Wafanyabiashara walioporwa mabilioni na Mwendazake kurejeshewa fedha hizo na Rais Samia

Umeshaamka kutoka kwenye usingizi mzito? Au ulikuwa nje ya nchi na hukuwa na muda wa kusoma mambo yaliyokuwa yanatokea humu nchini

Hivi umesahau kwamba Mo alitekwa nyara na jamaa zaake wakatangaza dau la bilioni moja na nusu pale atakapopatikan? Ule mchezo wa kuigiza?

Kama ni kweli walikwepa (na inawezekana sana) kwa nini hakuna ofisa wa TRA aliyepelekwa mahakamani kwa kusaidia au kuruhusu ukwepaji huo wa kodi?
 
Hakuna mtu aliporwa, hao ni wapiga dili haramu na wakwepa kodi kwa mgongo wa vigogo waliokuwa nyuma yao na walipata kile walichostahili kupata, ndomana hutawasikia wakitoka hadharani kuyasema Haya.

Mambo mengine ni mazito yangewekwa hadharani kuna watu husingewaheshimu tena,

Pia kila nchi unayoijua wewe sio kila jambo linapatiwa ufumbuzi mahakamani, zipo njia mbadala ambazo zimetumika kwa watu wengi tu ulimwenguni yakiwemo mauaji, kunyang'anya mali n.k
 
As'habu l'kahfi hao wamelala usingizi wa miaka mia tatu.
 
Zilienda wapi hizo hela? Isije ikawa walikula wengine halafu Kodi za wa wananchi wavuja jasho ndio ziwalipe
Hizo fedha zilijenga uwanja wa ndege Chato, Kivuko cha wasafiri Chato, ndege za serikali Chato, mbuga ya wanyama Chato, hospitali ya rufaa Chato, VETA chato na barabara za Chato. Ijapokuwa hizi fedha zilinufaisha kikundi kidogo cha wananchi, afadhali ilmradi zilitumika hapa nchini.
 
Mh, ni jambo jema lakini hayo asiyafanye kama yeye hakuwemo kwenye ile serikali na yeye alikuwemo na alishiriki
Yes; alikuwemo kwenye serikali lakini mabaya mengi yaliyofanywa na mwendazake yeye hakuhusika. Ndio maana ameamua kuwarejeshea fedha wafanyabiashara, kuwalipa mafao wafanyakazi wa vyeti feki na kumfunga jambazi Sabaya. Hivi ni viashiria tosha kwamba yeye hakuwa mmoja wa watenda maovu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Walikwapuliwa Tsh ngapi? Wanarudishiwa Tsh ngapi? Tutajuaje kuwa kiasi kinachorudishwa ndicho kilichokwapuliwa? Raisi asiyefata taratibu za nchi yake lazima alete maafa mbeleni.

Hata kama ni kweli walikwepa kodi, nani alithibitisha hilo? JPM? Moja ya udhaifu mkubwa wa serikali ya awamu ya 5 ni kupuuza taratibu na sheria tulizojiwekea kama nchi. Na haya ndo matokeo yake, watu wanaweza tumia mwanya pakafanyika ufisadi.

Mtu kakwepa kodi, badala ya kushtakiwa kisha mahakama imuhukumu unakwapua pesa zake.

Mahakama ingetoa hukumu kwa mujibu wa sheria, huo ndo utaratibu tunatakiwa kuufata. Kiongozi wa juu wa nchi alipaswa kuufata, kama walionewa mahakama leo ingethibitisha hilo, pesa zingejulikana ni kiasi gani, na kiasi cha fidia kingekuwa wazi.
 
 
Watakwambia Mwendazake alitenda wema akaenda zake 😁😁
 
Waliokula hizo Pesa ndio warudishe sio Kodi yetu itumike kuwa refund,sio sawa.
 
 
Ulikuwa unaishi Tanzania au Mars? Unaweza mahitaji Jiwe?
 
Mazito yapi ,Nani asiyemjua Jiwe alikuwa mwongo,katili na ambae alikuwa anasingizia watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…