Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Unyanyasaji wa vipi, terms za mkataba si wanazijua lakini..?
Wewe unaweza kwenda kukodi duka, ukawekeza kwenye furnitures, ulinzi, kwenda kukopa bank na kununua inventory; kama unajua baada ya miezi mitatu mwenye jengo baada ya miezi atakuja kukutoa.

Ndio maana kwenye mkataba wa biashara kuna kitu kinaitwa ‘customary term’ hiyo ni implied term ambayo mahakama itaizingatia ata isipokuwa expressed kwenye mkataba.

Logical inatumika kuangalia uhalisia wa scenario, uwezi kuvunja mkataba hasa wa kibiashara kiholela bila ya fidia.
 
NHC wakitoka hapo K/koo wahamie pale Fire wavunje yale majengo yote ya kikoloni, wajenge malls.

Kanjibhai wakahamie kando ya mji kama chanika n.k sio kukaa K/koo,posta na upanga tu.

Pia hii barabara ya kutoka fire kuelekea muhimbili kuna majengo mengi ya kizamani yanatakiwa kuvunjwa na kujengwa malls na maeneo mapya ya makazi.

Kwa utawala wa Mama Samia, Dar-es-salaam inaenda kuwa kama Dubai.
 
Naona kama wameadhibiwa wale kwasababu ya ule mgomo, sitegemei hao jamaa waje kupangishwa tena kwenye hayo majengo mbele ya safari, ndio wameshaondolewa kijanja hivyo.

Ngoja tuone kama kweli huo mradi mpya utaanza hivi karibuni, au ndio kwasababu wameshapata sababu ya kuwaondoa hao jamaa, basi na mambo mengine yatalala.
Wakubwa wana pesa za kusimamisha kitu hapo sio cha kawaida !!

Bear in mind sehemu hiyo ni hotcake kwa biashara !!
 
Huo ni mkataba wao tu; ila hiyo ni taasisi ya serikali kuna sheria mama ambayo ni universal kwa taasisi zote za serikali.

Ni vilaza tu, msiolewa including huyo lawyer alie draft huo mkataba.

Halafu Issue kubwa zaidi uwezi kupoteza biashara zaidi ya elfu moja na watu zaidi ya 10000 si ajabu wenye direct and indirect dependant na hizo biashara; pamoja na kodi za biashara kishamba ivyo.

This why people do investment appraisals first. Swala ambalo sidhani kama wamepelekewa kwenye baraza la mawaziri ku-justify uharibifu huo kwanza.

Kama pako vile kuna biashara hio uliosema ww.je pakiwekwa kisasa zaid?huoni kua ndio idadi itaongezeka
 
Wakavunje Michenzani Zanzibar kuna majengo nayo yamechoka mbaya na yakizamani; na wapangaji ZHC wanamikataba kama hiyo.

Zanzibar inapokea watalii wengi sana wakijenga nyumba mpya za kisasa na gated community; awawezi kukosa wazungu wakuwapangisha kama holiday let mwaka mzima kwa hela nyingi sana za kigeni.

Point hapo ni kwamba hela ina mipaka uwezi ku disrupt maisha ya watu kisa eneo unadhani linathamani zaidi; na wala huna alternative ya kuwapeleka watu unaowatoa kwenda kwingine huo ni unyanyasaji.
Vipi eneo likuwa lako usingeliendeleza?
 
Comment zako nyingi ni negative hata sehemu ya kutumia akili ndogo tu wewe huwezi bali unaendeshwa na mihemko ya kipumbavu,bila shaka utakua unapitia kwenye maisha magumu sana,hivyo unatumia hizi negative comment zako kama njia mojawapo ya kujifariji.
Hayo ni mawazo yako.Mimi ninasema ukweli. Ukiona huo ukweli ni negative kwako,pole .
 
NHC wakitoka hapo K/koo wahamie pale Fire wavunje yale majengo yote ya kikoloni, wajenge malls.

Kanjibhai wakahamie kando ya mji kama chanika n.k sio kukaa K/koo,posta na upanga tu.

Pia hii barabara ya kutoka fire kuelekea muhimbili kuna majengo mengi ya kizamani yanatakiwa kuvunjwa na kujengwa malls na maeneo mapya ya makazi.

Kwa utawala wa Mama Samia, Dar-es-salaam inaenda kuwa kama Dubai.

Nakazia hapo.dsm inatakiwa iwe ya kisasa zaid majengo ya kizamani yabaki bagamoyo na zenji [emoji28][emoji28]hatuitaji magofu tena
 
Kama pako vile kuna biashara hio uliosema ww.je pakiwekwa kisasa zaid?huoni kua ndio idadi itaongezeka
Wewe ndio umesema hivyo, lakini hakuna justification.

Unajuwa kwanini China supermarket za kigeni nyingi sana tena zenye majina makubwa zilifeli.

Kwasababu wachina wenye maisha ya kawaida washazoea kufanya manunuzi yao yote kwenye masoko ya mlundikano kama Kariakoo na yapo prime areas; serikali yao aitoi hayo maeneo kwa mtu yeyote.

Sasa wewe unajuaje hao watafanikiwa, wakati atujui hata hiyo PPP model itakayotumika hapo; si ajabu NHC ndio wakapoteza income.
 
Kwanini uvunje investments ambazo ni cashcows za shirika kisa tu ni prime area. Badala ya kutafuta maeneo ya wazi utanue jiji kama una hiyo mitaji.

Hizo ndio akili za investment za watanzania kupenda mambo rahisi. Serikali imewapa hela ya kumaliza mradi wao wa Kinondoni na Kawe apartments; kwanini wasisubiri iishe wapime occupancy rates ya hiyo miradi kabla ya kuruhusu upuuzi mwingine.

Ni mipango ya ovyo mno; kwa sasa NHC inapata 100% revenue ya hayo majengo, si ajabu baada ya uwekezaji wa ubia kila kitu kikikiisha mapato yakawa chini baada ya kukagawana na mwekezaji.

Hakuna la maana hapo zaidi ya uwekezaji, halafu kuondoa biashara 1000 ambazo zinalipa kodi kiasi gani unapoteza serikali, kiasi gani cha hasara unaweza zipa Bank, familia ngapi unazipa umaskini.

Huyu mama anachezewa sana na mafisadi, 2025 nyumba yake ya uraisi anayostahili kujengewa na serikali huko Kizimkazi au popote alipochahua tuakikishe ishaisha; hiyo kazi sio ya size ata kidogo tunalazimisha tu.
Nchi imekuwa ya hovyo sana. Mwenye nyumbani anataka kuboresha nyumba yake hivyo anakupa notisi ya kuhama kwa mujibu wa mkataba wewe unakimbilia kwa Rais azuie uboreshaji ili wewe uendelee kuitumia!

Upuuzi mtupu!
 
Back
Top Bottom