Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Unyanyasaji wa vipi, terms za mkataba si wanazijua lakini..?
Wewe unaweza kwenda kukodi duka, ukawekeza kwenye furnitures, ulinzi, kwenda kukopa bank na kununua inventory; kama unajua baada ya miezi mitatu mwenye jengo baada ya miezi atakuja kukutoa.

Ndio maana kwenye mkataba wa biashara kuna kitu kinaitwa ‘customary term’ hiyo ni implied term ambayo mahakama itaizingatia ata isipokuwa expressed kwenye mkataba.

Logical inatumika kuangalia uhalisia wa scenario, uwezi kuvunja mkataba hasa wa kibiashara kiholela bila ya fidia.
 
NHC wakitoka hapo K/koo wahamie pale Fire wavunje yale majengo yote ya kikoloni, wajenge malls.

Kanjibhai wakahamie kando ya mji kama chanika n.k sio kukaa K/koo,posta na upanga tu.

Pia hii barabara ya kutoka fire kuelekea muhimbili kuna majengo mengi ya kizamani yanatakiwa kuvunjwa na kujengwa malls na maeneo mapya ya makazi.

Kwa utawala wa Mama Samia, Dar-es-salaam inaenda kuwa kama Dubai.
 
Wakubwa wana pesa za kusimamisha kitu hapo sio cha kawaida !!

Bear in mind sehemu hiyo ni hotcake kwa biashara !!
 

Kama pako vile kuna biashara hio uliosema ww.je pakiwekwa kisasa zaid?huoni kua ndio idadi itaongezeka
 
Vipi eneo likuwa lako usingeliendeleza?
 
Hayo ni mawazo yako.Mimi ninasema ukweli. Ukiona huo ukweli ni negative kwako,pole .
 

Nakazia hapo.dsm inatakiwa iwe ya kisasa zaid majengo ya kizamani yabaki bagamoyo na zenji [emoji28][emoji28]hatuitaji magofu tena
 
Kama pako vile kuna biashara hio uliosema ww.je pakiwekwa kisasa zaid?huoni kua ndio idadi itaongezeka
Wewe ndio umesema hivyo, lakini hakuna justification.

Unajuwa kwanini China supermarket za kigeni nyingi sana tena zenye majina makubwa zilifeli.

Kwasababu wachina wenye maisha ya kawaida washazoea kufanya manunuzi yao yote kwenye masoko ya mlundikano kama Kariakoo na yapo prime areas; serikali yao aitoi hayo maeneo kwa mtu yeyote.

Sasa wewe unajuaje hao watafanikiwa, wakati atujui hata hiyo PPP model itakayotumika hapo; si ajabu NHC ndio wakapoteza income.
 
Nchi imekuwa ya hovyo sana. Mwenye nyumbani anataka kuboresha nyumba yake hivyo anakupa notisi ya kuhama kwa mujibu wa mkataba wewe unakimbilia kwa Rais azuie uboreshaji ili wewe uendelee kuitumia!

Upuuzi mtupu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…