Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wakuu ni chimbo zipi Kwa katolo wanafungua mitumba gred one nguo za kina Dada na akina mama na Kwa upande Wa Geita pia ni wapi hufungua hizo belo za gred wajuzi na wenyeji naomba kuelekezwa machimbo ya mitumba gred ,Asante
 
Chimbo la jeans za kike, vyupi vyupi na bra msaada.
 
Hivyo vitu vyote unavyovitaka vinapatikana mtaa wa mchikichi na sikukuu kuna maduka ya wachina na wakinga, hapo mchikichi kuna duka maarufu la VICTAN la mchina ambapo asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanaenda kuchukua chupi,vest na boxer quality za cotton kwa bei ya jumla mtaa wa Mhonda na msimbazi,yaani ukifika kituo cha mwendokasi Msimbazi B ingia kushoto kwako kuna maduka ya nje na ya ndani utakutana na chupi za kila aina ambazo pia mara nyingi wanaenda kuchukua kwa huyo Mchina wa Mchikichi, Wasomali na hao Wakinga.
Nimefanikiwa kwa karibu 85%, na duka nishafungua, na biashara inaenda poa, ndani ya wiki moja tu nimeuza karibu 1m, na hapo faida si chini ya 250k, nasimama mwenyewe golini kwa sasa, ctaki kuajiri muuzaj maana bado pachanga, kwa nionavyo biashara imeanza kwa mwanzo mzuri, nilichukua mzigo wa 6m. Shukrani sana kwa Charity na wadau wengine walojitolea kutoa madini kiuhalisia bila kuweka chai.
 
Nimefanikiwa kwa karibu 85%, na duka nishafungua, na biashara inaenda poa,ndani ya wiki moja tu nimeuza karibu 1m, na hapo faida si chini ya 250k, nasimama mwenyewe golini kwa sasa, ctaki kuajiri muuzaj maana bado pachanga, kwa nionavyo biashara imeanza kwa mwanzo mzuri, nilichukua mzigo wa 6m. Shukrani sana kwa Charity na wadau wengine walojitolea kutoa madini kiuhalisia bila kuweka chai.
Hongera sana mkuu
 
Nashukuru sana, J3 najiandaa nikakate leseni ya biashara na kulipa mapato, maana nilianza kibishi bishi tu bila kufuata utaratibu, wasije wakanibananisha.
Fanya hivyo mkuu kuepuka usumbufu.
Inaonekana umeweka location nzuri sana? Na vipi ni aina gani ya nguo unauza mkuu?
 
Vitambaa vingi vipo msimbazi/narung'ombe kuna maduka mengi ya washihiri wanauza jumla! Ila kuna vitambaa ambavyo ukifika kule hauvikuti lkn maduka ya rejareja wanavyo! Cjui sasa wanavipatiaga wapi! Hata Mimi natafuta hayo machimbo coz nmefungua duka LA vitambaa! Pls ukiyapata hayo maduka nijulishe kipenzi
Tandika
 
Ni kweli frem ipo site Kali balaa, niliiotea baada ya mtangulizi wangu kifilisiwa na haya mataasisi binafsi yanayokopesha,na kiujumla nauza zagazaga zote ndogo ndogo km,vyupi vya kila aina na kila bei, boxer, bra, skin tight, vitambaa vya kichwa/mitandio ya kila design, mashati ya shule,maushungi ya wtt wa shule,soksi za kila aina km za pundamilia, khaki nk,pia nauza leso, vest, bukta, underskirt na vingine vingine, vitu vyangu ni vidogo vidogo na vya bei ya kawaida na bei za kati, wadada, wamama na baadhi ya wababa akiingia dukan kwangu hatoki kavu bila kuchukua kakitu japo cha 2000,nawauzia pia baadhi ya machinga kwa bei ya jumla.

Hii kazi ina changamoto kiasi flani hasa kuzidiwa na idadi ya wateja na ukizingatia niko mwenyewe tu dukani,ckutaka kuweka MTU dukani ila sasa nalazimika kutafuta kijana mwaminifu nianze kumzoesha japo ctamuacha peke yake,na biashara ya nguo km ujuavyo mteja mmoja atataka kuchagua aina tofauti tofauti za bidhaa ile mambo ya lete na rangi ile nione mara size hii ndogo lete kubwa yake ni kawaida sana ktk biashara ya nguo,hapo bado hajaanza kuomba punguzo LA bei,unajikuta umezungukwa na wateja km wanne na wote ni wale wa lete na hio niione mara cjui nipunguzie,usipokua makini wengine wataondoka bila kulipa,ningeweza kumwambia wife aje tusaidiane ila yy nimemuachia ofic nyingine asimamie.ni hivyo mkuu
Fanya hivyo mkuu kuepuka usumbufu.
Inaonekana umeweka location nzuri sana?na vipi ni aina gani ya nguo unauza mkuu?
 
Back
Top Bottom