Mpwimbe
JF-Expert Member
- Oct 13, 2023
- 455
- 818
Watanzania Sasa hivi njaa imekiwa ni kaliiii, ukijumlisha na tamaa kalintumekuwa watu wa ovyoooo.Hii ya leo imeniuma Sana hadi nimelia.....
Kuna watu wanaroho mbaya Sana.
Wafaanya biashara wa online wenzangu mnaelewa jinsi ilivyo kazi kumpata mteja 😭😭
Bas mwenzenu Mimi nafanya biashara online, Sina bidhaa Ila nikipta mteja baada ya kupost ndo nikamchukulie.
Sasa pale kariakoo nimewazoea baadhi ya WENYE maduka,
Maana nimekua mteja kwao kwa siku nyingi,
Hivyo wakati mwingine mteja hunipgia cm hello, nipo kariakoo nielekeze duka lako lilipo nikachukue kitu flan, hapo KUMBUKA nimepigiwa cm ghafla na Mimi nipo gheto
Sasa ili nisiikose hela bas namtafuta mwenye duka namwelekeza Basi mteja atfikaa hapo dukan na atachukua kile alichokitaka kwa Bei ambayo Mimi nauza.
Siku za mwanzo mwenye duka alikua muaminifu maybe nimesema hiki kitu ni 50,000 Ila dukan huuzwa 40,000
Basi mwenye duka atachukua 40,000 yake na 10,000 ataniwekea .
Sasa baade kila nikipta mteja wa ghafla bas nafanya hivyo, Basi mwenye duka akaanza kuniambia mteja wako alifika Ila hajachukuaa chochote, Mara ya kwanza nikaamini
Sasa ikajiludia Tena na Tena kila nikipata mteja huniambia alifika ila hajachukua chochote Ila nikimuuliza mteja kuwa vipi ulipata anajibu ndyo Ahsante nimeshapata sister.
Kwahyo zaidi ya Mara 5 muuzaji huniambia kila aliyefika hakununua
Huku wateja wote huludi kunishukuru kuwa walichokitaka wamepata
Leo tena mwenye duka akanifanyia hiv hivi
Nimelia Sana , nimelia mnooo
Jinsi nahangaika kutaafuta wateja Mimi nalia sana
Mungu anisaidie nipate office yangu.
Wengine wenye maduka yenu najua mpo humu, jamani mtuonee huruma.
Mimi ninamshukuru Mungu kwa haya, Moyo wangu unaumia jamani daah nahangaika sana
Kila mbongo amegeuka tapeli tapeli, janja janja nyiiingi za kishamba kabisa.
Uaminifu umekuwa sifuri kabisa anawaza kutapeli au kuiba kwa mtu.
Pole Mkuu, tafuta mfanyabiashara anayeelewa thamaninya kile nachofanya.