Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wakuu me nahitaji chimbo la dawa za kilimo kwa bei za jumla maana nmezunguka hapo K.koo naona bei zao ni bora hata Morogoro.
 
mkuu
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa. Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale. Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Mkuu Mungu akubariki sana na me mwaka huu nataka kuanza biashara hiyo unaweza ukanisaidia contact zako ili nikija Dar tuonane sisi watu wa mkoani hatujui machimbo uliyoyataja yalipo hivo msaada wako utakua ni wa muhimu sana kwangu plzzz
 
Wakuu ningependa kujua chimbo la vifaa vya viatu,kuanzia kamba,soli,makapeti ya viatu na rangi mbalimbali kwa bei ya jumla hapo k.koo
 
Huu Uzi ubarikiwe sana na Udumu daima.

Hakika Wakuu wote mbarikiwe.

Mafanikio nmeanza kuyaona.
 
Natafuta chimbo la hardmaterial ya ujenzi kama koleo,sururu,majembe,slesha,shoka n.k nmeangaika week nzma apa karkoo kila ninapooingia nagongana na bei za mkoan kwetu jana nmefanikiwa kuingia goodone lakn nmeambulia maumivu tu wanataka nichukue mzgo kuanzia 5m, nmekimbia ! tafadhal mwenye uelewa wa hili swala ata kama n out na karkoo nitafata mali

Jaribu Kwenda Kamaka
 
natafuta chimbo la hardmaterial ya ujenz kama koleo,sururu,majembe,slesha,shoka n.k nmeangaika week nzma apa karkoo kila ninapooingia nagongana na bei za mkoan kwetu jana nmefanikiwa kuingia goodone lakn nmeambulia maumivu tu wanataka nichukue mzgo kuanzia 5m ...nmekimbia ! tafadhal mwenye uelewa wa hili swala ata kama n out na karkoo nitafata mali
Jaribu Kwenda Kamaka
 
Wapi nitapata hii Swiss Gear back pack?

FB_IMG_15257657491239437.jpg
 
Wakuu,
Wapi lilipo chimbo LA bei chee kwa CD za season,action kwa bei ya jumla zilizotafsiriwa.

Natanguliza shukran
 
Vifaa vya stationery:

Paper reams, Counter books, Daftari, Peni, Stappler machine, Soll tapes, Cards, Frame, Files na vingine vingine vya stationery.

Niomba kujua chimbo lake ambako vipo kwa bei ya punguzo.
 
Back
Top Bottom