Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wawalipe fidia za loss of income kwa miaka kadhaa ndio watu wanavyofanya na gharama fixtures and fittings za maduka yao; sio kupenda mambo rahisi.

Yaani unachukulia poa tu kisa jengo mali yako utadhani watu awakutafuta hizo hela za kuwekeza hapo.
Kwani mikataba yao inasemaje? Kusoma hawawezi sasa hata kusikiliza hawawezi!
 
Nchi imekuwa ya hovyo sana. Mwenye nyumbani anataka kuboresha nyumba yake hivyo anakupa notisi ya kuhama kwa mujibu wa mkataba wewe unakimbilia kwa Rais azuie uboreshaji ili wewe uendelee kuitumia!

Upuuzi mtupu!
Raisi asipozuia wajiandae kulipa mabillioni ya fidia hao wafanyabiashara wakitafuta mwanasheria mzuri.

👋
 
Mbona walishindwa kuendeleza bilicanas ya mbowe licha ya kuivunja
 
Hivi ni NHC waliwaweka hapo au walijipeleka wenyewe tena kwa kubembeleza!
 
Wengi hapo wanawaza kukosa nafasi za maduka mradi utakapokamilika ,maana wataaanza kuomba kupangishwa kama wapangaji wapya. Hivyo Kuna uwezekano Wengi wakakosa Kwa sababu mkatabata baina Yao utakuwa umeisha,hivyo Kila atakayetaka kuwa mpangaji sharti afuate taratibu za Shirika ambapo utalipia miezi mitatu mbele halafu ndio uanze kulipia Kodi Yako ya Kila mwezi.
 
Biashara 1000 zinaweza kuwa zimeajiri watu wangapi kila duka. Ukishawatoa hao wenye maduka na wafanyakazi wao hao watu wanaenda kula wapi?

Haya tupe jibu wewe mwelewa?
Ebo hiyo siyo hoja, mwenye nyumba anataka nyumba yake! Hama kajenge nyumba yako ufanye hizo biashara zako!

Unafanya biashara kwa kutegemea nyumba ya mwenzako, ujinga gani huo!
 
Alokwambia kuwa nyumba za michenzani ni za kupanga nani? Tulivunjiwa nyumba zetu, zikajengwa flats na tukapewa flats kama mali zetu na documemts zote tunazo. Flats za serikali ambazo ni za kupanga ni zile za mwisho kumalizwa kujengwa na mtoto wa marehemu Karume. Hizo labda wataweza kuzivunja ila kutoka block number 1 hadi 8 watahitaji kutupa compensation na kama flats za kilimani watajikuta na upinzani wa kqweli kwa sababu flats zile si mali ya serikali.
 
Watanuna sana hapo!!

Wazee wa dili waandike maumivu!!

Mama kaamua maendeleo yaende mkoani Dar anakodisha yote hadi ikulu ni makumbusho SASA na mwekezaji atawekeza!!

Wanaume wa Dar karibuni mkoani!!
 
Wanatwambia Mapato kutoka tril 31 hadi 67 bila kutwambia Matumizi ni sh ngapi na tutagawana shi ngapi ma DP
 
Kwani kulipia hiyo miezi mitatu mbele unadhani ni tatizo kwao Mkuu?Ikiwa Kodi zao wanalipa kwa Mwaka?

Hapo kinachowafanya wapate sintofahamu ni Issue za vilemba...
 
Ebo hiyo siyo hoja, mwenye nyumba anataka nyumba yake! Hama kajenge nyumba yako ufanye hizo biashara zako!

Unafanya biashara kwa kutegemea nyumba ya mwenzako, ujinga gani huo!
Umeishiwa hoja

Subiri waende mahakamani uone kama watatolewa.

Uwezi kuwa na mkataba wa kukodisha mtu shamba ata kama umesema unaweza vunja muda wowote. Ukifanya hivyo huyo mkulima ata shinda kesi hizo terms zako utaambiwa ni batili, uwezi kukodisha shamba bila mkulima kuvuna; hizo ndio customary implied terms za mkataba.

Kila industry ina customary norms zake ndio maana nakueleza unaropoka tu; subiri waende mahakamani uone kama serikali aitotozwa billions za fidia; huo muda ni mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…