TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

Kifupi ukiona gari ya megendo imekataa kusimama achana nayo. Ongea na polisi wa check point waweke kikwazo.
Wale madereva ni sawa na mtu asiyetumia kondom kwa mwanamke wa bar ya Kinondoni.
Exactly.
 
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso. Walikuwa wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA wa Tunduma, Omary Mnzava amewataja watumishi watano wa mamlaka hiyo kikosi kazi cha fast track waliofariki ajalini leo asubuhi Jumatatu mkoani humo ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.
Hivi vifo vya kujitakia,wao ni task force,hawakuwa law enforcement,maswala ya kukimbizana na magari ya uharifu wapi na wapi?
Dereva wa serikali hana mafunzo ya kuendesha gari kk kukimbizana na wahalifu,hii ni kazi ya polisi ambao Wana mafunzo maalum,sasa utakuta hapo walivimba vichwa,wakamshinikiza dereva!kimbiza huyo,tukimpata tumuonyeshe.
Hawa vijana wa mapato akili hawana kabisa,wakiwa kwenye program ya kukamata magendo au upekuzi hijifanya kama "makomandoo"
Kuna jamaa walikuja speed na defender yao,wakanichomekea kwa mbele ghafla,nikawauliza Mimi nina Landcruiser Tena ina ngao ya chuma,je ningeipiga hiyo defender yao ubavuni wakaumia,ningekuwa na kosa!!
Poleni wafiwa,lakini mamlaka husika fundisheni vijana wenu waaache "vigilantism"wawe weredi kazi za kufukuzana na watu waziache kwa wenye ujuzi nazo
 
TRA inakimbizana na wafanya biashara haramu/magendo. Walishindwaje kutoa taarifa kwa polisi waliyokuwa doria kulifukuza hilo gari? Acha wapumzike watu wapate ajira maana kufukuzia magendo lazims uchoke hivyo yakubidi upumzike
Hao tra ni kamati ya roho mbaya plus majivuno kama wao ni special sana
 
Eeh 1Hz ikikubali gia unapepea tu manina 😅 kila ukitia kidonge bado inadai tu
Hawa jamaa wa TRA na NHIF sijui walikua na mkutano Dar? Maana nimekutana nao wengi njia ya dar-Moro weekend hii! Wanakimbizana na hayo ma-Landcruiser
 
Una kuta TRA wamenyoka na Boda. Unajiuliza akili zao zipo likizo Ama!
 
kama ni mpambanaji, na hujarithi chochote wala huishi kwa ajira... huwezi kuwafurahia hawa jamaa... kibaya hawakupi elimu wala kutaka kifanyike kilicho ndani ya utaratibu ili serikali ipate mapato... ni rushwa kwanza then ndo mengine ya utaratibu yafate.
Kabisa kuna baadhi yao jamaa ni wala rushwa wakubwa

Ova
 
Kwa mazingira ya kodi tanzania ili upate pesa lazima urisk hadi uhai sasa nikitoka chimbo either niondoke mimi au wewe kamwe sikubali pesa ipotee natoka tunduma mdogomdogo natanguliza tupu yenye turubai kama yangu ukianza kutoka naingiza gari uchochoroni unapita ukikuta ya mbele unaona iko tupu, ukiifuata najitahidi vwawa hauvuki nikikuhurumia sana senjele umebaki, kodi kubwa hata hazilipiki VAT 18% wapi na wapi, tukifika mbalizi nagadi kiaina hata wiki lakini lazima nifike nakoenda au nifie njiani na pesa yangu .
 
Mi sio trafiki, ila hawa jamaa wanaonekana walikua wana overtake wakakutana face to face.. maana wapo upande wa kulia.. yaan ugonge gari kwa nyuma uchakae hivo?
mkuu uso kwa uso vp..huoni lory limepigwa nyuma hapo..nau mbona gari ipo upande wa kushoto au mm sioni vizuri
 
Usifanye mchezo na pesa mtaji wenyewe niliupata kwa magendo ya mtumba burundi wewe umetoka chuo juzi unachomekea utake kunilipua wewe unasoma mimi narusha sigara kuanzia ndola hadi mlowo leo kindezi unichape kwa kalamu uliyokua unanunua shilingi mia moja big no weka kodi za kulipika uone kama silipi kikubwa nibaki na faida tu na wewe chukua chako kidogo unataka ubaki na faida kubwa kama mtaji ulitafuta na mimi wewe vipi
 
Labda tuendeshe punda ila kwa magari kuharibika ni kitu cha kawaida
Sawa lakini uwekwe utaratibu.. Kwa mfano, gari bovu likiripotiwa, lisikae barabarani zaidi ya 30mins. Ukishindwa kutengeneza ndani ya huo muda, livutwe na utalipia hizo gharama. Simple.

Nimewahi kukuta lorry kwenye barabara Jumanne, narudi Ijumaa bado lipo. Ndio maana nasema, barabara zisiwe garage.
 
Wewe niweze kutembea na bangi msumbiji hadi somalia, unishike kwenye sukari haiwezekani haiwezekani nishadhulumiwa hadi moyo unaganzi nasubiri kufa tu, weka kodi yakulipika kwa uwazi usiandae mazingira ya rushwa uone kama nitatembea na gendo mimi sio kichaa
 
Hayajakukuta.
Huo huo usingizi jiulize umesababishwa na Nini.
Kua uyaone au likizo ijayotembelea Mbozi
Mmmh inahuzunisha sana kuweka kipaumbele hayo mambo kwangu mimi chanzo kilikuwa kufukuzana(mwendokasi)hayo mengine ni deceiving.
 
Back
Top Bottom