Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Mbona Treni ipo katikati ya mji?. Na hata uwanja wa ndege upo katikati ya mji ila stendi ya mabasi wamepeleka mafichoni.
Viwanja vya ndege vyote hapa nchini na nje ya nchi huwa vinatakiwa kujengwa nje ya mji....
Sema kwa Mkoa wetu huu,Mipango miji huwa wanaruhusu ujenzi holela na watu kufanya ujenzi kwenye maeneo yaliyotengwa kwa maviwanda makubwa na miundombinu kama hiyo..mm
 
kurasa zote nimesoma sijaona aliyeongelea sababu za mabasi kukwepa stendi ya mkoa
Mabasi hayakwepi lazima yaingie stand ila huko kote yanakopita kama mfano linatoka tanga kuna abiria wa bunju litawaacha bunju kabla ya kuingia stand ya magufuli kisha kama linaenda urafiki litaondoka na wanaoelekea kule. Same kama linaenda tanga liaanzia urafk litakuja ana abiria kutoka huko liingie magufuli kisha likitoka lipite tegeta likute abiriaa libebe bu ju hivyo.
Sasa hao wauza crips wanalazimisha yani naishi bunju gari litapita bunju eti gari lisipakie niende nikapande pale magufuli na nikiwa narudi lipire bunju kinaache magufuli then nianze tena tafta usafiri wa kurudi bunju. Hizo ni akili au matope
 
Kitu ambacho huelewi ni kwamba abiria wanaooelekwa urafiki au shekilango ni kama offer ya mwenye basi na sio sheria. Ni mwenye basi kumjali mteja wake na kumpunguzia gharama zisizo za lazima.
Hiko sikatai lakini mfumo ilitakiwa Mfumo wote wa Mabasi makubwa:Kuanzia stendi hadi Karakana ni zikae nje ya mji....

Soko huru bila kufuata mipango mji ni ukichaa,,,,ndiyo maana sikuhizi kuna sheri mpaka karibu na Masoko....Shule zimejengwa karibu na Barabara
 
Mimi nafikiri mabasi yote yawe yanaingia na kutoka stendi ya JPM lakini yasizuiliwe kupakia na kushusha vituo vingine! Basi linaloenda mikoani lipakie abiria huko kwenye vituo vingine liingie stendi kujazia abiria, hivyo hivyo likitoka mkoani liingie stend kushusha abiria wanaotaka kushuka then liendelea kwenda kushusha abiria vituo vingine.
Vile vile serikali ijenge vituo vingine zaidi vya kushusha na kupakia abiria mji wa Dar umepanuka zaidi.
 
🤣🤣🤣
Ulishatoa mada, jukwaa zima limetofautiana na wewe ungekuwa muungwana ungejitafakari lakini wewe michango ya kukomaa naiona unajibu kila mchango wa mwanajukwaa. Katafute biashara nyingine.
mi naona poa hajakosea,,,,Hapa ni sehemu ya kubadilishana mawazo mkuu....
Inasaidia mtu kuona jambo kwa angle nyingine.
 
Mimi mfano nakaa mbezi ila nikifika kituoni nataka kwenda Moro naambiwa usafiri wa mabasi ya Abood haupatikani hapo ...Yapo Urafiki. Basi linajazia urafiki then linapita juu kwa juu Mbezi bila ya kuingia ndani stendi!

Zaidi ya asilimia 75-80 ya basi zinazoondoka alfajiri haziingii ndani ya stendi ya Magufuli badala yake zinapita juu kwa juu.

Wamiliki wa mabasi wanaihijumu serikali , wanaikosesha serikali mapato yake ya getini. Pia wanawahujumu watanzania kwa kuwakosesha ajira
 
  • Abiria wanaoishi nje ya stendi ya Magufuli,,,wanatakiwa wafike stendi kwa mfumo wa usafiri wa ndani ya jiji....(Daladala,bolt,Bajaaj,boda)
  • Kwani unafkiri Ubungo ilikuwa karibu kwa kila mtu,,,watu wa Bunju,Chanika,Mbande,Kibada,Ununio,Mbweni,Kimbiji....ushawahi kaa hayo maeneo ,,,nayo yapo mbali kutoka Ubungo.
Tutaangalia interest ya abiria. Ndio maana huko kote Kuna mabasi yanaanza huko. Kwa watu wa mbande, kimbiji etc Kuna stendi Kigamboni, chanika, Temeke nk. Kwa bunju mabasi yanapitia njia ya bagamoyo au anaweza kukimbilia basi magomeni au urafiki Lazima tuwa appreciate wenye mabasi kwa kuwajali abiria baadala ya kulaumu.
 
  • Abiria wanaoishi nje ya stendi ya Magufuli,,,wanatakiwa wafike stendi kwa mfumo wa usafiri wa ndani ya jiji....(Daladala,bolt,Bajaaj,boda)
  • Kwani unafkiri Ubungo ilikuwa karibu kwa kila mtu,,,watu wa Bunju,Chanika,Mbande,Kibada,Ununio,Mbweni,Kimbiji....ushawahi kaa hayo maeneo ,,,nayo yapo mbali kutoka Ubungo.
Lazima utambue kwamba katika suala la usafiri abiria ndiye center ( ndiye customer) ya jambo hilo.

Chochote kinachofanywa ni lazima yaangaliwe masilahi yake.

Anapaswa asogezewe huduma hiyo kwa urahisi kila iwezekanavyo. Yahani ikitokea basi likasema lina magari ya kampuni ya kuwapeleka au kuwachukua majumbani hilo lipongezwe.

Ninyi mnataka mtu atumie shilingi 30,000 kutoka Mbezi kwenda Mbande usiku si ndiyo?
 
S
Siku zote biashara haitakiwi kutegemea Stendi, bali stendi ndio inapaswa kutegemea biashara yako, shida ni hawa wafanyabiashara walidanganywa na ccm

Nimepita hapo stendi zaidi ya mara 50 lakini sikuwahi kununua chochote, hii ni kwa sababu si lazima abiria kununua kitu hapo stendi, sasa wanacholilia ni nini?
Siyo kweli, biashara inategemea watu wanao kuzunguka pamoja na hao abiria, changamoto ya hizi biashara zilizoko kwenye stendi bidhaa huuzwa Kwa bei ya juu,(biashara nyingi ni za kulazimisha mteja anunue), hata mimi Huwa spendelei kununua vitu stendi, hata hivyo unatakiwa uuze bidhaa ambazo unajua wateja watazinunua na siyo unazo fikiria watanunua, (you have to sale what you know they are going to buy not what you what you think they are going to buy).
 
Abood Bus service

BM

Ally's star

Katarama

Happynation

Kilimanjaro

Tilisho

Kimbinyiko

Shabiby

Newforce

N.k

Ni miongoni mwa kampuni nyingi ambazo hazitaki kuingia Magufuli Bus terminal....usafiri wa asubuhi ni kazi sana , wanapita juu kwa juu
 
Sasa wenye Mabasi hawatakiwi waachwe huru kiasi hiko....
Lazima wafuate utaratibu,,,
Mana sasa hayo Mabasi hadi Chanika na Vijibweni nisha yaona.....

Hatakama tupo Soko huru lakini lazima vitu vifanyke kwa utaratibu...
Sidhani Kama wameachiwa. Wanapitia Mbezi na kulipa ushuuru ila Kama Kuna abiria wanaenda basi linapoishia wanapewa offer mpaka huko. Kwa mfano mabasi ya Tabora Dar, yanaishia Magomeni, lakini lazima yaingie Magufuli hata mabasi ya Dar Mwanza mengi ni shekilango lakini lazima yaingie Magufuli. Wanachojaribu kufanya Hawa wamiliki wa mabasi ni kuwafikia abiria kwa iharaka kutokana na ushindani na pia kuwapa offer abiria
 
Back
Top Bottom