TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso. Walikuwa wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Polisi imethibitisha.
R.I.P NDUGU ZETU
 
Hii ajali ya ajabu aisee! Sasa inakuwaje dereva anagonga gari kwa nyuma alikuwa haoni ama ni mambo ya mzizioloji 👻?
Kwa spidi ya "kukimbiza" + msimu wa baridi ya ukungu + ilikuwa saa 11 alfajiri wala sishangai kuivagaa gari nyingine nyuma. Halafu kama ilikuwa imesisimama ndio mbaya zaidi. Inshort waliuvagaa mwamba! Kama Cruiser imejipiga hivi, ingekuwa Passo sijui ingebaki nini.Scarry stuff,
 
Noma sana yani hapo paso ingebaki number plate tu
 
Back
Top Bottom