TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

TANZIA Wafanyakazi watano wa TRA wafariki dunia kwenye ajali

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso. Walikuwa wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA wa Tunduma, Omary Mnzava amewataja watumishi watano wa mamlaka hiyo kikosi kazi cha fast track waliofariki ajalini leo asubuhi Jumatatu mkoani humo ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.
ajali imetokea leo saa 11 alfajiri. Yani maana yake hawa watu mida ya saa 9 usiku walikuwa wazima kabisa, eti sasa hivi hawapo lah!!!!!!!!!!! aiseeeee!!!!!!!! tukanyage ardhi ya Mwenyeenzi MUNGU kwa nidhamu na adabu na tuishi kwa kuheshimiana bila ya kujalisha lolote wala chochote, maana hatujui muda wala saa.
 
Poleni ndugu , jamaa na marafiki.

Polisi,TRA,NEMC,TISS ,TASK FORCE ,Jifunzeni kwa haya matukio ,hakuna haja ya kukimbizana barabarani na kuhatarisha maisha! Nakumbuka ilishaletwa thread humu kuna gari la NEMC lilikuwa linafukuza Fuso ya Mchanga ,ikatokea ajali FUSO ikalamba bodaboda kama 10 hivi.
 
kwa nn wasingepiga simu polisi wao ndio wafanye utaratibu wa kuisimamisha hyo Gari? mana huwezi sema watakimbia watakimbilia wapi?
 
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso. Walikuwa wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.

Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA wa Tunduma, Omary Mnzava amewataja watumishi watano wa mamlaka hiyo kikosi kazi cha fast track waliofariki ajalini leo asubuhi Jumatatu mkoani humo ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.
Hao TRA wanacheza na mikoa ya Mbeya , Iringa wanaumia.
Wamuulize Mwamwindi, na Mkuu wa Mkoa ndugu yake Mwalimu aliyerudi kwao na umauti.
Natamani Sabaya angeetwa mitaa hii.
 
Hii ajali ya ajabu aisee! Sasa inakuwaje dereva anagonga gari kwa nyuma alikuwa haoni ama ni mambo ya mzizioloji 👻?
Mkuu binafsi najaribu kufikiria hili tukio lilivokaa landcruiser imegonga gari nyingine kwa nyuma sasa ukiangalia hiyo iliogonga ilivoisha ni balaa
 
We jamaa hii sayansi au sayanzi umeandika hapa 😅😅😅😅😅
Mkuu ni physics mkuu. Nafahamu kabisa wewe ni teacher wa geology. Ila imeniuma kati ya wale waliochmwa Dodoma wakidhaniwa ni wanyonya damu ni mwanafunzi wako.
 
Fuso ni kiroli...hiyo cruiser ingekutana na semi iko full loaded ingekuaje? Hili ni funzo kwa TRA, hii tabia ya kufukuza watu na cruiser zenu alafu mnapaki kwa mbele mkiomba risiti muache...hizo cruiser ndio zinakuwa hivo sasa, ata uyo fuso kawatega maksudi tu, wanakera sana hawa jamaa.
 
Si walikuwa mwendo
Wanafata mwendo wa gari ya magendo
Gari za magendo zinakwenda mzee

Ova
Hahahahah gari yenye msala unakuta ina 260kph wao wanapambana na 160KPH yao jamaa kawatoka akawauza😅
 
Hawajulikani kwa majina?
IMG-20210823-WA0009.jpg
 
Fuso ni kiroli...hiyo cruiser ingekutana na semi iko full loaded ingekuaje? Hili ni funzo kwa TRA, hii tabia ya kufukuza watu na cruiser zenu alafu mnapaki kwa mbele mkiomba risiti muache...hizo cruiser ndio zinakuwa hivo sasa, ata uyo fuso kawatega maksudi tu, wanakera sana hawa jamaa.
Jamaa atakuwa alikandamiza brake bila shaka yani jamaa anataka kuitolea ubavuni tu jamaa akamtilia brake zote jamaa wakajaaa mazima 😂😂😂af Fuso unaita kiroli labda ikiwa tupu ila ikiwa fully loaded ni mziki mwengine!
 
Back
Top Bottom