Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Ninavyo vijora natoa mombasa nauza jumla ......ni pm nikuletee
 
  • Thanks
Reactions: Osu
Wakuu naomba kufahamu chimbo la viatu vya kike vya mtumba kama flats,sendo,slippers kwa bei poa
 
Habari wakuu! Jana nilitembea k/koo mtaa wa sokoni nilikuwa natafuta Vijora vya Mombasa kwa ajili ya biashara sasa si mzoefu ila bei niliyoikuta ni hii je ni sahihi au wapi naweza pata iliyopoa zaidi.

Vijora vyenye mtandio kwa 12000 jumla
Vijora bila mtandio 6000
Vijora vile vya Shiffon bila kamba 6000
Vijora vya shiffon na kamba 12000

Nikaelekea kitumbini hapa nilienda angalia vitenge nilikutana na hali hii ya bei;-

1.Java zile za china zisizopauka bei 20000 hadi 19500 hapa ni (oriental au Disco) nilivoshauriwa na wanaofanya hii biashara kuwa hizi brand ndo nzuri
2.Java no 2 ambazo ni brand nyingine au wanasema nyepesi bei ni 15000 hadi 14000

3.Nikaja wax hapa sikujua brand gani ni nzuri ila kuna dada aliniambia ANGEL ndo haichuji na kupauka huwa inatoka china ambayo bei ni 21000 hadi 20000

4.Wax no 2 ambazo hizi za moro na nyingine nyingi kuna za 10000 hadi 15000

5.Vitenge vya kawaida nikakuta na vile vya pc 2 kwa bei ya 7000 kwingine 5000 kwingine 6000. Nikauliza urafiki wakasema saaa hivi haifanyi kazi ko hawana mzigo wake

Nimeleta hapa ili kama kuna yeyote anafahamu wapi ntapata mzigo mzuri kw bei nzuri zaidi pia napokea ushauri kipi kibaya kipi kizuri kabla ya kufanya maamuzi ya kuingiza pesa.Karibuni sana.
Mie hapo nafaham kuhusu vijora ni kwel bei yake ndo hyo ila km unachukuwa pcs nying kwa wafanyabiashara wengine anapunguza anakufanyia 5500 visivyo na mtandio na 11500 vyenye mtandio.
 
Mie hapo nafaham kuhusu vijora ni kwel bei yake ndo hyo ila km unachukuwa pcs nying kwa wafanyabiashara wengine anapunguza anakufanyia 5500 visivyo na mtandio na 11500 vyenye mtandio.
Anhaa mfano vingapi hivi?! Atleast kidogo
 
Pia aina gani huwa markertable sana hope una uzoefu katika hii biashara!
Uzoefu sio sana ila nmepga hatua mie nauzia mikoan nauza sana vijora visivyo na mtandio na vyenye mtandio, ila nauza madera ya khanga na madera flani yanaitwa makhenz nachanganya na mitandio ya aina tofaut tofaut, ukitaka upge ha2a jitahd uuze jumla na rejareja utpga hatua kwa urahisi sana.
 
Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko, Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc. Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka kutype ah.
Viatu vya jinsia zote Au vyakike 2
 
Asalaaaaaaam wakuu

Za siku nyingi, nilimiss sana JF angalau sasa imerudi naenjoy maishaa kwa habr na updates mbali mbali

Km kichwa cha habari wakuu napenda kuuliza mtu ukitaka kufungua duka la cosmetics lile standard tuu la katii unatakiwa uwe angalau na mtaji kiasi gan?
Na ni masharti yapi au sheria ipi waga zipo za kufata pamoja na expenses zote za biashara hyoo ikiwemo lesen ya biashara
Nawasilisha wakuu mchango wako ni wa muhimu sana kwangu asante[emoji120] [emoji120] [emoji120]
Cont: 0769939879
 
Asalaaaaaaam wakuu
Za siku nyingi , nilimiss sana Jf angalau sasa imerudi naenjoy maishaa kwa habr na updates mbali mbali

Km kichwa cha habari wakuu napenda kuuliza mtu ukitaka kufungua duka la cosmetics lile standard tuu la katii unatakiwa uwe angalau na mtaji kiasi gan????
Na ni masharti yapi au sheria ipi waga zipo za kufata pamoja na expenses zote za biashara hyoo ikiwemo lesen ya biashara
Nawasilisha wakuu mchango wako ni wa muhimu sana kwangu asante[emoji120] [emoji120] [emoji120]
Cont: 0769939879
Kwa vile umeshaweka contact zako jilinde sana na watu wasiojulikana maana wataanza kucheki post zako za nyuma[emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom