DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kama Watu wanathubutu kukaangia chipsi mafuta ya transformers, unadhani hao ni Binadamu halisi?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Ahsante kwa taarifa lakini ngoja nishare ninachokijua kuhusu hii habari:

Kwanza kabisa matunda yote yanapokuwa kwenye uhalisia wake yani yakiwa kwenye mti wake yanakuwa na uwezo wa kutengeneza hormone au kichochoe kinachoitwa ethylene ambacho hufanya kazi ya kubadilisha baadhi ya vitu vilivyopo kwenye hilo tunda kama vile starch huwadilishwa kwenda kwenye sukari nyepesi yani simple sugar kama vile glucose n.k.

Sasa unapochuma hilo tunda maana yake imelitoa kwenye asili yake hivyo utahitaji hiyo ethylene ili matunda hayo yaweze kuiva kwa haraka na kwa wingi ingawa zipo njia za asili kama vile kuchimba shimo na kukoka moto ndani ya hilo shimo kisha zima huu moto na kisha weka ndizi zako na funika na majani ya ndizi na udongo kisha moto kidogo kwa juu na uuzima baadaye.

Baada ya siku sita ndizi zitakuwa zimeiva na hapo ni vitu viwili vimesababisha ziive, moja ni natural ethylene iliobaki kwenye ndizi pamoja na joto iliolitengeneza kwenye hilo shimo.

HIVYO HIYO ETHYLENE HAINA SHIDA
 
Na zile gari za embe pale mwandege zile embe za kazi gani? Hebu tupe elimu kidogo.
Embe moja juisi katoni mbili.
Soma boksi la juisi ujue vitu unavyokunywa na sisi kubungaa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.
Nasikitia zaidi wazazi waonywesha watoto wao juisi za viwandani.
 
Nikila ndizi za kuvundika napata kwikwi kali mno saiv ndiz zangu ni zile og zenye sukari nyingi na vidoti vyeusi waniata malindi
 
Hapa hapa mjini ila watu tunavuna
Nipo mjini ila kama shamba za leo leoπŸ˜‚
 
Mtaan wanaweka maparachichi mabichi na ndizi na kuzifunika. Ndani ya siku mbili zinaiva.

Secondary chemistry walituambia ili tunda liive linahitaji acetylene cpd. Inawezekana hapo Dar mnatumia industrial acetylene, badala ya natural inayotoka kwenye matunda yenyewe.
 
Inasikitisha sana akili za wabongo wengi
 
 
wacha uongo,
 
Hata ukifanyaivo nakwambia utakufa tuuu
 
Najibu Kama Mwl wa Kemia na Bailojia

'Etheneβ€˜ ndo huivisha matunda na imo kwenye mmea kama kichocheo 'phytohormone' ambayo kazi yake ni kuivisha tunda.

'Ethene' ama β€˜ethylene’ ni kemikali ogania kundi la hidrokaboni familia ya 'alkini'. Inapatika katika uasili na inaweza kutengenezwa na binadamu.

Miongoni matumizi ni kuivisha matunda: kiasilia na isivyoasilia (artificiall ripening).

Wafanyabiashara hutoa matunda shambani yakiwa bado mabichi, hii ina faida: usafirishaji na utunzaji. Muda mwafaka ukifika muuzaji atalazimika kuvundika ili matunda yaive na ndipo matumizi ya kichocheo hiki hutumika.

Kuivisha matunda isivyoasilia kwa kutumia kemikali ya 'ethene' kiafya haina shida; shida ipo kwenye vyanzo vya hiyo 'ethene'.

Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanazijua njia za asili za kuzalisha ethene na kuharakisha uivaji wa matunda k.v kutumia mbegu za maparachichi ambazo huzalisha ethene na kuharakisha uivaji wa matunda husika.

Maswali ya hii ni salama au sisalama, yako juu ya njia ya kuivisha matunda, vyanzo vya kemikali husika, inatoka wapi? Na namna ya kuitumia. Weledi wa wavundikaji uko vipi? Rafu ziko hapo!

Nashauri:
 

Attachments

  • Screenshot_20241015-002656.png
    102.9 KB · Views: 3
Biashara ya ndizi mbivu Imekuwa kubwa sana hivyo wauzaji wanaangalia faida na si afya ya mlaji
 
Sio kweli ndizi huivishwa haraka na parachichi kama huku Rombo wanakata Kata parachichi lililoiva kwenye Tenga la ndizi mbichi Hadi wakifikia Dar zimeshaiva kununua parachichi saa nyingine mbovu au za kuokota mgombani ni rahisi kuliko kununua hizo kemikali ambazo umeshindwa kudhibitisha lingine msiongee vitu kama hujui hata kemikali inaitwaje na wanawekea wap Kuna ndugu zetu wanategemea biashara hiyo kula kusomesha kuvaa na kuishi mjini kwahiyo usiwaharibie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…