Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Jambo la msingi ni kuweka bei kwa mwenye bidhaa hapo ndipo wenzetu wanatushinda kuandika namba ya simu bado haijendi uaminifu
 
Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi,siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona.Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka,vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia.Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hats bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
 
Natafuta chimbo la hardmaterial ya ujenz kama koleo,sururu,majembe,slesha,shoka n.k nmeangaika week nzma apa karkoo kila ninapooingia nagongana na bei za mkoan kwetu jana nmefanikiwa kuingia goodone lakn nmeambulia maumivu tu wanataka nichukue mzgo kuanzia 5m ...nmekimbia ! tafadhal mwenye uelewa wa hili swala ata kama n out na karkoo nitafata mali.
 
Earphones za jumla nimeambiwa kariakoo ni bei cheap mpaka 2000 unapata zile ambazo mkoani zinauzwa ghali mno hii ni kweli?
 
Kama ni Used vifaa vinapatikana karibu na stand ya mwendokasi gerezani..but kwa original ni mtaa wa msimbaz ukitokea fire...ila kwa hapa sijui chimbo lake exactly maana vifaa vya magari viko very complicated but kama ulikua ujui kabsa wanapouzia unaweza kucheki hayo maeneo niliyokutajia
Na mtaa wa lindi pia
 
Earphones za jumla nimeambiwa kariakoo ni bei cheap mpaka 2000 unapata zile ambazo mkoani zinauzwa ghali mno hii ni kweli???
Hizi earphone za 2000... Ni zile baada ya mda zina katika. Kuna za book jero, buku tatu, buku nne na kuendelea. Huwezi pata ofia kwa book mbili au nec au Samsung; wewe upo wapi nicheki kwa namba hii 0754660061
 
Ndio u
Natafuta chimbo la hardmaterial ya ujenz kama koleo,sururu,majembe,slesha,shoka n.k nmeangaika week nzma apa karkoo kila ninapooingia nagongana na bei za mkoan kwetu jana nmefanikiwa kuingia goodone lakn nmeambulia maumivu tu wanataka nichukue mzgo kuanzia 5m ...nmekimbia ! tafadhal mwenye uelewa wa hili swala ata kama n out na karkoo nitafata mali
Ndio utaratibu ulivyo boss.
 
Nimemaliza kupitia uzi huu. Kuna mengi ya kujifunza humu.
Baada ya hapa, ni kupambana ili siku moja nami frame yangu ijae.
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Watanzania wengi tungekuwa kama wewe mbona tungefika mbali, mwenzio akiwa na hali mbaya unafaidika na nini,hongera sana mkuu,we kweli Bongo bahati mbaya.
 
Kwa ujumla wafanya biashara wa Dar ni waaminifu sana na niwakalimu kuliko sisi wa mikoani maana ukituma pesa ikatokea mzigo uloagiza pesa imebaki utashangaa unapigiwa sm nakuambiwa pesa imebaki kias flani uamuz unabaki kwako uludishiwe au uongeze mzigo ,mm hii imetokea Mara kibao laki wauzaji wa jumla uku mikoan usishangae anakuibia ukiwa dukani kwake, Hongera zenu wauzaji wa jumla was Dar.
Dunia ya leo usipokuwa mwaminifu kwenye biashara utasubiri sana
 
Back
Top Bottom