Wafanyabiashara wa online wenzangu mnaelewa jinsi ilivyo kazi kumpata mteja 😭

Kumpeleka mteja kwenye chimbo lako hesabu umeshampoteza
 
Yaani wewe ulipata wazo zuri la kufanya biashara ila kosa lako haufanyi kwa malengo.
Mteja anapokucheki halafu unamuelekeza aende kwenye duka mwenyewe huoni kwamba huyu mteja akitaka kuagiza kwa mara ya pili utakuwa umemkosa maana duka ameshalijua atakuwa anaenda mwenyewe siku zingine bila ya kukutafuta?Hapo utakuwa umemfanyia kazi ya bure mwenye duka ya marketing na atakuwa anaongeza mtandao wa wateja wakati huo wewe utakuwa uko palepale yaani kila siku utakuwa unaanza upya kusaka wateja tofauti kitu ambacho kitakupa stress na kuona biashara ni ngumu kumbe wewe mwenyewe ndio haujaipangilia.
Kumbuka kwenye biashara kuna wateja ambao huletwa na wateja wako wa awali uliowahudumia wanakutambulisha kwa ndugu na jamaa zao wengine ambao ndio watakuwa wateja wako wapya sasa hawa wote utakuwa unawakosa na wataenda moja kwa moja kwa mwenye duka.
Na kama unajua dili zako zinafanyika maeneo ya kariakoo kwa nini ukae mbali na kariakoo hapo inaonyesha bado haujawa serious na kitu ukifanyacho na haujajipanga.
 


Pole sana, Mungu yupo na anaishi.

Machozi yako na kilio chako anavisikia.

Umefanya vyema kujituma kuliko kuomba omba au kusubiri kutumiwa.

Asiyefanya kazi na asile

Umefanya kazi, ulipwe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…