Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Wafanyakazi 3 wa Uhamiaji wasimamishwa kazi kwa kosa la kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael

Mkuu hao askari wa uhamiaji hawawezi kumchukulia sheria mkononi kwa kumpiga wakati kuna vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya kushughulikia tuhuma zinazomkabili,ilitakiwa akamatwe na kupelekwa kwenye vyombo husika ili hatua za uchunguzi/ushahidi na kupelekwa mahakamani.
Bureaucracy/inefficiencies ya Uhamiaji ktk kutoa huduma zao, zina encourage corrupt tendencies kama hizo. Na hiyo kilichotokea ni matokeo tu....Sasa hayo ni yaleyale ya' create a problem, and pretend that you are sorting it out'....kazi iendelee.
 
Tapeli kaogeshwa maji na kugaragara chini ndo salama yake ingekuwa kakamatwa mtaani wangempiga vibaya hata kumuuwa.
Na huyo tapeli aache utapeli.
Nashauri Askari hao wapewe onyo kali kwani ni Kama walidhani mtu akiingia kwenye himaya yao ni halali yao hivyo walikengeuka. Wale wa magwanda ya kijani ni wajanja. Wanakushughulikia biila kukupa promo. Raia tuache kumpa tembo tano.
 
Kwa mimi naona wamewaonea matapeli yanaumiza sana wandugu au nyi nyi hamjawahi tapeliwa?
 
Ni mwanzo mzuri wa dalili za utawala wa sheria kurejea mahali pake.
Ahasante sana Kamishina!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni kweli wanayafanya hayo je udhaifu uko wapi? Ni dhahiri sheria zetu ndizo zenye shida
Wala hazina shida, tatizo ni kwenye kuthibitisha , unaweza tapeliwa pesa , ukamkamata alie kutapeli , shida inakuja kwako huna nyaraka za kuthibitisha transaction ni kwel ilifanyika

Hao wanao tapeli waanakili ujue ooh
 
Ule upuuzi waliomfanyia yule jamaa ni mambo ya kawaida kabisa jeshini. Sio haki hata kidogo.

Yule polisi mzungu alimuua kwa kumuwekea mguu shingoni George Floyd, na tukio lile linafanana kabisa na hili la hawa askari wa uhamiaji.

Angekufa yule jamaa ile ni kesi ya mauaji. Bahati mbaya ni kwamba kwa nchi hii polisi na jeshi ni haki kabisa kujaa wale wenye vyeti feki na waliofeli mashuleni, kwa mataifa ya dunia ya kwanza polisi na jeshi ni taasisi zenye watu waliofaulu mashuleni.
 
Lakn matapeli wanaumiza sana watu. Watu wamekufa kwa pressure watu wamejiua, wastaafu wanatapeliwa pension zao.

Mbaya zaidi hizi kesi za kutapeli zinapoteza muda tu mara nyingi wanaachiwa..
Kwani huyo ni tapeli? Tapeli ni yule anayekulaghai kukupatia huduma au kitu na mwisho wake akatoweka bila kufanya hivyo. Nadhani yule bwana ni middle man, hata Kama Hana vibali, lakini anafacilitate process ya upatikanaji wa hati bila wewe kusumbuka sumbuka. Kama mm sipendi usumbufu sumbufu natumiaga hao hao. Hata ulitaka visa mbona watu hao wapo wanasaidia watu.
But kitendo walichofanya askali wale Hakina tofauti na yule askali mzungu wa USA aliyemkandamiza Ben George Ford. Unaanzaje kujichukulia Sheria?
 
Mkuu hao askari wa uhamiaji hawawezi kumchukulia sheria mkononi kwa kumpiga wakati kuna vyombo vilivyowekwa kwa ajili ya kushughulikia tuhuma zinazomkabili,ilitakiwa akamatwe na kupelekwa kwenye vyombo husika ili hatua za uchunguzi/ushahidi na kupelekwa mahakamani.
True fursa imejileta yenyewe eti unaimwagia maji .
 
Lakn matapeli wanaumiza sana watu. Watu wamekufa kwa pressure watu wamejiua, wastaafu wanatapeliwa pension zao.

Mbaya zaidi hizi kesi za kutapeli zinapoteza muda tu mara nyingi wanaachiwa..
Hawa sio matapeli hawa ni vishoka na huwa na connection na baadhi ya wahusika. Wapo ofisi zote zente uchelewameshwaji wa mambo...wapo TRA, TANESCO, UHAMIAJI N.K UKIONA VISHOKA OFISINI KWAKO UJUWE WATUMISHI WAKO HAWAFANHI KAZI SAWASAWA . NDUGU HUJAPATWA NA SHIDA WA JAMBO LA HARAKA. HAWA JAMAA NI MSAADA SANA UKIWA NA DHARURA. ITAKUWA WALICHOMEANA WAHUSIKA
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi Idara ya Uhamiaji, imewasimamisha kazi wafanyakazi watatu kutokana na tukio la Askari wa Uhamiaji kutumia nguvu dhidi ya Alex Raphael Kyai kama video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Mei 30, 2021 Kamishina Jenerali wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala, amesema mnamo Mei 27 mwaka 2021, Idara ya Uhamiaji ilimkamata mtuhumiwa wa utapeli anayefahamika kwa jina Alex Raphael Kyai katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini mkoani Dar es salaam ambaye aliongozana na mteja wa huduma za pasipoti, aliyemtambulisha kama mkewe.

Aidha Dk. Makakala amesema baada ya mahojiano, ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwalaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka, pia mtuhumiwa huyo amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

"Idara ya Uhamiaji inakiri kutokea kwa tukio hilo na pia inalaani kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji tayari imechukua hatua za kinidhamu dhidi ya askari hao" amesema Dk. Makakala.

Sambamba na hayo, Idara ya uhamiaji inatoa wito kwa Wananchi wote wanaohitaji huduma za kiuhamiaji kufika wenyewe katika ofisi za Uhamiaji, pia Uhamiaji wanawahakikishia kwamba idara itaendelea kutoa huduma zake kwa weledi, uwazi na bila kutumia mtu wa kati ( Vishoka).

Aidha Idara ya uhamiaji imetoa onyo kwa yeyote ambaye atajaribu kujifanya kuwa Afisa wa Uhamiaji au Afisa wa Serikali ili kumsaidia mtu mwingine kwa maslahi yake binafsi hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria, Pia idara hiyo imewataka Watanzania wote kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya aina hiyo.

Pia soma; Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

nchi hii viwatu vilivyoenda depo kidogo tu hata miezi mitatu tu kama uhamiaji, vinajifanya vikakamavu na vina uwezo kutoa adhabu za kijeshi kwa raia ambao sio wanajeshi. wanajifanya wajuaji na kufanyia mazoezi maisha ya watu. binafsi huwa nawadharau hawa jamaa kiasi kwamba sidhani kama wana hadhi ya kuitwa askari wa uhamiaji. uhamiaji sio askari, hata mgambo bora kuliko wao, wao waitwe tu wafanyakazi wa ofisi ya uhamiaji. sio askari hao. wanaofuatia ni PCCB jinsi wanavyojifanyaga usalama wa taifa.
 
Nyie watu ni wajinga sana,hamueleweki mnataka nini mamlaka yoyote ifanye, taperi kafanywa vile ili funzo kwa Wengine, leo tayari taperi anaonekana ana haki kuliko wale askari, hapo mnatamani hata ikiwezekana aachiwe huru kabisa bila kupelekwa court
Labda ni matapeli wenzake ndio wanaomtetea huku. Hawa watu wanaumiza wewe wasikie tu.
 
Hilo jambo lingefanywa na Mzungu dunia nzima ingepiga kelele
 
nchi hii viwatu vilivyoenda depo kidogo tu hata miezi mitatu tu kama uhamiaji, vinajifanya vikakamavu na vina uwezo kutoa adhabu za kijeshi kwa raia ambao sio wanajeshi. wanajifanya wajuaji na kufanyia mazoezi maisha ya watu. binafsi huwa nawadharau hawa jamaa kiasi kwamba sidhani kama wana hadhi ya kuitwa askari wa uhamiaji. uhamiaji sio askari, hata mgambo bora kuliko wao, wao waitwe tu wafanyakazi wa ofisi ya uhamiaji. sio askari hao. wanaofuatia ni PCCB jinsi wanavyojifanyaga usalama wa taifa.
Anayesema Uhamiaji sio Askari hilo ni tatizo lake binafsi, Hao jamaa wanapiga mafunzo yao miezi 9 depo na wapo kamili kulinda mipaka ya nchi na vipenyo vyake, tuwe na heshima na majeshi yetu, Hili ndio jeshi lenye wasomi wengi zaidi nchini.
Hakuna aliyefyukuzwa kazi kati ya hao waliotoa doso.

PIC8.jpg
 
Back
Top Bottom