Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale.Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Mkuu vipodozi vinapatikana wapi
 
Sasa umesema k/koo ndo vinachukuliwa vitu,unataka nini tena?
Wenyeji wa dar wasikupeleke k/koo? basi wenyeji wako wachoyo.
Naamini hata hao wenyeji wa Dar kama si wajanja kivile waishia kununua bidhaa kwenye maduka ya barabarani.

ukweli ni kwamba Kariakaa kuna machimbo ambayo hata wenye madox maeneo ya karibu huchukua na kuuza kwa bei ya juu.

Mfano kuna chimbo moja wanauza viatu vya kiume mfano Sebago pale wanauza Tsh 40,000 wakati huo ukipiga hatua mbili upande mwingine same sebago inauzwa 60 na maeneo ya pembezoni ni hadi 100K.

So ni kweli kuna haja ya wadau kujuzana machimbo.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana,miwani za Tiba wanauza waha kwa jumla ambapo hata shule hawakwenda.Wakati wenye profession wamelala kwenye ajira,unakuta jamaa anakupa mzigo hata kuandika jina kwenye risiti anambwela.Bongo wasomi wakishtuka biashara itanoga
Miwani za tiba, hao waha wapo wapi
 
Nimepata maswali mengi pm nijibu tu hapa kwa faida ya wengi sababu wengi wao ni wanataka kuanza biashara

Aina ya biashara
Fanya utafiti juu ya biashara unayotaka kufanya like km uko dar tembelea maeneo hata hapo kkoo jifunze vitu vidogo mf unataka kuuza nguo za watoto ziko design nyingi kuna ronya quality kidogo, quality ya Kati na ile quality kabisa pita madukani jifanye kuuliza hata bei soma lebo baada ya muda utajua kutofautisha. hii itakusaidia unaponunua ununue bidhaa inayoenda na pesa na isikupe tabu katika soko lako.

Aina ya wateja
Chagua aina ya wateja wako like maskini, hali ya Kati au matajiri!! Hii itakusaidia kujua watu unaodeal nao na hapo juu umeshapita kuangalia quality na bei sababu kila bei na quality ya nguo ina kundi lake katika Jamii

Location
Location ni muhimu sababu kila kundi katika
Jamii linapatikana sehemu husika so chagua kundi linaloendana na mazingira husika.

Aina za nguo
Kuna aina nyingi za nguo unaweza chagua aina unayotaka Kama vile nguo za watoto kipato cha Kati, nguo za heshima kipato cha Kati, nguo za kimalaya kipato cha Kati... Hii itakusaidia kupata kundi moja kwa wakati mmoja na kwa bei zinazolingana ina maana mteja akija kwako hatoki kirahisi..

Anza biashara
Ukifanya hizo key point kiufasaha anza biashara yako hutapata shida yoyote..

Mtaji.
Wengi wameniuliza kuhusu mtaji sh ngapi
Kwa mie mtaji ni pesa yoyote uliyo nayo as long as unahitaji kuingia kwenye kufanya biashara na si kujaribu biashara.

Mf
Mi nilikosa mtaji kabisa ilikua mwaka 2013 Oct na nilianza na laki na nusu na mzigo wangu wa Kwanza kufunga hapo kkoo ilikua urembo cheni, hereni, bangili na lipsick na huo mzigo niliuza kwa kutembeza na ulizaa 375000 na kupitia huo mzigo nikipata oda nyingi sana za nguo... Kwa pesa hio hio ilinilazimu nitumie usafiri wa kutoka moja kati ya wilaya za mpkani mwa tz mpk dar

Hapo nimetoa mfano tu wa mliouliza kuhusu mtaji.. Anza na ulichonacho kwa mfanyabiashara hakuna hela ndogo.
Muhimu fanya utafiti hata kama umeelekezwa kabla ya kununua fanya utafiti wewe mwenyewe iwe kkoo,, Uganda au nairobi.

Kwa Wale mlioniuliza pm naona nimewajibu
wote kwani kujibu mmoja mmoja siwezi..
Nimefaidika sana kwa Maelezo yako japo mtaji sina be blessed
 
Back
Top Bottom