiashara wa kkoo kesho nitakua front

Anyway, ngoja na mimi kesho nisifungue, tuone itakuwaje
 
Ni kweli, Na Hatufungui KWELI...

Kama maisha yanaenda bila k.koo kaeni sasa tuone mwisho wake.

Ubunifu zero,kodi kila eneo usifanye hiki hawa hapa,usiweke hiki Hawa hapa

Yani unashindwa hata waelewa wanachotaka ni nini na miaka yote marais wengine walikua wanaendeshaje Nchi!
 

Huwajui kkoo vzr hawachelewi kukuchomea duka
 
Labla baadhi ila si wote watafunga mtanzania na mgomo wapi na wapi 🤷🏼‍♀️
 
Nchi hii inahujumiwa na sera mbovu za kodi kwa makusudi! Lengo la kodi ni kufukarisha wananchi wa kipato cha chini. Ndiyo maana TRA wapo kwa lengo la kuwabana machinga, mamantilie, baa na vigrosary mitaani, watu wasio na mitaji au wenye mitaji midogo.
Hiyo ndiyo kazi ya TRA ambao wako wengi kuliko uhalisia, na wanalipwa mishahara minono ili wafanye kazi yao kwa nguvu zote.
 
Tuna mifumo mobovu sana eb we fikiria tanzania tuna agiza samaki toka nje , tanzania tuna agiza toothpick toka nje .... halafu kama taifa tuna pata 1% kutokana na mazao ya baharini (including maziwa) imagine
 
Wafanyabiashara wa Kariakoo kufungwa maduka siku ya Jumatatu tarehe 15/05/2023

 
What!
Ninawabembeleza wafanyabiashara wa Kariakoo wasigome iyo kesho.
Endapo watagoma, basi watakuwa wamejifuta kwenye ulimwengu wa biashara kwenye nchi hii.
Tuliwakabidhi kijiti cha kuendesha biashara za ndani na za kimataifa za nchi hii!
Endapo watatuangusha hiyo kesho 'nitazielekeza' halmashauri tano za jiji la Dar kufuta leseni za biashara za wafanya biashara wote wa Dar (K/koo) na kuielekeza wizara ya viwanda na biashara ku take over hizo biashara.
Kwa mikopo waliyokuwa nayo, wafanya biashara wa Kariakoo, watajikuta wamekuwa watu masikini kabisa katika nchi hii.
Chonde chonde... Msigome. Itakula kwenu...
Plz n so plz... Dont try this at Kariakoo!
 
Kwani ACP Muroto si bado yupo? Waandamane waone
 
Mm nimembiwa na mmoja wa wafanyabiashara kariakoo kuwa wanagomea tozo zinazolazimishwa mizigo ya stoo
 
Ila wabongo nakuandamana wapi na wapi jaman maana wengi tunahofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…