Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

A bit too late.. Wana mbeleko kubwa ya chama chawala
I think wachina ni much better kulik wabongo. Mbongo anachukua kiatu kipya cha mchina, anaenda kukisugua soli na ngozi halafu anakuja kukwambia ni mtumba anakupiga bei mara tatu ya ile ungetumia kununua kiatu kipya.
Waulize wale mafundi viatu wanaopatikana maeneo vinapouzwa viatu, unadhani kazi yao ni kupunguza urefu kama vitakuzidi urefu?
 
Wabongo wengi hawawezi kuwaza hivi kwa sababu akili hawana.
 
Hata akiuza mara 8 ni afadhar mbongo auze hivyo na atajirike kuliko hawa wachina na wahindi. Mbongo akiuza hivyo mzunguko wa pesa yake utaenda kwa wabongo wengine kwa kuajiri, kununua matumizi ya nyumbani kwake.Kuliko Hawa wanaopeleka kila kitu kwao.
 
Hata akiuza mara 8 ni afadhar mbongo auze hivyo na atajirike kuliko hawa wachina na wahindi. Mbongo akiuza hivyo mzunguko wa pesa yake utaenda kwa wabongo wengine kwa kuajiri, kununua matumizi ya nyumbani kwake.Kuliko Hawa wanaopeleka kila kitu kwao.
Atajirike yeye kwa kukutia hasara wewe? Kama hafikiri kuhusu wewe na hasara utakazopata basi hana faida, ni bora hata ya Mhindi na Mchina wanaokupa kitu kulingana na thamani na kodi wanalipa,
 
Atajirike yeye kwa kukutia hasara wewe? Kama hafikiri kuhusu wewe na hasara utakazopata basi hana faida, ni bora hata ya Mhindi na Mchina wanaokupa kitu kulingana na thamani na kodi wanalipa,
Kila Mhindi bilionea unayemuona bongo ana uraia Canada au UK huku Tanzania ananyonya tu.

Iddi Amin alipowapa masharti ya kupokea uraia wa Uganda walikataa sababu ni shithole country, ila muda huohuo walikuwa mitaa ya Kampala na Entebbe wanafanya biashara. Akawapa miezi mitatu wahame bila kitu, Wahindi 80,000 wakakimbilia Uingereza chanzo kidogo tu ni mgogoro wa kukataa uraia.

Mchina akiuza mitumba yake anapeleka faida China, huku anabaki na hela ya kula tu. Thamani ya shilingi inaporomoka kila siku, hela inatoka kwenye mzunguko wa bongo inaenda nje.

Ukitoa shilingi 10,000 kununua tshirt ya Mchina, ile tshirt kaichukua kwa 2,000 kwao akaongeza usafiri na kodi maybe 2,000 nyingine faida anakuwa na 6,000. Mbongo akiuza tshirt ileile kwa 12,000 kainunua kwa 3,000 sababu Wachina wanauziana kwa bei ndogo mbongo hawezi nunua kwa 2,000. Na akiongeza 2,000 gharama. Anapata faida ya 7,000.

6,000 faida ya Mchina atatoa kama 1,000 ya matumizi ile 5,000 arudishe China kujenga kiwanda, kuajiri, kujenga makazi, kununua hisa, etc. Wakati ile faida ya 7,000 ya mbongo akitoa matumizi yote na uwekezaji wote ni hapahapa bongo. Ukitoa 10,000 kwa Mchina unajikuta umeondoa 5,000 kwenye mzunguko wa fedha nchini na umeua thamani ya TZS.
 
Ni mjinga gani anaweza kununua box la kigae kwa 35,000/= wakati Mchina box hilohilo na kampuni hiyo hiyo anauza 25,000/=
Hoja ya Mzunguko wa Pesa kubaki ndani ni uongo hata hao wafanyabiashara wanafata bidhaa China na pesa inaenda nje kila uchwao wao wauze reasonable Price uone kama kuna mtu atanunua kwa Mchina
 
Hii ni aina nyingine ya Xenophobia iliyopo katika nchi ya Tanzania
 
Wachina wanawazidi ujanja.

Wakati nyinyi mnalalamika watu wanauza nje y maduka ynu, wao wameingoa mtaani kaboisa chinga. Na nyinyi jifunzeni mbinu hizo, mmejaza "mawinga" Wachina wamewastukia, sasa yeye huyo anauza jumla, anauza rejareja, chinga yeye, winga yeye, na mizigo yake anabeba mwenyewe, na mteja anampelekea mpaka anapotaka.

Wasiondolewe, waendelee kuwafundisha Wagtanzania kuchapa kazi, siyo uzembe wenu mliouzowea.

Anachokiweza kwa ufanisi Mtanzania ni wizi na ubabaishaji.
 
Hilo swala nalielewa vizuri sana. Issue yangu ni kwanini huyo Mtanzania asiende China au India akawanyonye ili awaplekee hela watanzania wenzake, baala yake na yeue anaungana nao kwenye kuwaumiza?
Wenzake wanaumiza ugenini, yeye anawaumiza wa nyimbani?
Mtu aje kukumiza Usukumani kisa hapeleki hela nje bali anaenda kujenga uchagani?
 
Hii pia ni point muhimu, ni muunge mkono mtanzania anayenitia hasara wakati wafanyabiashara wa kitanzania wenyewe wanalalamikiana kama hapa
T14 Armata hapa unasemaje? Mimi kwangu naona bora ya mhindi na mchina wanaoniuzia kiatu kipya kwa shilingi 20,000 kuliko mbongo anayenunua kwa mchina halafu anaenda kuvisugua ngozi na soli vioneka ni european used halafu ananiuzia 70,000 hadi 90,000/-
 
Ushauri wangu tuweke Masharti Magumu kwao ila sio kuwazuia ni kweli nilishawahi kusikia kuna baadhi ya bidhaa za India ili uwe wakala huku Africa nilazima uwe muhindi pia ukiona muhindi amejenga Bongo ujue ni nyumba ya biashara wengi wanama apartment Canada na familia zao zipo huko, au ukutane na Muhindi choko aliekuja kama kibarua ndio kidogo wanawajengea madem zao wakiwazalisha wenzie wakijua tu jua watamludishwa India
Pili hawa jamaa mie nahisi Kuna mkono wa serikari zao kupitia mikopo nafuu kutoka kwenye Benk zao ndio maana wanakuwa na mitaji na bidhaa za kutosha tofauti na kwetu hapa mabenki mengi ni fully Commercial hivyo kuwashindanisha na wafanyabiashara wetu inakuwa ngumu maana watu wana stress za malejesho
Kwakweli kuna factor nyingi za kuangalia japo wafanyabiashara wetu nao sometime wazinguaji
 
Watanzania ni wavivu sana! Kuzalisha bidhaa hawawezi. Sawa! Kuuza mako wanauza kiduwanzi sana, mara zote wateja ndio tunawaomba watuuzie, mako kuna mlolongo mrefu sana.
Unakuta mtu ameweka tangazo la bidhaa halieleweki, upimpigia simu akutajie bei, utapiga mara kadhaa, anakujibu nakutumia. Ukilipia bidhaa mpaka akakusafirishie ni kipengele. Yaani Karne ya 21 watu wanaishi kiduwanzi sana
 
Wakiondoa wachina waondoe na mawinga bei ziandikwe kwenye kila bidhaa. Maana mawinga n wezi wapya
 
Work permit ya mgeni kufanya kazi Tanzania kwa mwaka ni mil 2 mpaka 5. Nakazi zenyewe nizile Professional, sasa naomba uniambie kama Kuna Mchina anapewa Work-permit yakua Chinga kaliakoo.

Na mtu akishakua machinga maana yake anauza bila kutoa risiti, Je tumeruhusu wageni kuuza bidhaa bila kutoa risiti?. Watalipaje Kodi stahiki?.

Na kigezo Cha Work-permit nikufanya kazi zile professional ambazo wazawa hawaziwezi. Sasa niambie umachinga umewashinda watanzania?.
 
Wakiondoa wachina waondoe na mawinga bei ziandikwe kwenye kila bidhaa. Maana mawinga n wezi wapya
Hawa Mawinga ndio janga, Sijui kwa nini Serikali inawalea. Au hao machinga wanaouza bidhaa nje ya maduka makubwa sijui kwa nini wanashindwa kuondolewa, Serikali inalalamika walipaji Kodi directly niwatz wasiozidi mil 2 kwenye nchi yenye watu wazima zaidi ya mil 30 . Halafu wanajaza machinga Kila eneo.
 
Hata akiuza mara 8 ni afadhar mbongo auze hivyo na atajirike kuliko hawa wachina na wahindi. Mbongo akiuza hivyo mzunguko wa pesa yake utaenda kwa wabongo wengine kwa kuajiri, kununua matumizi ya nyumbani kwake.Kuliko Hawa wanaopeleka kila kitu kwao.
Si kweli, kuuza kwa gharama za juu ni kuchochea inflation na mwisho ni kuangusha sarafu

Kwa uchumi wa watu wetu ni Bora mchina auze bei ndogo kuliko mzawa kuuza bei juu
 
Poleni sana nyie majamaa ya kariakoo.

Ila hao ndugu zake Bruce Lee kuondoka ni ngumu sana.

Labda kama wamekiuka masharti ya permits zao, otherwise wapo sana tu.
 
Si kweli, kuuza kwa gharama za juu ni kuchochea inflation na mwisho ni kuangusha sarafu

Kwa uchumi wa watu wetu ni Bora mchina auze bei ndogo kuliko mzawa kuuza bei juu
Auze bei ndogo dukani kwake lkn sio auze kama machinga mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…