Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wadau habari, nahitaj kufanya biashara ya modern jeans za kike na simple za kike vyenye quality nzur, naomba kufahamishwa chimbo zur kwa kariakoo juu ya hiz bidhaa..
 
Hizi earphone za 2000... Ni zile baada ya mda zina katika.. Kuna za book jero.. Book tatu.. Book nne na kuendelea.. Huwezi pata ofia kwa book mbili.. Au nec au samsung Wewe upo wapi nicheki kwa namba hii 0754660061
Iko hivo mkuu hizi earphone k/koo 2500 na ni jiwe vibaya mno
IMG_20180411_210648.jpg
 
Nakubaliana nawe na maduka yake yapo agrey na likoma i think..karibu na bank ya azania plus flash na phones accessories!wanauza bei rahis mno.

Dada nisaidie hivi wapi naweza pata kanzu kwa bei ya jumla,pili saa zile za mikononi za aina mbalimbali,cap zile za sasa na bidhaa za body spray? Ahsanteh
 
Natafuta chimbo la hardmaterial ya ujenz kama koleo,sururu,majembe,slesha,shoka n.k nmeangaika week nzma apa karkoo kila ninapooingia nagongana na bei za mkoan kwetu jana nmefanikiwa kuingia goodone lakn nmeambulia maumivu tu wanataka nichukue mzgo kuanzia 5m ...nmekimbia ! tafadhal mwenye uelewa wa hili swala ata kama n out na karkoo nitafata mali
Umeenda mtaa wa Gerezani? maana huko ndo material zote za ujenz kama tiles..alluminium poles..rangi..vifaa vya mabomba yote yapo huko!uliza watu wakuelekeze.
 
Dada nisaidie hivi wapi naweza pata kanzu kwa bei ya jumla,pili saa zile za mikononi za aina mbalimbali,cap zile za sasa na bidhaa za body spray? Ahsanteh
Kanzu zinauzwa kwa wingi msikiti wa mtoro!yaani katikat ya mtaa wa mchikichi na narung'ombe,

Saa za mkononi ambazo ni zile english Gold quality kuna wachina wanashusha mtaa wa mchikich kwa ndani ndani ulizia watu watakuonesha ukifika hayo maeneo

Cap za kisasa kuna maduka ya katikat ya congo na msimbazi!yaani karibia na DDC kuna maza mmoja anauza hapo yaani karibia wafanyabiashara wa kofia wote wanaenda kuchukua hapo

Body spray nazo zipo mtaa wa mchikichi sio kwa nje ni kwa ndani unaingia vile vijimtaa utaziona.
 
Charty bidhaa kama T-shirt za manga au hot basic kwa jumla bei simpo ninaweza kupata maeneo gani mkuu?

Nataka nipate mzigo then niziprint halafu niziingize sokoni..
Tatizo machimbo ya bei rahisi ndo siyafahamu..
Na jeans na raba Pia kama unafahasmu..
Kuanzia jins quality..cheap...form six na hizo tshirt za manga wengi wanachukulia kwenye maduka karibia na wanyama hotel kariakoo..yaani hayo maduka yapo kwa ndani ndani unazama huko utapata bei za jumla!hayo maduka yapo kati ya mtaa wa congo na nyamwezi hakikisha unazama ndani ndani siyo nje.
 
Miwani za wapi wanauza Jumla, tuelekeze kamanda
Miwani za kibishoo..za kusomea..za frame maduka yake yanapatikana mtaa wa mchikichi karibia na msikiti wa Mtoro pia ukivuka ule mtaa wa livingtone na mchikichi kama unaenda kutokea barabara ya lumumba!wanauza bei za jumla na rahisiii.
 
Kanzu zinauzwa kwa wingi msikiti wa mtoro!yaani katikat ya mtaa wa mchikichi na narung'ombe,

Saa za mkononi ambazo ni zile english Gold quality kuna wachina wanashusha mtaa wa mchikich kwa ndani ndani ulizia watu watakuonesha ukifika hayo maeneo

Cap za kisasa kuna maduka ya katikat ya congo na msimbazi!yaani karibia na DDC kuna maza mmoja anauza hapo yaani karibia wafanyabiashara wa kofia wote wanaenda kuchukua hapo

Body spray nazo zipo mtaa wa mchikichi sio kwa nje ni kwa ndani unaingia vile vijimtaa utaziona.
Doh nashukuru dada wacha nitachimba huko asee
 
Huu uzi umeenda vizuri hadi raha tuendelee kusaidiana tu kuelekezana inapendeza zaidi,samahani niliochelewa kujibu quote zenu!tatizo sikuhizi sipati notifications za jf!!![emoji52]
Be blessed charity. Amani, watu wengi sana waliokuwa na shida za kuanzisa biashara lakini hawajui hizi taarifa umewasaidia sana.

Naamini hata wenyeji wa dara, majority of huwa hawafahamu haya machimbo.
God bless you too.

Ila for sure kuna haja ya kutengeneza network, hasa na wewe. Sina wasiwasi na uaminifu wako. Sina hata kidogo. Ili mtu wa mkoani kama atashindwa kuja, basi akutumie wewe. Aku-facilitate na kisha umchukulie mzigo na kumtumia.
Hii sio kwa wakati ukiwa dar pekee, hata ukienda Nai pia, we can do the same.

Kizuri zaidi, hawa wa mikoani ambako wewe huna biashara they cant be your competitors.

Alternative ya pili, ni kutumia wale wa mikoani ambao wako interested, kufungua nao Kampuni. Then DSM inakuwa kama HQ, na ofisi za mikoani zinakuwa kama Branches.

Then mwisho wa mwaka Mnajadiliana kwenye faida.
GOD BLESS YOU CHARTY
 
Iko hivo mkuu hizi earphone k/koo 2500 na ni jiwe vibaya mnoView attachment 741609
Namba yako muhimu mkuu.
Vipi, kuna uwezekano wa kupata mzigo mabaki ya vifaa vya simu inayouzwaga kweny vi-sulphate? Kuna mtu aliniambia zinapatika kwenye maduka yaliyo opposite na Shule ya Uhuru. am not sure kama ni kweli. Confirm pliz
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale.Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Charty,
Na wapi vinapatikana viatu vya kiume quality kwa bei ya jumla?
 
Mtaji wa masikini umekuwa si nguvu zake mwenyewe tena,bali umekua ni uaminifu wake mwenyewe,ukiwa mwaminifu hata mimi naweza sema mkuu chukua hii milioni moja kazungushe biashara ukipata utakuja kunirudishia,mfano siku hizi **** biashara ya internet yaani networking ila huwezi amini wabongo wengi wanaofanya hii biashara wenfi ni matapeli,anauza kitu mtandaoni ukimpa tu pesa kwanza basi umekwisha,sasa sidhani makampuni makubwa kama amazon yangekuwa hayana uaminifu sijui kama yangefika hapa leo,maana unatuma pesa wao ndio wanakutumia mzigo,na wanautuma kwa uhakika kabisa.
 
Wanajamvi naomba kujuzwa mtaa ambao kuna maduka ya SAA za mkononi kwa bei ya jumla.. SAA za bei ya chini 2500, 3000 za kike na kiume. Msaada please
 
Nenda maduka yalio zunguka DDC kuna duka moja lina saa za kutosha pia kkoo siku iz yamefunguliwa maduka mengi ya saa kama wewe n mtembez utayaona mengi
 
Back
Top Bottom