Wafanyabiashara walioporwa mabilioni na Mwendazake kurejeshewa fedha hizo na Rais Samia

Samia anachofanya ni utoto na kushindwa kuwajibika, kwenye uporaji alishiriki na hakujiuzuru. Leo anataka kurudisha uporaji walioufanya awamu ya tano ambayo alikuwa no 2 kiutawala. Kama kweli hakukubaliana na uporaji kwanini hakujiuzuru? Sasa pesa za kurudisha anampora nani ni awarudishie walioporwa?
Huyu ni mnafiki tu anatafuta cheap popularity ili apewe kura za huruma.
Kama waporaji anawajua awafirisi siyo kuja kutupora na sisi ambao hatukushiriki uporaji alioufanya yeye na serikali yake.
Fikiria Kama JPM asingefariki, mama bado angekuwa kwenye serikali ya waporaji maana kakaa humo miaka 6 leo anajifanya kurudisha walichopora, kama alikuwa hakubaliani na uporaji angeejiuzuru.
Mimi sipendi uporaji walioufanya yeye na JPM.
 
Vipi mmiliki wa lile mjengo wetu tuliokuwa tunapatia burudani la Bilicanas? Naye awepo kwenye list.
 
Hongera Rais Samia, Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu ya baraka
Huwa napenda ile nyimbo ya TOT inayomkaribishaga jukwaani, Kuna ile tezi huwa wanasema "WAPO WALIOKUTWEZWA, JITIHADA ZAKO", For me Ssmia is the best president of our generation, kaipokea nchi ikiwa imegawanyika mnoo, haijawahi kutokea, ila anapambana kuiweka sawa, na itakaa sawa
 
Shida Mama ana shika hapa ana acha, ana hamia pengine. Hatuoni hitimisho la anayo yaanzisha.
Wapi hitimisho la maridhiano? Katiba mpya....
 
Wahusika wengi wapo akiwemo makonda SABAYA hapi na kina mnyeti wataifishwe mapesa hayo yarudi Kwa wenyewe
 
Rais Samia Suluhu siku akiondoka madarakani atakumbukwa kwa mengi aisee hataki kuona mtu yeyote yule kaonewa kwakweli mama anaupiga mwingi katika suala zima la kusimamia haki
 
Lakini sasa nchi ipo katika mikono salama ya Rais Samia Suluhu watu hawaishi kwa hofu tena kama zamani mama anasimamia haki na amani ya nchi yake
 

Waliporwa na magufuli au na serikali ya awamu ya tano?
 
Amin usiamini mpango ulishasukwa kitambo kwamba iwe mvua au jua lazima tuhakikishe kuwa Mbowe si mwenyekiti wa CHADEMA kwa namna yoyote ile,Rejea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019,Uchaguzi Mkuu 2022 na sakata la Wabunge 19.
Na si hilo tu bali Mwendazake alitaka kuua upinzani nchini Tanzania kwa maslahi yake binafisi. Hata wale wabunge wawili wa CCM (Hawa Gasia na Ally Kessy) walionyanganywa ubunge na kupewa CUF na CHADEMA, mtawalia, hawakuwa kwenye hesabu za mwendazake. Vinginevyo, nchi nzima ingekuwa chini ya CCM
 
WWewe
Wewe utakuwa mjinga uliezaliwa mwaka 2021 mwezi wa nne hivi ukatili wa lile jambazi unaenda kulishtaki wapi maana organ zote za utawala bora alizi paralyze akawa yeye ndio sheria yeye ndio msahafu.
 
Ukweli ndiyo huo.
 
Lakini sasa nchi ipo katika mikono salama ya Rais Samia Suluhu watu hawaishi kwa hofu tena kama zamani mama anasimamia haki na amani ya nchi yake
Bado majambazi huku Dodoma Mkurugenzi wa Jiji ananyanganya Mashamba yenye hati miliki kwa mtindo was asilimia za Jiji ujinga kabisa Jiji lini lilimilikishwa hiyo Ardhi wizi mtupu Hizo nisera za Waziri Jizi lililokuwa linataka Uraisi leave hizi pesa chafu za asilimia katika maeneo ya watu
 
Mahakama gani, wewe unaona hii nchi kweli ina mahakama au wewe unaishi Denmark.
 
Wafanyabiashara wa bureau de change Arusha wameporwa pesa zao kisa kikiwa utakatishaji.

Kaka yangu amelipa kodi mara mbili licha ya kuwa na vielelezo sahihi vya kiserikali, shilingi milioni 200.

Task force iliyofutwa na SSH ilikuwa ni mtindo wa maisha wa awamu ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…